figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Heshima kwenu wakuu,
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dr Shein, amesema hatishwi na vitisho vya TANESCO vya kuikatia umeme Zanzibar kwa sababu ya deni la Umeme kwani deni sio la leo, deni lina zaidi ya miaka 20.
Amesema wote wanafahamu Zanzibar inadaiwa, na anaimani hamna anayeweza kuikatia umeme Zanzibar lakini kamawakitaka kukata wakate tu, tutawasha Vibatari.
Hatua hii imekuja baada ya TANESCO kutoa siku 14 kwa wadaiwa Sugu wa umeme kulipa vinginevyo watakaitwa umeme. Zanzibar inadaiwa deni la umeme zaidi ya Bil 121.
=======
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.
Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.
Dkt. Shein katika mazungumzo yake na vyombo vya habari alilezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema mkutano huo utaleta tija na faida kubwa kwa wazanzibari na watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii,uvuvi,ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.
Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya na ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.
Chanzo: ITV