Rais Uhuru Kenyatta aapishwa rasmi.

Rais Uhuru Kenyatta aapishwa rasmi.

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,952
th


Leo tarehe 28.11.2017 katika uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi kulikua na tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta na Naibu Rais Mh William Rutto, katika hafla hiyo iliohudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi na wawakilishi kutoka jumla ya nchi 40 kutoka Mataifa mbalimbali Afrika, baadhi ya viongozi waliokuwepo ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali mstaafu Ian Khama, Rais wa Gabon Ali Bongo, Rais wa Rwanda Jenerali mstaafu Paul Kagame, Rais wa Uganda Jenerali Mstaafu Yoweri Kaguta Museveni ambae alisema wananchi nchini Kenya wanahitaji amani, utulivu, maendeleo na kuacha siasa, aidha pia viongozi wengine waliohudhuria walikua Rais wa Sudani Kusini Jenerali Salva kiir na mke wake,Rais wa Djibout,Makamo wa Rais wa Nigeria,Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu wa Ethiopia na viongozi wengine wa nchi mbalimbali, viapo vya Rais wa Kenya na Naibu Rais wa Kenya viliendeshwa na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji Maranga na Msajili wa Mahakama kuu ya Kenya,aidha baada ya viapo hivyo viongozi hao yaani Rais na Naibu Rais walipata wasaa wa kulihutubia Taifa la Kenya,kwa upande wa Naibu Rais Mh Rutto amesema wananchi wote wa Kenya sasa wafanye kazi ili wajenge Taifa lao na ni Mungu ndio aliowezesha yote kutokea, nae Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenya amesema atakua Rais wa Wakenya wote na sasa kazi ilibaki ni kujenga jamii bora na kuleta maendeleo ya kweli nchini Kenya, Aidha katika hali ya kushangaza leo katika makutano ya barabara ya manyanja jijini Nairobi aliekua mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha upinzani cha NASA bwana Raila Amollo Odinga alikua akihutubia wafuasi wake na kusema yeye anasubiri kuapishwa tarehe 22.12.2017 na hatambui serikali ya Kenyatta na kuiita ni serikali bandia lakini ghafla vikosi mbalimbali vya Ulinzi na Usalama nchini Kenya vilivamia mkutano huo na kuwatawanya wote kwa mabomu ya machozi na hadi sasa bado vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini Kenya vinaendelea na msako katika maeneo ya mitaa ya barabara ya manyanja ili kutuliza hali hiyo na kuleta utulivu.
 
Back
Top Bottom