Rais wa Russia: Sijawahi kumiliki Smart Phone

Still core code ni android ya google hata uicustomize vipi...
Sailfish pia imetengenezwa na jolla community ambao ni finish.... so hawako salama unless wa develope yao

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
Ndo nnachojaribu kusema hapa chifu .. Vitu vingi wanavyotumia wanajaribu as much as possible viwe vya kwao.. Especially vinavyotumiwa serikalini ama jeshini
 
Maisha siyo lazima smartphone......na ukitaka uishi katika uhalisia,kufikiri zaidi,na kuwa na mawazo huru lazima smartphone na teknolojia isiwe chaguo lako la kwanza....maana inapumbaza!
 
Anajua akitumia smartphone ni rahisi sana Marekani kumdukua.

Ila kiukweli smartphone sio salama kabisa katika maisha yetu na ndio maana Kwa Kiduku Kim Jong ndio nchi inayoongoza kuwa na Siri nyingi kwa sababu kule ni mwendo wa SLP tu.
SLP ndio nini mkuu
 
Anaona aibu kwa sababu makampuni makubwa ya simu ni ya kimarekani na hata haya ya nchi nyingine yanatumia IOS au android ambayo ni technology ya Mmarekani
 
Hapana sio wa ajabu. Mimi nina Mzee wangu mmoja hatumii kabisa smartphone. Anaweza kuwaletea watu smartphone kama zawadi lakini yeye hana. Akihitaji mawasiliano ya kimtandao anaazima simu ya mtu mwingine.
Kwa kuazima za wengine ina maana anatumia.
 
View attachment 693161

SINA simu ya smartphone,” ndivyo ambavyo husema Rais wa Russia, Vladimir Putin, kila anapoulizwa iwapo ana simu hizo za kisasa.

Licha ya kuambiwa kwamba “kila mtu ana smartphone mfukoni” huko Siberia, nchini Russia, wakati akiwa ziarani, kiongozi huyo pia aliwahi kusema kwamba hataki kutumia tovuti (website) na aliwahi kukiri kwamba mtandao wa Internet ni kimradi cha shirika la ujasusi la Marekani – CIA – na kwamba nusu ya kazi yake ni kuonyesha ngono.

Pamoja na kwamba watu wengi nchini mwake, wakiwemo wanafunzi, huchakarika ili kupata aina hizo za simu, Putin amefichua kwamba analitawala taifa hilo la watu milioni 144 bila kutumia smartphone.

Akiwa amekiri pia kwamba hapendi mambo ya technolojia mpya, amesema kamwe huwa hatumii Internet na kama ikilazimika, huwatumia wasaidizi wake kumtafutia kitu anachokitaka.

Putin mwenye umri wa miaka 65, alithibitisha kutopenda kwake masuala ya mitandao (apps) alipokutana na wanasayansi na wasomi huko Siberia ambako mkuu wa kituo cha uafiti wa zana za nyuklia, Kurchatov alimwambia kwamba “kila mtu ana smartphone mfukoni”.

Amesema pia kwamba hapendi kujiunga katika mitandao ya kijamii, kinyume na mwenzake wa Marekani, Rais Donald Trump, anayetumia mtandao wa Twitter kama silaha yake binafsi ya kisiasa.

Mwaka jana alipokutana na watoto wa shule, Putin aliulizwa iwapo huwa anatazama mtandao wa Instagram au mitandao mingine ya kijamii wakati wake wa mapumziko, naye akasema: “Mimi binafsi situmii kitu hiki. Huwa nafanya kazi kubwa hadi usiku, sina muda wa Instagram.”

Kauli hizo za Putin zimekuja wakati kuna ripoti kwamba wadukuaji wa mitandao wa Russia wanajaribu kuhujumu chaguzi katika nchi za kidemokrasia za Magharibi.
I guess Akili yake itakua fresh Sana huyu jamaa,sababu anaishi maisha nachuro kama binadam kwa asilimia kubwa Sana, hii Mitandao unatufanya inatukontroo Sana, nusu watu nusu Maroboti
 
Back
Top Bottom