Rais wa Botswana ''amtaka Mugabe kujiuzulu''

Rais wa Botswana ''amtaka Mugabe kujiuzulu''

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,104
Reaction score
34,926
_91331430_iankhama.jpg

Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe

Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kujiuzulu mara moja kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Ameambia Reuters kuwa taifa la Zimbabwe linahitaji uongozi mpya ili kukabiliana na changaomoto za kisiasa na za kiuchumi zinazokabili taifa hilo.

''Ni wazi kwamba umri wake na hali ambayo Zimbabwe ipo kwa sasa hana uwezo wa kutoa uongozi ambao unaweza kulinusuru taifa hilo''.

Bwana Mugabe ameliongoza taifa hilo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.

Bwana Khama amemlaumu kiongozi huyo kwa tatizo linalokabili uchumi wa eneo hilo.

Amesema mgogoro uliopo Zimbabwe umewafanya raia wengi kulitoroka taifa hilo,huku wengine wakielekea Botswana ambayo inawahifadhi zaidi raia 100,000 wa Zimbabwe.

Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili ,huku akiwashtumu viongozi wanaotaka kusalia madarakani kwa mda mrefu

chanzo.BBC
 
kwani huyo mbotswana ameishajiuzulu?

swissme
 
Rais Khama anasema kuwa ataondoka afisini mwaka 2018 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili
kwani katiba yao ni muhula 2 au 1 yeye ajione kisha amuone simba wa yuda king Mgabe.



swissme
 
wazimbabwe ndio wamekua wezi botswana,Fransistown na Gaborone hao wamepakana tuu..,
 
Huyu rais wa Botswana ajiandae kisaikolojia kwa jibu atakalo jibiwa na Mugabe awe tu mpole!!
 
Ila kusema kweli huyu jamaa amechoka ni vizuri aachie damu changa,ili walete mageuzi ya uchumi.
 
Back
Top Bottom