Rais wa mpito aapishwa Venezueala

Rais wa mpito aapishwa Venezueala

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
53,997
Reaction score
43,162
Wanaukumbi.

Delcy Rodríguez ameapishwa kuwa rais wa mpito wa Venezuela katika kikao cha bunge kilichoanza kwa wito wa kuachiliwa kwa rais aliyeondolewa na kuzuiliwa nchini Marekani Nicolás Maduro.

Rodríguez, 56, makamu wa rais tangu 2018, alisema aliumizwa na kile alichokiita "kutekwa nyara" kwa Maduro na mkewe Cilia Flores ambao walikamatwa na vikosi vya Amerika katika uvamizi wa usiku wa Jumamosi.

Katika matukio ya kushangaza ndani ya chumba cha mahakama jijini New York saa kadhaa hapo awali, Maduro alisisitiza kuwa bado ni rais wa Venezuela huku akikana mashtaka manne ya ulanguzi wa dawa za kulevya na ugaidi.

Marekani imekosolewa vikali mkali Umojnaa wa Mataifa, lakini balozi wa Marekani alisema hifadhi kubwa zaidi ya nishati duniani haiwezi kuachwa mikononi mwa kiongozi haramu, " mkwepaji haki".
Kabla ya Maduro kufikishwa mahakamani, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya Venezuela.

Balozi wa Venezuela, Samuel Moncada, alisema nchi yake imekuwa ikilengwa na "shambulio haramu la silaha lisilo na uhalali wowote wa kisheria".

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, alihalalisha shambulio hilo kwa kumtaja Maduro kama "rais haramu".

Source: BBC News Venezuela swears in interim leader after Maduro appears in court - BBC News
 
Kufa Kufanana, She is now in Power

Ukute sasa Maduro nae alikuwa ana Mnanga VP wake may be kwasababu ya gender yake ndio balaa linaanzia Apo

Btw VP wa Maduro amesha sema yupo tayari Kufanya kazi na Marekani zile bwebwe za Kutaka Maduro aachiliwe zilikuwa awali tu kuonesha kinafiki kuwa hajafurahishwa na Decision za US

Ila Kwa sasa Power inavyobadili mtu sidhani kama uyo mwanamama ambae yupo termed kama Interim President atachia icho kiti mana tayari amesha assure wakina Marco Rubio kuwapa ushirikiano.
 
Hapo kunatengenezwa machafuko ya lazima nchini venezuera, huyo rais aliyenyakuliwa,pindi akiachiwa huru ataleta upinzani mkali kujaribu kurejesha mamlaka aliyonyang'anywa kwa nguvu.
Ufahamu siasa za Venezuela, wamefanya hivi makusudi kukwamisha mipango ya Trump ya kuleta Rais wake. Machafuko tayari raia hawataki Marekani wachuke mafuta yao.
 
Haramu kwako kwao ndiyo utaratibu wao na katiba yao Bunge ndiyo limempitsha.
Hakushinda uchaguzi, aliiba uchaguzi na hata matokeo ya idadi ya kura hayajawahi kubandikwa(kuwa published) mpaka Leo. Bongo kama Venezuela tu.
 
Hapo kunatengenezwa machafuko ya lazima nchini venezuera, huyo rais aliyenyakuliwa,pindi akiachiwa huru ataleta upinzani mkali kujaribu kurejesha mamlaka aliyonyang'anywa kwa nguvu.
Ni Ngumu sana afu uungwaji wake Mkono Venezuela Ulikuwa mdogo mana ata Combat za Jeshi wakati ananyakuliwa zilikuwa very miminimal, Jamaa akiwekwa uko Korokoroni for a while atapoteza influence kabisa

Samaki ana nguvu akiwa ndani ya Maji
Maduro anaweza kurejea na asiamini kabisa Visanga atakavyokuwa anafanyiwa na Aliyekuwa VP wake ambae ndio ame sworn in kama Interim President

Huenda akaenda mbali zaidi mpaka kusaka asylum uko Urusi
Mana Russia ana Policies nzuri sana za kuwaficha Hawa Oligarchs na Powerful Politicians
 
Ufahamu siasa za Venezuela, wamefanya hivi makusudi kukwamisha mipango ya Trump ya kuleta Rais wake. Machafuko tayari raia hawataki Marekani wachuke mafuta yao.

1767768606231.png
 
Huyo makamu wa rais inaonesha wazi ni kibaraka wa marekani tangu kitambo sana ila ndo hivo anajifanya kuleta unafki. Na mpango wote aliufahamu hata kabla haujatokea
 
Ni Ngumu sana afu uungwaji wake Mkono Venezuela Ulikuwa mdogo mana ata Combat za Jeshi wakati ananyakuliwa zilikuwa very miminimal, Jamaa akiwekwa uko Korokoroni for a while atapoteza influence kabisa

Samaki ana nguvu akiwa ndani ya Maji
Maduro anaweza kurejea na asiamini kabisa Visanga atakavyokuwa anafanyiwa na Aliyekuwa VP wake ambae ndio ame sworn in kama Interim President

Huenda akaenda mbali zaidi mpaka kusaka asylum uko Urusi
Mana Russia ana Policies nzuri sana za kuwaficha Hawa Oligarchs na Powerful Politicians
Mkuu unahisi Maduro anaweza kuachiwa hivi karibuni?
 
Back
Top Bottom