Rais wa Zanzibar, Dr. Shein: Mkitaka kuzima umeme zimeni, tutawasha vibatari

Heshima kwenu wakuu,

Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr Shein, amesema hatishwi na vitisho vya TANESCO vya kuikatia umeme Zanzibar kwa sababu ya deni la Umeme kwani deni sio la leo, deni lina zaidi ya miaka 20.



Amesema wote wanafahamu Zanzibar inadaiwa, na anaimani hamna anayeweza kuikatia umeme Zanzibar lakini kamawakitaka kukata wakate tu, tutawasha Vibatari.
View attachment 478694
Hatua hii imekuja baada ya TANESCO kutoa siku 14 kwa wadaiwa Sugu wa umeme kulipa vinginevyo watakaitwa umeme. Zanzibar inadaiwa deni la umeme zaidi ya Bil 121.

=======

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.

Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.

Dkt. Shein katika mazungumzo yake na vyombo vya habari alilezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema mkutano huo utaleta tija na faida kubwa kwa wazanzibari na watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii,uvuvi,ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.

Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya na ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.



Chanzo: ITV


DR SHEIN MAGUFULI ALISEMA YEYE HAJARIBIWI AMA ALIKUA ANATISHIA NYAU WATU WAZIMA ? HAYA SASA MAJARIBIO NDIO HAYO .KATA UMEME KAMA HUJARIBIWI.
 
Hivi mnakumbuka wakati wa kampeni,baadhi ya watu walizungumza kwamba magufuli anakurupuka,je ni sahihi sasa kukiri kwamba magufuli anakurupuka?

Karibuni tuchangie kama GT.

Sasa hapo unataka tuchangie ''ndio au hapana'' mkuu
acha chukii
 
The one who feeds you controls you...tuache mambo ya Russia n.a. Ukraine's
 
Namuunga mkono Dr Shein, tuko tayari kutumia vibatari. Ndugu Magu asitutishe kabisa , nafikiri Ndugu Magu hajuwi history ya hii nchi Vizuri !!
8e4a8479f394c0e9996bcc6a224b629e.jpg
Magu anahusikaje hapo?
 
Ndugu wanajukwaa,
Mtakumbuka ktk ziara iiyofanywa na Raisi Magufuli mikoa ya kusini alitueleza wananchi wa tanzania kupitia kwa waziri muhongo kwamba wadaiwa sugu wote wakatiwe umeme ikiwemo zanzibar ambao wanadaiwa takribani bili 161.
Kama tujuavyo kauli ya Raisi huwa haipingwi isipokuwa inatekelezwa,leo hii Raisi Shein naye kaijibu kauli ya magufuli kwamba wao wako radhi kukatiwa umeme kwa sababu deni hilo sio la leo lina miaka 20 na akaongezea kama wakikata basi wao wako tayari kuwasha vibatali na wala hakuna shida.

Sasa swali ni kwamba je kweli Zanzibar watakatiwa umeme kama tanesco walivyo agizwa?

Kama tanesco hawatakata je hilo deni litalipwa lini? na magufuli atawezaje kusahihisha kauli yake hiyo?

Hivi mnakumbuka wakati wa kampeni,baadhi ya watu walizungumza kwamba magufuli anakurupuka,je ni sahihi sasa kukiri kwamba magufuli anakurupuka?

Karibuni tuchangie kama GT.


Swelana
As usual ni sera ya kukurupuka na kutoa matamko tata kwa mtindo mmoja..........
 
Ngoja safari hii kupitia nishati ya umeme tuone nani mwenye nguvu kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Tanzania Visiwani.

Je Amiri Jeshi mkuu atasalimu amri kwa amiri jeshi wa KMKM??

"Zima umeme" inaweza kuwa sawa na kampeni ya "weka vyeti"??
 
Alipe deni tanesco yetu ijiendeshe hatutaki blah blah hapa
Kwanza lipa siasa baadae
Hakulipa tunakata
Kumbuka 14 days
Wewe ushalipa matrilioni unayodaiwa ya National Debt? Au Tanganyika haidaiwi? Mambo mengine mkae kisha mfikiri sawasawa. Ushawahi kusikia zanzibar imekopa bilioni kujenga Reli? Au barabara? Mnapoipa 4% ya Grants and aid kwani wao hawajui hesabu kwamba nyie mnabakiwa na 96? Mlipoamua kuungana hamkujua kama nchi yao ndogo lakini ilikuwa na mamlaka ya kinchi? Mnapokodisha eneo la bahari kuu kwa ajili ya uvuvi je una hakika Tanganyika ina bahari kuu. Haya mambo ni kaa la moto. Tanganyika ikitaka kupotea basi ijaribu gesturing kwenye Muungano. Huyo mtu wenu mwisho wake kunduchi tu, hata chumbe hayo maropo hayafiki.
 
Ngoja safari hii kupitia nishati ya umeme tuone nani mwenye nguvu kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Tanzania Visiwani.

Je Amiri Jeshi mkuu atasalimu amri kwa amiri jeshi wa KMKM??

"Zima umeme" inaweza kuwa sawa na kampeni ya "weka vyeti"??

Kwa upole wa Sheni amekwishasemmkikata wao hawana shida watawasha vibatali! Hataki kubishana,na hiyo ndiyo tofauti ya kiongozi na mtawala.
 
Back
Top Bottom