Rais wangu, Ahadi ni deni! Vipi Computer zetu kwa Shule za msingi zimefika wapi?

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487

Kutokana na kuamini kwangu kuwa wewe ni mmoja wa wanajamii wanaopenda kuperuzi katika jamvi hili, nimeona kabla siku hazija yoyoma nikukumbushe kuwa kati ya AHADI rukuki ulizo ahidi wakati wa kampeni zako, kubwa ninalokumbuka ni lile la kumwaga Computer katika shule zote za msingi nchi nzima! Swali langu pamoja na kukaa chini kwetu madarasani! Je, Computer hizo lini tutazipata?
 
Walio ahadi kutoa msaada wamtosa ndiyo maana kila siku :msela:anapiga misele kusaka computer
 
huko mavyuoni tu hamna computer ndio ataweza kuleta huku chini? kwanza yeye mwenyewe alishasahau kama aliwahi kuongea kitu kama hicho.
 
Ipi ambayo ameshatimiza???...mimi naona moja ya UDINI na uchomaji makanisa ndio kafanikiwa kwa asilimia 80,hajui kua hiyo ishirini aliyobakiza itakuja kumcost .
 
ilikuwa ni password ya uchaguzi, hana haja ya kuhangaika na ahadi zake kibao, mbona hujauliza maisha bora kwa kila mtanzania! UNAKUMBUKA SUALA LA KUPITIA UPYA MIKATABA....
 
Majibu yenu yote yamekaa vizuri. Ili ujue mzigo wa ahadi alionao angalia kibonzo cha TWAWEZA kupitia Star tv. Kazi kwelikwali.
 
madawati tu ambayo gharama yake haifiki hata laki moja bado ni tatizo mashuleni leo computer kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiii hii ndiyo tz bhana
 
Bedui amerudi jana akitokea Oman, huenda hizo computer ziko njiani zinakuja na meli.
 
Hizo shule zina umeme?
Security ya hizo computer?
Waalimu?
Resources za kufanya reparing?
Mangapi ya maana aliahidi hajafanikisha?




Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Bwana mwalimu bado unasubiri ahadi ya computer? Hehehe, ile ilikuwa ni gia ya kuzipata kura zenu ninyi wanyonge
 
Back
Top Bottom