Rais wa zamani wa Chama cha walimu, Gratian Mukoba achukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kagera

iu
Walivyojipanga kwenye hii picha ndivyo walivyoondoka..lupaso>Chato>mkuranga
 
Hii unataka kusema nini ili ueleweshwe vizuri, fafanua.
Kigezo kimoja cha commitment yake ni muda aliokuwa mwanachama na mchango wake pia. Watajitokeza wengi uchaguzi unapokaribia ambao nia yao ni kujiongeza value ili watamaniwe na vyama vingine.

Amandla...
 
Nitoke nje ya mada.

Hivi huu utaratibu wa kufunga kishikizo kimoja kwenye koti la vishikizo viwili huwa una maana gani? Na kwanini cha juu tu na si cha chini? Ni protocol ama ubishoo na/uhuni?

Kama hicho cha chini hakina kazi si fundi asikiweke tu
Una hoja mujarabu
 
Kigezo kimoja cha commitment yake ni muda aliokuwa mwanachama na mchango wake pia. Watajitokeza wengi uchaguzi unapokaribia ambao nia yao ni kujiongeza value ili watamaniwe na vyama vingine.

Amandla...
Uanachama wa Mkoba ni wa muda mrefu, ama kuhusu mchango wake ktk chama ni pamoja na uzalendo wake uliotukuka kwa taifa lake tangu alipoanza kupigania haki za wananchi katika eneo lake la kazi (walimu) huu ndo mchango wa thamani ktk chama kama huduma kwa wananchi.

Hata hivyo bado katiba ya chama iko upande wake. Mkoba hakuwahi kuwa na viashiria vyovyote vya unafiki wa upande ule hata pale alipolazimishwa kuunga juhudi akiwa rais wa cwt hakuweza kuwasaliti walimu kama ilivyotokea baada ya kuondoka kwake.
 
Hii ndio Taarifa mpya ya leo kutoka mjini Bukoba , kama ilivyosambazwa na Mwananchi Digital .

Zaidi jionee Mwenyewe

Kigogo wa zamani wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mkoba amejitokeza kuchukua fomu kuwania uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Kagera.

Mkoba, aliyewahi pia kuwa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), amechukua fomu hiyo, Machi 13, 2024 katika ofisi za Chadema mkoa wa Kagera zilizopo manispaa ya Bukoba.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa, Machi 15, 2024, Mkoba amesema licha kuhudumu nafasi mbalimbali, lakini alikuwa katika siasa, akisema siasa ni maisha huwezi kuiacha hadi mtu akifariki dunia.

Amesema kuanzia asubuhi, kuamka, kushinda, kutembea, kula na kulala ni siasa na unapofanya kazi pia ni siasa.
Ni mwanachama wenu wa muda mrefu au katumwa na CCM?
 
CHADEMA akili zenu mnazijuwa ninyi wenyewe na wakati ambapo zinashika mtandao mnajuwa wenyewe.ninyi si mlisema walimu wanatumika na kutumiwa na CCM? Si mlisema kuwa walimu siyo watu wa kuwaamini na hawafai kabisa hata kupewa jukumu la kusimamia uchaguzi kwa kuwa hawajitambui na wanafuata maagizo ya CCM? Si kila siku mnawatukana walimu? Sasa inakuwaje leo mnatoa meno yenu nje nje kwa kufurahia kigogo huyo kuwa chamani kwenu?

Aliyewaiteni ninyi nyumbu hakukosea hata kidogo.
Lini na wapi CHADEMA wametoa msimamo wao huo kwa maandishi au vyombo husika? Heche, Pambalu na Bony yai wote ni waalimu.
 
CHADEMA akili zenu mnazijuwa ninyi wenyewe na wakati ambapo zinashika mtandao mnajuwa wenyewe.ninyi si mlisema walimu wanatumika na kutumiwa na CCM? Si mlisema kuwa walimu siyo watu wa kuwaamini na hawafai kabisa hata kupewa jukumu la kusimamia uchaguzi kwa kuwa hawajitambui na wanafuata maagizo ya CCM? Si kila siku mnawatukana walimu? Sasa inakuwaje leo mnatoa meno yenu nje nje kwa kufurahia kigogo huyo kuwa chamani kwenu?

Aliyewaiteni ninyi nyumbu hakukosea hata kidogo.
Tafalari kabla hujaandika . Unatia kinyaa
 
Acha kachelo wetu akawazamishe nyumbu mtoni waliwe na mamba
Acha kudanganya, huyu tunamjua vizuri ni hofu yenu mnapokumbuka alivyowachachafya ccm akiwa Rais wa cwt mkimtisha hata kutaka kumtoa roho kwamba aachane na harakati za kudai haki za walimu au aunge juhudi.

Aliweza kuitisha mgomo wa walimu kudai haki za walimu baada ya ccm kupuuza maslahi ya walimu na alifanikiwa ingawa mlitaka ku "Mlimboka"
 
Sawa,mpeni nafasi anawafaa
 
Uanachama wa Mkoba ni wa muda mrefu, ama kuhusu mchango wake ktk chama ni pamoja na uzalendo wake uliotukuka kwa taifa lake tangu alipoanza kupigania haki za wananchi katika eneo lake la kazi (walimu) huu ndo mchango wa thamani ktk chama kama huduma kwa wananchi.

Hata hivyo bado katiba ya chama iko upande wake. Mkoba hakuwahi kuwa na viashiria vyovyote vya unafiki wa upande ule hata pale alipolazimishwa kuunga juhudi akiwa rais wa cwt hakuweza kuwasaliti walimu kama ilivyotokea baada ya kuondoka kwake.
Mimi binafsi ndio kwanza namsikia.

Amandla....
 
Back
Top Bottom