Rais wa Tanzania 2015, Rais wa Tanganyika 2015, Rais wa Tanganyika 2025 na Rais wa Tanganyika 2025. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa Tanzania 2015, Rais wa Tanganyika 2015, Rais wa Tanganyika 2025 na Rais wa Tanganyika 2025.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Jul 22, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Baadhi ya watanzania hawataki kujifunza kutokana na makosa yao wenyewe. Wanatumia muda mwingi kweli kushabikia nani awe rais badala ya kutumia muda huo na juhudi zao kuwabana viongozi wetu watimize wajibu wao na kushinikiza waondoke madarakani kama hawawezi au hawataki kutekeleza wajibu huo.
  Hivi hamkumbuki mambo ya watu waliotamani kuwa rais yanavyoigharimu Tanzania mpaka dakika hii?. JK ni rais leo kwa kuwa alitamani kuwa rais na kujipanga akisaidiwa na wanamtandao wenzake kama EL, RA, SS, B.Membe, nk. Hawa jamaa walijipanga zaidi kujiremba ili wapendeze machoni pa watu na kuchafua wenzao ili waweze kuchaguliwa. Hata siku moja hawakuwaza wakiingia madarakani watafanya nini kuwasaidia wapigakura wao. Kama mnabisha chunguzenu utendaji na utekelezaji wa sera zao. Very poorly organised!
  Baadhi ya wanamtandao wanaendelea kuandaa kuchaguliwa kwao miaka ijayo na kwa ujinga wa baadhi yetu tuko busy kushangilia mara Membe, mara Sitta mara nani.....2015 wengine wanajipanga kutawala nchi kwa karne kibao kupitia vizazi vyao vijavyo na bado wanashabikiwa.
  Swali: Hawa watu wamefanya nini hata mkadhani wataweza?
  Ushauri: Kwa nini tusipime watu kwa uwezo wao na kushinikiza vyama vyao kuwapendekeza kwa staili ile ya CDM na Dr. Slaa. Naamini Mbowe anapenda kuwa rais lakini alipima umakini wa Slaa ambao umeonekana wazi na kusikia sauti ya umma na kumwomba agombee. Upande wa magamba naona mtu mwenyewe anaanza kutafuta fedha anaitumia kujitangaza na kuchafua wenzake kisha anataka aonekane anaweza.
  Mpaka dakika hii nawaogopa watu wanaotajwatajwa ndani ya magamba kwa kuwa ukweli ni wao wenyewe wanaotaka urais na si watu wengi wanawapendekeza.
  Wakuu naomba tulijadili hili.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  You a re a real analysit. Nimeipenda hii.
   
 3. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  tunahitaji watu wenye kufikiri vema kama wewe...
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,609
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  He is indeed a true analyst.Straight to the point right on the money....And indeed,i ma bank on this.
  Tusubiri waharibifu wa hoja.Kwa hakika watakuwepo maana ndiyo hao hao wenye maslahi.Wamejipanga kuchukua madaraka na wako kimaslahi zaidi.

  Back to the point,ni kweli tunahitaji tubadili mindsets zetu.Tujadili namna katiba mpya itakavyowawajibisha viongozi wetu ili ikiwa kweli wanataka madaraka wafikiri mara mbili mbili. kabla ya kujitosa,kutumia pesa zao,kuchafuana nk.

  Tunataka katiba itakayowabana ili wawajibike for the people!Katiba itakayowafanya wajiulize mara mbili mbli kutumia pesa zao kuingia madarakani kuiongoza nchi masikini kama yetu.Katiba yetu ni lazima iwe tofauti na katiba za nchi zilizoendelea.Tuanzie hapo.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Analyst,
  Mkuu kama upo kichwani mwangu yaani sisi na Tararilaaaa ndio umefika. Sisi kama viongozi wetu wote macho yako uchaguzi wa mwaka 2015, hali matatizo yapo leo tena ya kuua mtu..Inasikitisha sana kuona hata wale viongozi ambao wananchi wanawapa nafasi na matumaini wamekaa kimya ati wakijipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2015..wengine tayari wameisha anza kampeni zao hali uchumi wa nchi unazidi kudidimia siku hadi siku, maisha ya wananchi yanaendeshwa kwa imani tu..

  Hata Wamalawi ambao wanajulikana kwa upole na layback, sasa hivi wamechukua maamuzi magumu sisi bado - Tararila tararila yaani hata sijui niseme kipi maanake watu wanakaa masaa 12 bila umeme, mbu ndio usiseme na hizo mbiu ambazo ni mafumbo kwa wananchi... Ebu nambieni jamani mbiu isemayo - BILA MALARIA HAIWEZEKANI! mnaitafsiri vipi nyie kama sii kusema hatuwezi kuishi bila malaria! mimi siku zote nashindwa kabisa kuelewa huwa wana maana gani...

  Halafu ktk fikra za kukomesha malaria, JK katuletea vyandarua badala ya ku deal na mbu, ambao wamewezesghwa zaidi kuzaana kwa kusimama kwa maji bila mitaro, joto na giza (hakuna Umeme) kunaongeza muda wa mashambulizi ya mbu kueneza malaria maanake sii lazima uwe kitandani umelala...kisha wenyewe wanakwambia - Bongo Tambalale wakiwa na maana Bongo imezidi kuharibika!
   
 6. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Thanx for the complement Bro.
  Nakuunga mkono zaidi ya 100%. Imagine rais alazimishwe na katiba kuteua mawaziri+manaibu wasiozidi 20 na kulazimika kuondoka madarakani anaposhindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi. Taasisi ya Kupambana na Rushwa iwe huru na rais asiwe na mamlaka ya kumwandikia vimemo mkurugenzi wake, Usalama wa Taifa washughulikie maswala ya Intelligence na Security kwa weledi na si kwa siasa nk. Wabunge walipwe mshahara wa mwalimu wa sekondari na mambo mengi yenye manufaa kwa taifa zima. Katiba inapowabana watawala inasaidia watu wazembe na wajingawajinga kama hawa wa sasa wasithubutu kuhonga ili kupata madaraka.
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mkuu sina cha kuongezea umemaliza kazi kwao CCM
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Mkuu umetoa analysis murua ingawa title haiendani na ccontent. Sababu za magamba kupigana vikumbo kwenye post 1 tu ambayo inahitaji mtu makini ni
  1.Tanzania ni shamba la bibi. Hapo kila mtu anatazama tumbo lake
  2. Mtazamo wa kumalizana\kulipizana visasi kunakotokana na minyukano mikali ndan ya magamba kunakosababishwa na 1 hapo juu
  3. Udini. Hapa sitafafanua
  4. Prestige.

  Kwa hali hiyo hakuna mwanamagamba atakayeweza ku-meet expectations za wananchi pindi akiwa Rais na ndio hapo sasa CHADEMA wanatakiwa ku-capitalise ili kuiteka nji hii
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Thank u sana kwa analysis nzuri, I wish mchango wako ungefika vijijini na kwa kina mama wa uswazi; ambapo watu wanaexploit ignorance ya watu kwa manufaa yao!

  Pia post za kisiasa zipungue DC na RC, watu waaply post za uwaziri badala ya kuteuliwa toka kwa wabunge; hii itawafanya wabunge wawabane vizuri.
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Safi sana mkuu!
   
 11. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  You are so right! Watanzania wengi wenye uwezo wa kuelewa na kutafakari wanaweza kutoa mawazo mazuri na tukipunguza zile interest za makundi kama udini, ukabila nk. vilivyozidishwa na kauli za JK na vilaza wenzake tunaweza kupata katiba nzuri na ambayo watu watajivunia. Hofu yangu ni kwamba haitatokea nafasi hiyo kwa visingizio kibao ili Katiba iendelee kuwanufaisha wanaodhani watatawala nchi hii milele.
  Wakati wa uchaguzi wanadai wizara zinaweza kutekeleza shughuli zao pasipo uwepo wa mawaziri na manaibu wao. Sasa kama hili linawezekana kuna haja gani ya kuwa nao wengi + manaibu waziri?
  Natarajia kuandika mapendekezo ya namna ya kuiendesha serikali kwa kirefu kuzingatia hali ya umaskini wetu wa kujitakia na ushindani mkubwa kutoka kwa jirani zetu.

   
 12. u

  ugawafisi Senior Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  analysis imetulia ila sidhani kama watekelezaji wapo kwa sasa, elimu inahitajika zaidi kwani waTz hawajui viongozi wanaowahitaji ili tupige hatua na kuondokana na mifumo isiyokua na tija.
   
Loading...