Napenda sana watu waliochanganyikiwa kama wewe hawajui washauri nini waache nini.SLAA hawezi kuwa Rais wa nchi hii,kwa sababu muda (wakati) wa vyama vya upinzani kushika dola bado haujafika na hii ni kutokana na vyama hinyo kuwa na uchanga,ubinafsi ndani yake pamoja na dira butu.kutokana na matatizo hayo vinashindwa hata kuunganisha nguvu zao na kuweka mgombea mmoja wa urais.Si hivyo tu bali pia vimejikita sana maeneo ya mjini tu na kusahau maeneo ya vijijini.
Vyama vya upinzani kwa sasa vingejizatiti zaidi katika kuwania nafasi za ubunge na siyo urais kama Slaa na wenzake walivyoamua kufanya. Hivyo SLAA hawezi katika uchaguzi huu kushinda kiti cha urais.Utapoteza kura yako bure ,vyama vya upinzani bado havijajipanga vizuri,tuvipe muda zaidi ili viweze kujipanga.