Rais wa zamani wa Malawi Anyang'anywa Pasipoti Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa zamani wa Malawi Anyang'anywa Pasipoti Yake

Discussion in 'International Forum' started by TANMO, Jun 23, 2009.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Watanzania tunaweza kujifunza kutokana na hii habari ninayoweza kuiita njema....

  Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi amenyang'anywa pasipoti yake na tiketi yake ya ndege wakati akijiandaa kuelekea Uingereza kwaajili ya matibabu kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili nchini humo.

  Bakili Muluzi, alikuwa akijiandaa kusafiri kuelekea Uingereza kwaajili ya uchunguzi wa afya yake wakati maafisa wa kupambana na rushwa walipoamua kumnyang'anya pasipoti yake na tiketi yake ya ndege.

  "Tumeishikilia pasipoti ya Muluzi ili kumfanyia uchunguzi wa mambo mbali mbali" alisema Alex Nampota, mkuu wa kitengo cha kupambana na rushwa nchini Malawi (ACB).

  Muluzi alikuwa asafiri jana jumapili kuelekea Uingereza ambako amekuwa akienda mara kwa mara kwaajili ya uchunguzi wa afya yake.

  Mkuu huyo wa kitengo cha rushwa alifanikiwa kupata kibali toka mahakama kuu cha kushikilia nyaraka za kusafiria za Bakili Muluzi.

  Muluzi aliyeiongoza Malawi toka mwaka 1994 hadi 2004 anakabiliwa pia na tuhuma za kuiba dola milioni 12 toka kwenye mfuko wa misaada.

  Nampota alisema pia kwamba amefanikiwa kupata kibali cha kuchukua mali za Muluzi na kuzipiga mnada ili kuzirudisha pesa hizo iwapo Muluzi atashindwa katika kesi yake hiyo inayomkabili ambayo bado haijaanza kusikilizwa.

  Muluzi ndiye kiongozi wa ngazi ya juu sana kuchukuliwa hatua katika harakati za rais wa Malawi wa sasa Bingu wa Mutharika ambaye amedhamiria kutokomeza rushwa nchini humo.

  Muluzi kwa upande wake alisema kuwa ameshangazwa na hatua hiyo ya kumzuia kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji ambao hauwezi kufanyika nchini Malawi.

  "Sidhani kama nchi hii ingewafanyia marais wake waliopita vitu kama hivi" alisema Bakili Muluzi.

  Wakili wa Muluzi, ndugu Jai Banda alisema kuwa wataipinga hatua hiyo ya ACB jumatatu.  Huyo mnafki tu.. Kama huo ugonjwa angekuwa nao raia wa kawaida ambaye hana pesa za kwenda kufanyiwa upasuaji Uingereza ni haki yake kufa siyo?
  Kwa nini alivyokuwa rais asingefungua hosiptali hapo malawi ambayo ingekuwa na uwezo wa kumtibu yeye ili na wananchi nao wanufaike nayo?
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Bingu anaonyesha wasomi wanatakiwa kufanya nini kwenye siasa. Mambo yamebadilika sana baada ya yeye kuiongoza Malawi.
   
Loading...