Rais Uhuru Kenyatta amthubutu William Ruto kuondoka Serikalini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya siku ya Jumatatu alimthubutu naibu wake William Ruto kuondoka serikali badala ya kushambulia serikali kutoka ndani.

Akizungumza na wahariri nchini humo, rais hakuficha kukasirishwa kwake na ukosoaji uliotolewa dhidi ya utawala wake na kambi ya Ruto.

Rais alisema hakuwa na ufahamu wowote kwa nini upande wa DP Ruto umechagua mashambulio dhidi ya utawala wake

Aliwaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kwamba hakuwa na shida na Ruto kujenga ngome yake kisiasa lakini alihoji njia ambazo timu ya UDA inatumia. UDA ni chama kipya kinachoungwa mkono na naibu wa rais

"Sijui nini kimetokea isipokuwa ukweli ni kwamba anajaribu kujenga ngome yake ya kisiasa . Ninahisi ni bahati mbaya jinsi anavyofanya.. ni vibaya," rais alisema.

Uhuru aliongeza kuwa alishangaa kwanini naibu wake alikuwa akipinga mchakato wa BBI akisema "maswala yaliyopelekea kuundwa kwa BBI ndio yaleyale yaliyowaleta pamoja".

"Ikiwa ninataka sasa kupanua hilo, kuna shida? Tukirudi nyuma hadi mwaka wa 2013 imekuwa ajenda yangu ya kuleta watu pamoja," Uhuru alisema.

"Ikiwa mgawanyiko wa 2007 ulituleta pamoja, kuna shida tukiwaleta watu wengine ndani?" alihoji

Rais alihimiza utulivu akisema hatua yake ya kuiunganisha nchi haimaanishi kupunguza nafasi za mtu yeyote kumrithi.

"Haikunyimii nafasi zako Sio Uhuru anayechagua, ni Wakenya."

Alijutia pia kwamba maswala kadhaa yaliyosababisha mgawanyiko ambao umetikisa utawala wake yanatokana na ari yake ya kuleta umoja

"Kuna shida gani ikiwa tuna hali ya kila mtu kujumuishwa ...ambayo haijalishi ni nani atashinda, hakuna Mkenya aliyepoteza?" Aliuliza.

Mchakato wa kurekebisha katiba wa BBI ulionekana kujenga mgawanyiko hata Zaidi kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Ruto ambao walishinda uchaguzi mara mbili wakigombea kwa tiketi moja

Kwa mujibu wa katiba ya sasa rais hawezi kumfuta kazi naibu wake.Hatua hiyo ndio inayosababisha rais kuonekana kumtaka Ruto kuondoka serikalini badala ya kuikosoa akiwa ndani

Licha ya kuendelea na kampeini zake za kuchaguliwa kama rais mwaka ujao ,Ruto amekuwa akieleza mafanikio ya serikali ya Jubilee huku wakati mwingine akikosoa baadhi ya sera na maamuzi yanayofanywa na serikali

Miongoni mwa mambo ambayo Ruto hakupendezwa nayo serikalini ni mchakato huo wa BBI na ushirikiano wa karibu wa rais Kenyatta na viongozi wa upinzani hasa kiongozi wa ODM Raila Odinga

Rais pia alisema hakukubaliana na uamuzi wa mahakama ya rufaa kutupilia mbali kesi ya BBI lakini alisema ataheshimu uamuzi huo .Ruto au upande wake haujasema lolote kuhusu tamko hilo la rais kumtaka aondoke serikalini

Source: BBC Swahili
 
Amthubutu. President Uhuru Dares Ruto au imekaaje wajuvi wa lugha?
 
Hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Ruto alipoamua kuungana na Uhuru na kumsaidia kumwangusha Raila aliamini kabisa njia ya ikulu ingekua nyepesi kwake. Maskini hakujua angewaza kutumika na kutupwa nje vilevile

Nimpongeze kwa kuamua kukomaa, mwanaume amekataa kushindwa kirahisi, baada ya kutumika. Ila akumbuke tuu kwa ukabila uliokuwepo Kenya bado safari yake ni ngumu bila kuwa na support ya Raila.

Achilia mbali Daniel Arap Moi aliyekua rais japo hakuwa mkikuyu, linapokuja suala la Urais Kenya wakikuyu wapo tayari kufanya lolote Rais awe mkikuyu

Tusishangae kuja kumwona yeye na Raila wakiungana tena kabla ya uchaguzi ujao. Wakiungana Wa luo na Kalenjin wanaweza kushinda na kuvunja mfumo wa ukikuyu kenya na pia wakijipanga vizuri wanaweza kuondoa kabisa roho ya ukabila

Ila wakikuyu nao wanajua kuzaliana!!!!!!
Screenshot_20210824-094441.jpg

Mungu ibariki Tanzania.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere utaendelea kuwa Rais bora kuwahi kutokea duniani uliyweza kuunganisha taifa kwa kuondoa ubaguzi wa makabila, rangi hata dini
 
Ruto ni nyoka mwenye sumu kali sio wa kusogelea. RIP Prof Saitoti

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Siasa ya Kenya nimeipenda sana haina unafiki viongozi wanachanana live

Siasa ya Kenya ni ya kipuuzi mnooo

Sio kwamba haina unafki! Ina ukabila ambao mwananchi yupo tayari kuchagua kachagua Rais wa kabila lake bila kujali kama anabeba maslahi ya taifa au lah, na huo ni unafki uliokoleaaaa

Ukabila ukikolea hata ukihitaji huduma hadimu unauziwa tuu pale unapothibitika kuongea kilugha cha muuzaji

Nyerere aendelee kupumzika kwa amani
 
Yaani Ruto anaona sawa abakie analipwa Mishahara. Misafara na ulinzi kila kitu lakini besides serikali mbaya
 
Hivi Rutto ana nguvu gani Kenya? Maana naona kama anafanya anachotaka kwenye serikali ya Kenyatta.
 
Hivi Rutto ana nguvu gani Kenya? Maana naona kama anafanya anachotaka kwenye serikali ya Kenyatta.

Kwa sasa Ruto ana nguvu ya u DP

Ila awali Ruto alikua na nguvu ya kukubalika na makabila mengine kuacha wakikuyu. Alipojipoteza ni pale alipomwacha Raila na kuuingia mkenge wa uhuru
 
Hakuna ambaye sio mkorofi kule. Historical background ndio imewafanya kuwa walivyo
Wakalenjin wako more militia organized minded, try to ask any Kenyan and u will be told! Even PEV 2007 Kalenjins were the ones that drove Kikuyus out of Nakuru! Ni kama Wakurya Tanzania!
 
Back
Top Bottom