Rais wa zamani wa Burundi Jean-Baptiste Bagaza afariki dunia

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Bagaza-JEAN-Baptiste.jpg

Rais wa zamani wa Burundi Kanali Jean-Baptiste Bagaza amefariki akitibiwa nchini Ubelgiji.

Kanali Bagaza amekuwa akitibiwa kwa muda katika hospitali ya Sainte Elisabeth mjini Brussels.

"Imethibitishwa, rais wa zamani Jean Baptiste Bagaza amefariki dunia akiwa nchini Ubelgiji,2 ameandika mshauri wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe kwenye Twitter.

"Alikuwa seneta maisha.”

Kanali Bagaza aliingia madarakani Novemba 1976 kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Aliondolewa madarakani kupitia mapinduzi mengine yaliyoongozwa na binamu wake Meja Pierre Buyoya Septemba 1987.

Chanzo: BBC
 
raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. AMINA
 
Pengine alijutia madhambi yake na kutubu!
Amemfuata mwenzake maj. Gen Jean Bikomagu. Hawa jamaa walikuwa wanamwaga damu za binadamu kirahisi rahisi kama damu ya njiwa! Ndiyo maana Burundi inatembea kwenye laana ya umwagaji damu mpaka sasa kwa sababu ya misingi mibovu iliyowekwa na watawala waliotangulia kuitawala nchi hiyo.
 
Moja ya watu waliokuwa na misimamo mikali ya kikabila wakati wa Burundi Peace Negotiation.

Acha aende na mambo yake; Akwende
 
Pengine alijutia madhambi yake na kutubu!
Amemfuata mwenzake maj. Gen Jean Bikomagu. Hawa jamaa walikuwa wanamwaga damu za binadamu kirahisi rahisi kama damu ya njiwa! Ndiyo maana Burundi inatembea kwenye laana ya umwagaji damu mpaka sasa kwa sababu ya misingi mibovu iliyowekwa na watawala waliotangulia kuitawala nchi hiyo.
Mkuu jamaa wa aina ya bikomagu, buyoya, bagaza, kagame, mchambawima1, murutongore and the alike huwa sio wepesi kukiri makosa yao. Mara nyingi kuua mtu kwao ni sawasawa na kuua nyoka, bagaza wala bikomagu wala buyoya hawakuwahi kuomba msamaha popote pale iwe kanisani, msikitini wala kwenye majukwaa ya kisiasa. Kitendo cha bikomagu na buyoya kumuua raisi aliyechaguliwa kidemokrasia kabisa, kimeendelea kuiandama Burundi kwa laana kubwa. Raisi Melchior Ndadaye, muhutu wa kwanza kuwa rais wa Burundi kupitia sanduku la kura, alijitahidi sana kufuta na kusamehe madhambi yooote waliyoyatenda viongozi wa kitutsi. Ndio maana alimwita bagaza arudi Burundi baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka mingi. Shukurani ya bagaza kwa buyoya ilikuwa ni kushirikiana na binamu yake buyoya, Jean bikomagu na watusi wengine wakimtanguliza mbele muhutu François Ngeze kumuua rais Ndadaye. Hapo sasa msisahau mauaji ya hovyohovyo na ya kiholela waliyokuwa wanayafanya dhidi ya wahutu. Funga kazi ilikuwa mwaka 1972 na 2003 ndio waliamua kutaka kukimaliza kizazi cha wahutu kabisa. Wahutu ni wepesi sana kusamehe na kusahau ndio maana hata wanapopata nafasi za uongozi hawalipizi kisasi. Watusi walio wengi huwezi kuwatofautisha na makaburu wa afrika ya kusini. Kwa pamoja tumuombe mwenyezi Mungu wa haki, asiyehukumu kwa upendeleo, awape kile wanachostahili na awaweke bikomagu na bagaza pale anapoona panafaa kulingana na matendo yao walipokuwa bado wanaishi duniani.
 
Mkuu Vyuma edit hapo kwenye red, nadhani ulimaanisha Ndadaye!
Wahutu na Watutsi hata mimi nawafahamu, nimesoma nao tena wengi tu. Mhutu ukimuudhi ni mwepesi kukasirika na atakuonesha kwamba amekasirika lakini pia ni mwepesi kuachilia (kusamehe) na kuendelea na maisha bila kinyongo.
Lakini Mtutsi ukimuudhi atakuchekeachekea kumbe amekasirika vibaya mno huku akikutafutia muda na mahali muafaka aku-hit. Ni watu wenye vinyongo sana na hukaa navyo kwa muda mrefu mpaka alipize kisasi. Siyo wepesi kusamehe!
 
Back
Top Bottom