Rais wa Malawi amfuta kazi Waziri kwa kutumia vibaya fedha za Covid

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

Malawi has so far recorded more than 33,000 cases of Covid-19 and 1,138 deaths


Malawi hadi sasa imerekodi zaidi ya visa 33,000 na vifo 1,138 vya Covid-19
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amewafuta kazi maafisa wakuu akiwemo Waziri wa Leba Ken Kandodo juu ya madai ya ubadhirifu wa pesa za Covid.

Rais alisema hatua hiyo ilifuatia ukaguzi ambao alikuwa ameamuru kuhusu matumizi ya kwacha za Malawi bilioni 6.2 ($ 7.8m; £ 5.6m) kupambana na janga la Covid

Alisema hakutakuwa na watakaosazwakatika vita dhidi ya ufisadi akibainisha kuwa maafisa zaidi waandamizi waliohusishwa na ubadhirifu katika ripoti ya ukaguzi, pamoja na ofisini kwake na baraza la mawaziri, tayari wamekamatwa. Aliahidi kutakuwa na maafisa zaidi watakaokamatwa ndani ya utumishi wa umma.

"Siwezi kuwa na watundani ya baraza langu la mawaziri ambao wanatumia visivyo fedha zilizopangiwa kwa malengo tofauti’ alisema rais kupitia hotuba iliyopeperushwakwa taifa.

Waziri wa Leba ameshtumiwa kwakutumia vibaya kwacha 613,000 za Malawizilziofaa kutumiwa kupambana na Corona kugharamia safari za kwenda Afrika Kusini.

Rais amesema ingawaje waziri huyo amezirejesha fedha hizo ,hatua yake ya kuzitumia vibaya inamaanisha hazikuwepo wakati zilipohitajika
 
Back
Top Bottom