Rais Trump asema: "Lazima tuirudishe Dini"

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Kwanini Rais Trump amesema lazima wairudishe dini katika nchi yao?
Jibu la swali hilo utalipata katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa maombi ya kitaifa(National Prayer Breakfast) yanayofanyika kila mwaka katika nchi ya Marekani. Kwa kifupi alisema hivi:

"Kuanzia siku za mwanzo za Jamhuri yetu, imani kwa Mungu imekuwa chanzo kikuu cha nguvu inayopiga katika mioyo ya taifa letu. Lazima tuirudishe dini. Lazima tuirudishe kwa nguvu zaidi... Lazima tuirudishe.

Hata Thomas Jefferson[Rais wa tatu wa USA] aliwahi kuhudhuria ibada za Jumapili zilizofanyika Bungeni, hapa hapa ninaposimama leo...
Marekani daima itakuwa “taifa moja chini ya Mungu.”

Katika historia ya Marekani, nchi yetu imekuwa ikipata matumaini, ujasiri na msukumo kwa kumtumaini Mwenyezi Mungu. Ndani kabisa ya roho ya kila mzalendo kuna maarifa kwamba Mungu ana mpango maalum na kazi tukufu kwa ajili ya Marekani. Na mpango huo utatimia. Natumaini utatimia mapema sana.

Tunapaswa kumshukuru Williams kwa kufanya uhuru wa kidini kuwa sehemu ya msingi wa maisha ya Marekani. Na leo tunapaswa kulinda uhuru huo kwa uaminifu.

George Washington, mwanzilishi wa nchi yetu, mara kwa mara aliwaomba Wamarekani waungane katika sala — mara nyingi sana.

Habari za mashujaa kama Washington, Winthrop, na Williams zinatukumbusha kuwa bila imani kwa Mungu, kusingekuwa na chochote kinachosemwa kuhusu Marekani.

Chini ya ghorofa hili kuna sanamu ya Mchungaji Billy Graham, amesimama akiwa na Biblia iliyofunguliwa, inayoonyesha barua ya mtume Paulo, isemayo:
'Tusichoke kutenda mema, kwakuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.'”

Source: Remarks by President Trump at the National Prayer Breakfast
 
Trump tapeli tu, hata kanisani huwa anaenda Krismasi na Pasaka tu.
Sio kweli. Hiyo hotuba aliitoa Alhamisi(February 6, 2025), wakati wa maombi ya kitaifa. Haikuwa Krismasi wala Pasaka.
 
Marekani imeanzishwa juu ya genocide ya Wahindi wekundu na utumwa wa mtu mweusi, Wamarekani wapuuzi ndio huwa wanadanganya watu taifa lao limeanzishwa juu ya msingi wa Mungu na Ukristo
 
Trump hajui hata mstari mmoja wa Biblia, aliwahi kuulizwa mstari wake pendwa wa Biblia akawa anatoa macho tu.
Mbona kwenye hiyo hotuba ametaja mstari ulioandikwa na Mtume Paulo:
"Tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa."(Wagalatia 6:9-10).
 
Marekani imeanzishwa juu ya genocide ya Wahindi wekundu na utumwa wa mtu mweusi, Wamarekani wapuuzi ndio huwa wanadanganya watu taifa lao limeanzishwa juu ya msingi wa Mungu na Ukristo
Kwani we unaelewaje mtu akisema: "Lazima tuirudishe dini..."
 
Kwanini Rais Trump amesema lazima wairudishe dini katika nchi yao?
Jibu la swali hilo utalipata katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa maombi ya kitaifa(National Prayer Breakfast) yanayofanyika kila mwaka katika nchi ya Marekani. Kwa kifupi alisema hivi:

"Kuanzia siku za mwanzo za Jamhuri yetu, imani kwa Mungu imekuwa chanzo kikuu cha nguvu inayopiga katika mioyo ya taifa letu. Lazima tuirudishe dini. Lazima tuirudishe kwa nguvu zaidi... Lazima tuirudishe.

Hata Thomas Jefferson[Rais wa tatu wa USA] aliwahi kuhudhuria ibada za Jumapili zilizofanyika Bungeni, hapa hapa ninaposimama leo...
Marekani daima itakuwa “taifa moja chini ya Mungu.”

Katika historia ya Marekani, nchi yetu imekuwa ikipata matumaini, ujasiri na msukumo kwa kumtumaini Mwenyezi Mungu. Ndani kabisa ya roho ya kila mzalendo kuna maarifa kwamba Mungu ana mpango maalum na kazi tukufu kwa ajili ya Marekani. Na mpango huo utatimia. Natumaini utatimia mapema sana.

Tunapaswa kumshukuru Williams kwa kufanya uhuru wa kidini kuwa sehemu ya msingi wa maisha ya Marekani. Na leo tunapaswa kulinda uhuru huo kwa uaminifu.

George Washington, mwanzilishi wa nchi yetu, mara kwa mara aliwaomba Wamarekani waungane katika sala — mara nyingi sana.

Habari za mashujaa kama Washington, Winthrop, na Williams zinatukumbusha kuwa bila imani kwa Mungu, kusingekuwa na chochote kinachosemwa kuhusu Marekani.

Chini ya ghorofa hili kuna sanamu ya Mchungaji Billy Graham, amesimama akiwa na Biblia iliyofunguliwa, inayoonyesha barua ya mtume Paulo, isemayo:
'Tusichoke kutenda mema, kwakuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.'”

Source: Remarks by President Trump at the National Prayer Breakfast
hilo taifa kimaadili limeshaoza --- sisi waafrika tunafurahia anguko lao hilo
 
Trump hajui hata mstari mmoja wa Biblia, aliwahi kuulizwa mstari wake pendwa wa Biblia akawa anatoa macho tu.
636402117477958658-GTY-841608592.jpg
 
Anarudisha dini gani sasa? Maana hata yeye Trump sidhani kama hata kama anasali, na kama anasali sijui ni dhehebu gani?
 
Back
Top Bottom