Rais wangu Samia, ukifungua milango usiondoe pazia!

MenukaJr

Member
Apr 24, 2021
50
128
Rais wangu, nimekusudia kuendelea kukuandikia kwa nguvu zangu zote. Ninafanya hivi kwa utambuzi kuwa haya ndio mapenzi yangu kwako, ndio wajibu wangu wa msingi kama Mwana-CCM na Mwananchi mwema wa Tanzania. Wakati wa JPM nilifanya kazi hii kwa kiwango kizuri, licha ya masimango niliyoyapitia, usariti niliovishwa lakini nina fahari kubwa kwamba niliyoyashauri wakati ule bila kuzingatiwa yamegeuka mwiba nyuma yake. Hii inanipa ujasiri kwamba hata sasa nisiposikilizwa, baada ya kuondoka kwako ushauri wangu utakua na maana kubwa. Ni heri unisikilize sasa nikikukosoa na kukusahihisha ili baadaye tusije kulia na kujuta pamoja.

Rais wangu, video moja ilizunguka (siku za nyuma kidogo) katika mitandao ikikuonesha wakati unazungumza na wafanyabiashara wa Tanzania uliokutana nao Kenya wakati wa ziara yako huko. Katika mazungumzo yako hayo, mwisho ulisema unakwenda kufunguka. Ukarudia, unakusudia kuifungua nchi. Hewala!! Kuifungua nchi iliyofungwa ni jambo jema sana lakini kuifungua nchi iliyofungwa kwa uangalifu ni jambo lenye kuhitaji hadhari kubwa zaidi. Hii ndio sababu nakuomba utakapokuwa unaifungua nchi yetu, tafadhari fungua kwa tahadhari usiondoe pazia.

Rais wangu, wakati unazindua kitabu cha Mzee Mwinyi "Mzee Rukhsa" ulinukuu ukurasa wa 233 na 234. Ulisema, "ukifungua madirisha kuruhusu hewa safi kuingia ndani ya nyumba aghalabu Nzi, Mbu na vumbi huweza kuingia. Misamaha ya kodi iliyotolewa kuvutia uwekezaji na biashara ilitumika vibaya na baadhi ya wajanja".

Rais wangu, ni bahati mbaya kwamba wale wajanja waliozungumzwa na Mzee Mwinyi katika Kitabu chake bado hawajakwisha hata leo, baadhi yao ndio wale waliomchukia JPM na wanaokushangilia wewe kwa sasa. Kushangiliwa na adui yako mwanzo wa safari yako ni hamasa ya kupotea njia. Uamuzi wote ni wako, kufungua milango yote na kuondoa pazia ili waingie kwa uhuru wautakao au kufungua milango na kuacha pazia kwa uangalifu ili waingie kwa kufuata utaratibu tuutakao. Kupotea njia wakati wa kwenda ni bahati mbaya lakini kupotea njia wakati wa kurudi ni ujinga. Tujifunze kutoka kwa Mzee Mwinyi!

MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
 
Nchi yetu inasheria tulizojiwekea, na pia tunaweza kuzibadilisha au kuzifuta kabisa ili kwenda na wakati.Raisi Samia afungue Nchi tunataka Ajira au mnafurahi watu wanatoka Chuo wanashinda Vijiweni?
 
Nchi yetu inasheria tulizojiwekea, na pia tunaweza kuzibadilisha au kuzifuta kabisa ili kwenda na wakati.Raisi Samia afungue Nchi tunataka Ajira au mnafurahi watu wanatoka Chuo wanashinda Vijiweni?
Mkuu kwanza hongera swali ni kwamba sheria zilizopo zinafuatwa?kabla ya kuzidai mpya
 
Back
Top Bottom