Rais wenu Nakubalika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wenu Nakubalika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shishye, Dec 4, 2009.

 1. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado muda kidogo nitarudi kwenu kuwaeleza historia ya mambo meeeengi mazuri niliyoifanyia nchi hii tangu nilipochukua madaraka hadi sasa ambapo namaliza miaka yangu mitano ya kwanza. Leo nitawakumbusha moja tu kwa haraka haraka, nalo ni TRL. Mnalikumbuka shirika hili lilivyokuwa 2005 na kabla ukilinganisha na leo?

  Kama waziri wangu Mkuu alivyokwisha kuwaambia, kupambana na ufisadi ni kitu hakiwezekani maana wana nguvu mno, na ndio wanaoiendesha nchi. Ukiwakorofisha tu nchi yote itakolapsi. Kwa hiyo niko makini nao sana kuliko niwakabili bora nisafiri nje ya nchi.

  TRL sasa hivi ina matatizo madogo madogo tu ambayo taarifa nilizopewa na waziri wangu (kijana mchapakazi huyo!) yatatatuliwa karibuni. Wanaoathirika ni wananchi wachache tu (kwani kuna watu wengi wanaotumia treni siku hizi basi?) ambao hawana jinsi bali kuvumilia haya yaishe.

  Shirika letu limeboreshwa sana hasa baada ya kuwakabidhi wawekezaji wenye fedha. Shida tu ni kwamba watanzania hawaridhiki hata uwatengenezee mazingira mazuri kiasi gani; ndio maana mie nimeamua bora nitalii nitulize akili.

  Watu hawataki kuongelea mazuri mengi niliyokwisha yafanya hasa hili la TRL, Richmond, EPA, ufisadi kwa ujumla nk badala yake wanaendeleza chuki binafsi kunifuatilia mimi na ziara zangu za nje. Kwa leo ni hayo tu.
   
Loading...