Rais tunakuomba uturudishie shamba letu la Utegi wilayani Rorya

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi iendelee. Mhe. Rais uongozi wako umeturidhisha sisi Wananchi japo ni kwa muda mfupi. Mhe. Rais historia ya shamba hili ni ndefu lakini kwa kifupi naomba nitoe historia yake.

Mhe Rais katika miaka ya 1970 Serikali kwa nia nzuri kabisa iliamua kuanzisha Ranchi ya Utegi na kupelekea vijiji sita vilivyokuwa vinazunguka shamba hili kuhama ili kupisha uanzishaji wa ranchi hii. Sharti kubwa ilikuwa wafidiwe kama ilivyo taratibu na kisheria kuwa unapohamishwa ni sharti Serikali ikulipe.

Serikali kwa nia nzuri ilikubaliana na wananchi kuwa badala ya kufidiwa basi watapewa shamba hili badala ya fidia ambayo ingeigharimu fedha nyingi na hii ilikuwa baada ya ubinafshishaji wa Mashirika ya Umma. Sharti moja iliyotoa Serikali ni wananchi waweze kulipa kiasi cha Tshs.90,000,000 (Millioni tisini) ili shamba liwe mali ya vijiji hivyo kwa asilimia mia moja. Malipo ya fedha hizo zililipwa na kijana wetu mpendwa Otieno Igogo kwa lengo la kuja kumrudishia fedha zake alizolipa kwa ajili ya ununuzi wa shamba hilo. Pamoja na Ndugu huyu kulipa fedha hizi nia yake haikuwa nzuri na baadaye wananchi wa vijiji hivi walienda Mahakamani kupinga Ndugu huyu kufanya shamba hili kuwa mali yake.

Serikali ya awamu ya tano ilivyoona kuwa kulikuwa na mgogoro kati ya Ndugu huyu na Wananchi wa vijiji hivi ikaingilia kati na kuchukua/kuwanyang'anya wananchi wa vijiji hivi shamba lao bila hata kuwaeleza sababu ni kwa nini wamenyang'anywa shamba lao. Wameletwa Maaskari pale ambao wamekuwa maadui na wananchi katika shamba lao. Mwananchi hatikiwi kupita katika shamba hilo, hawatakiwi kuchunga mifugo ya katika shamba hilo, hawatakiwi kukata nyasi kwa ajili ya matumizi yao.

Sisi wananchi tumekuwa wakimbizi katika shamba letu. Ninakuomba Mhe. Rais umtume Mhe. Waziri wa mifugo na Uvuvi ili aje akuletee taarifa kamili kuhusu shamba letu la Utegi. Mhe Rais kwa heshima na taadhima tunaomba turudishiwe Shamba letu la mifugo la Utegi. Kweli inauma tukinyanyaswa katika shamba letu.
 
Nyinyi kama kijiji mlimlipa huyo bwana hizo mil 90 ili shamba liwe mali yenu kwa kuwa yeye alilipia hizo fedha serikalini?
 
Back
Top Bottom