Rais wa SMZ lazima uwe "Fisadi" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa SMZ lazima uwe "Fisadi"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Apr 24, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kuomba urais Zanzibar sharti kuwa na mil. 3/-

  MWANACHAMA wa chama chochote cha siasa kilicho na usajili visiwani hapa, anayetaka kuwania urais, atatakiwa kuwa na Sh milioni tatu ili aweze kupata fomu za kuwania nafasi hiyo ya juu nchini.

  Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza rasmi gharama hiyo na kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Khatib Mwinyichande, kiasi hicho kimepanda kutoka Sh milioni moja za mwaka 2005.

  Alisema wagombea ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, watachukua fomu kwa Sh 300,000, wakati wa usheha, watalipa Sh 50,000. Katika uchaguzi wa mwaka 2005, wawakilishi walilipa Sh 50,000 kwa fomu huku usheha ukilipiwa Sh 15,000 kwa fomu.

  Mchakato wa kuwania urais katika uchaguzi huo Visiwani hapa, unatarajiwa kufanyika kwa siku 20 kuanzia Agosti 10 mwaka huu.

  Mwinyichande alisema siku tano baadaye, itaanza ngwe nyingine, kwa ajili ya wanaowania kuingia katika Baraza la Wawakilishi. Mchakato wao unatarajiwa kuwa wa siku 15.

  “Kampeni za Uchaguzi Mkuu zitaanza Septemba 10 na kufikia kikomo jioni ya Oktoba 30,” alisema Mwinyichande aliyethibitisha kwamba, uchaguzi utafanyika Oktoba 31, siku ambayo nchi nzima ya Tanzania itakuwa katika uchaguzi.

  Aidha, ZEC inatarajiwa kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi huo Novemba 2, mwaka huu. Mwinyichande alisisitiza kwamba, ZEC iko katika harakati za kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa huru na wa haki.

  Wakati huohuo, kundi la Wazanzibari 12 wanaojiita 'Wawakilishi wa Watu wa Zanzibar’, liliibuka jana na kushikilia msimano wa kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wakidai kuwa “si halali na lazima utenguliwe.”  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, viongozi wa kundi hilo, Yussuf Mchenga, Amour Mbamba na Rashid Ahmed, walisema wanaendelea na harakati za kisheria kuhakikisha wanauvunja Muungano huo ambao keshokutwa unatimiza miaka 46.

  “Barua yetu tuliyoituma Umoja wa Mataifa (UN) imepokewa rasmi, sasa tunasubiri majibu kabla ya kwenda mahakamani. “Tunataka Mamlaka husika ya UN ithibitishe uhalali wa Muungano huu au iuvunje,” alisema.

  Ahmed alisema katika harakati za kufungua kesi, wanasheria wakuu wa Tanzania na Zanzibar, Katibu Mkuu wa UN kati ya mwaka 2005 na 2006, walishindwa kuonesha mkataba wa kuundwa kwa Muungano.

  Hata hivyo, wasemaji hao wa kundi hilo walikataa kueleza kilichomo katika barua yao UN na hata kueleza chanzo cha fedha inayowapa jeuri ya kutaka kufungua kesi dhidi ya Muungano.

  Katika hatua nyingine, wasemaji hao walimpongeza Rais Amani Karume kwa juhudi zake za kutaka kuhakikisha suala la mafuta na gesi ya asili visiwani hapa linaondolewa katika masuala ya Muungano.
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=6826
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I don't think that is the case. First of all no one becomes president from absolutely no where. They must have started off somewhere. By the time it reaches for them to run for president I don't think 3 million is a problem. Our MP's make more than that per month so what is 3 million to them? Also remember the money does not have to come directly from a person's pocket. It could be a donation from well wishers etc. I don't think any body who can't afford 3 million for the form would have reached the level to run for president. Mtazamo wangu tu.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama mtu hana hata mil 3, anafaa kweli kuwa raisi huyo?
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  What is 3mill? that peanut money you call it ufisadi! What kind of presida will you make if you cant even have 3mil!
  What a lame!!!!!!!!!
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  3Mil is 'fea' for presidency.
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  haya................
   
Loading...