Rais wa Manzese Madee

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
MADEE

Historia ya Pendo, aliyekuwa mpenzi wa msanii Madee, ni hadithi ya kusikitisha ya kifo chake kupitia ajali iliyotokea miaka mingi iliyopita,Ni miaka takribani 16 Tangu kifo cha pendo kitokee.. jambo lililoacha alama kubwa maishani mwa Madee. Madee alionyesha huzuni yake kwa kutunga wimbo maalumu unaoitwa "Pendo" akimshirikisha Matonya, uliolenga kusimulia kifo hicho.

MADEE - PENDO

Verse.1 .. Madee

" Asubuhi kumekucha nafuta Tongo Tongo
Nawaza nitakula Nini.? Hii ndio life la kibongo/
Hisia zangu kumbe leo nizaUongo yule niliyempenda kasharudi kwenye Udongo/
Yaani kama hadithi harafu haina maelewesho/
Kwanini umeikataa Pendo kuiona kesho/
Akili zanituma siku zirudi nyuma ili nikusamehe kabla Mola ajakutuma/
Yani kama utani umefika mbele ya Haki/
Viongo vimekubali lakini moyo hautaki/
Nalia sana machozi kama samaki/
Tena naongopa bundi wasishuke juu ya Bati/
Sitaki kukufuru eti mola kakosea/
Naomba akupe Nuru kila siku nakuombea/
Imani Yangu inasema unaniona maisha yangu bila wewe yatakoma/
Salamu zikufikie vaileth Marekani/
Pendo kasha ondoka hayupo Tena Duniani/
Aliniambia mwezi wa Saba unaolewa/
Dah.! Harusi Yako hashachelewa/
Kama nakuona vile unavyo Tabasamu/
Naumia kama Jay machozi,jasho na Damu/
Yah..!!
Hisia chungu na Damu , Namuomba sana Mola akuepushe na jehanam.."

Chorus: Matonya.

"Dua njema ndizo ninazokuombea Mama
Uuh.!!
Huko unakokwenda bora ufike Salama
Pendo..!!
Uuh..!!
Najua ipo siku tutaja onana
Uuuh.!!
Namuomba mola akupe makazi Mema"

Verse. 2. Madee.

"Bwana ametoa , Na Bwana ametwaa
jina lake lihimidiwe
Popote utakapo kaa
Bwana ametoa , Na Bwana ametwaa
Na jina lake lihimidiwe
Uko wapi.? Pendo.!!
Saa nane kamili ndo ulianza Safari/
Nakuja kukufuata upo tumbi hospitali/
Jina lako halipo kwenye Daftari Nesi akaniambia umelala mochwari/
Wakavuta jokofu mama Yangu, Pendo Wangu/
Harafu umependeza umevaa T- shirt Yangu/

Nikazimia sikujua kilichotokea/
Nikaja kushtuka Wanangu wananipepea/
Nenda kalale Pema nitafuata ulioniambia/
Niache umalaya, mikanja mixer na Beer 🍺/
Yah..!

Umelala kwenye Ngiza ,kufa kwetu ni Faida lakini mbona kunaumiza/
Mkononi nina Bible na peruzi
kurasa/

Kwa kanisa yuko Tonya machozi yanamuwasha/
Pumzika salama mimi nitakuja kesho/

Mwambie Dada vivi Muziki bado kichekesho/
Kama mshumaa Tayari ulishazimika/
Maombi Yangu mengi ndio yatakayo kumulika/
Kila nikikumbuka huwa napatwa kizunguzungu/
Ila kwa yote nasema Asante Mungu..

Chorus: Matonya

"Dua njema ndizo ninazokuombea Mama
Dhabiti
Uuh.!!
Huko unakokwenda bora ufike Salama
Jamani Pendo
Uuhuu..!!
Najua ipo siku tutaja onana
Uuuh.!!
Namuomba mola akupe makazi Mema"
Aaah..!!

Outro: Quick Racka

Yoh..!!
We pray πŸ™
Rest in Peace
Aaah..!!
Madee , na fan's Wote wa Bongo fleva
Tutakumiss Sanaa,
Njia yetu ni Moja, Soo.!!
Siku moja tutakuja kuonana huko uliko
Coz Bwana akitoa ni lazima atwae Pia
Soo..!! We pray πŸ™ Racka
Mungu ibariki Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
Mungu mubariki Pendo
Mlaze mahali Pema Peponi
Amen πŸ™

PICHA ZA PAMOJA
_
Picha ya Juu ni Msanii Madee akiwa pamoja na Marehemu Pendo, chini ni Madee na mtoto aliyeachiwa na Marehemu Pendo...❀️‍πŸ”₯❀️‍πŸ”₯❀️‍πŸ”₯❀️‍πŸ”₯

Hakuna mwanamke aliyemtesa Madee kumoveon kama Pendo palikuwa na Mapenzi ya kweli hapo.

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 
Kuna binti mmoja namuonaga Goba kafanana sana na huyu mtoto wa madee,
 
Huna audio yake
 
Aiseee
 
Couple kali za wasanii.
P funk & kajala & harmonise

Madee & pendo

Mj & shaa

Nature & sinta.

Jay dee & gadna G.

Nandy & ruge & billnenga.

Diamond & Zari & mobetto & majizzo & wema sepetu & zari & tanasha Donna & lulu & zuchu & wolper & anti ezekieli& mose iyobo & whozzu & rich mitindo & linna & kajala & marioo & harmonise etc (hii tunaweza kusema line ni ndefu sana)
 
Masikini akipata....
 
Aisee mna vichwa vya ziada au?

Mnawezaje kuhifadhi mambo yote haya kwenye kichwa hicho hicho kimoja kinachowaza mpateje hela?
 
Upandishe niusikilize aisee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…