Analyst,
Mkuu kama upo kichwani mwangu yaani sisi na Tararilaaaa ndio umefika. Sisi kama viongozi wetu wote macho yako uchaguzi wa mwaka 2015, hali matatizo yapo leo tena ya kuua mtu..Inasikitisha sana kuona hata wale viongozi ambao wananchi wanawapa nafasi na matumaini wamekaa kimya ati wakijipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2015..wengine tayari wameisha anza kampeni zao hali uchumi wa nchi unazidi kudidimia siku hadi siku, maisha ya wananchi yanaendeshwa kwa imani tu..
Hata Wamalawi ambao wanajulikana kwa upole na layback, sasa hivi wamechukua maamuzi magumu sisi bado - Tararila tararila yaani hata sijui niseme kipi maanake watu wanakaa masaa 12 bila umeme, mbu ndio usiseme na hizo mbiu ambazo ni mafumbo kwa wananchi... Ebu nambieni jamani mbiu isemayo - BILA MALARIA HAIWEZEKANI! mnaitafsiri vipi nyie kama sii kusema hatuwezi kuishi bila malaria! mimi siku zote nashindwa kabisa kuelewa huwa wana maana gani...
Halafu ktk fikra za kukomesha malaria, JK katuletea vyandarua badala ya ku deal na mbu, ambao wamewezesghwa zaidi kuzaana kwa kusimama kwa maji bila mitaro, joto na giza (hakuna Umeme) kunaongeza muda wa mashambulizi ya mbu kueneza malaria maanake sii lazima uwe kitandani umelala...kisha wenyewe wanakwambia - Bongo Tambalale wakiwa na maana Bongo imezidi kuharibika!