Rais Samia, wewe pia hauko juu ya Sheria

Rais Samia, wewe pia hauko juu ya Sheria

Tusidanganyane,

Kama HAKI hupatikana mahakamani, na wapo watu wamepewa Kinga ya kutoshtakiwa,

Ni dhahiri watu hao wapo juu ya sheria.

Kinga ya kutoshtakiwa iondolewe Kwa wote Ili tuwe sawa mbele ya SHERIA.

KATIBA mpya ni sasa kabla ya Uchaguzi wowote!!
Watakua juu ya sheria kama hamna sheria inayo waruhusu kua hivyo lakini kinyume na hapo wapo kwenye sheria
 
Mbona umeingia ndani ya nyumba kasoro tu umeogopa chumba kimoja hapo na utawakuta watu wawili wakiwa wamejifungia ndani huku wakiwa na Remote mbili kubwa kabisa....
Humo chumbani yumo JK na Mwingine ni R A.
Hao ndio wameshikilia na ku command kila action ya movie!


Kazi ipo.
 
Kwa taarifa yako rais wa Tanzania yuko juu ya sheria, katiba iliyopo inamlinda dhidi ya mashitaka toka anapopigiwa kura ashinde asishinde hauwezi kuhoji, na hauwezi kumshitaki kwa kosa lolote hata akimaliza muda wake wa urais.
Ila haimulindi kutoburuzwa katika mahakama za kijinai za kimataifa , ndo ndo iyoenda kutokea, kivipi

Hataki kuja na katiba mpya ili kwenda kwenye uchaguzi huru na haki akiamini ataiba kura kwa mabavu kwa back up ya vyombo vya dola ,hapa ndo anajidanganya, atatumia nguvu watu watakufa na mwisho ataburuzwa tu.

Pili kwa matendo ya kuwa na kiburi na kutotaka kusikiriza watu wanataka nini, na uonevu unaoendelea itafika watu wataingia barabarani ,hivyo vyombo vya dola vitatumia nguvu then watu watakufa next ataburuzwa tu

Endeleeni jidanganya Rais yupo juu sheria na kumjaza ,hamjui Dunia nyie
 
Kwa taarifa yako rais wa Tanzania yuko juu ya sheria, katiba iliyopo inamlinda dhidi ya mashitaka toka anapopigiwa kura ashinde asishinde hauwezi kuhoji, na hauwezi kumshitaki kwa kosa lolote hata akimaliza muda wake wa urais.
Ila haimulindi kutoburuzwa katika mahakama za kijinai za kimataifa , ndo ndo inayoenda kutokea, kivipi

Hataki kuja na katiba mpya ili kwenda kwenye uchaguzi huru na haki akiamini ataiba kura kwa mabavu kwa back up ya vyombo vya dola ,hapa ndo anajidanganya, atatumia nguvu watu watakufa na mwisho ataburuzwa tu.

Pili kwa matendo ya kuwa na kiburi na kutotaka kusikiriza watu wanataka nini, na uonevu unaoendelea itafika watu wataingia barabarani ,hivyo vyombo vya dola vitatumia nguvu then watu watakufa next ataburuzwa tu

Endeleeni jidanganya Rais yupo juu sheria na kumjaza ,hamjui Dunia
 
Hakuna aliye juu ya sheria, maana yake ni kuwa si "Kiongozi","Mtawala" na wala si "Mtawaliwa" au "Mwananchi" wa kawaida aliye juu ya sheria. Kwa maana kwamba hata pale kiongozi akisigina katiba, akivunja katiba awajibishwe na sheria.

Watawala wa kiafrika na serikali zao,Wanaitumia sheria hii vibaya. Sheria ni msumeno, unakata pande zote.
Rais Samia na serikali yake wanapaswa kuelewa hivyo, tunapaswa kuanzia hapoo!

Watawala wajuwe kwamba nchi inao watu na watu hao pia wana akili kama hizo walizo nazo wao, kulingana na maumbile ya kibinadamu tuliyopewa na mwenyezi Mungu tunazo fikra na tafakuri zinazotuwezeasha kujua mema na mabaya.

Tatizo ni kwamba ukiwa mtawala unakuwa umeweka daraja kati yako na wananchi. Na hivyo kudhania kwamba wewe na waliokuzunguka pekee ndio mnao wajibu wa kuwaza kwa niaba ya watanzania woote milioni zaidi ya sitini.

Watawala mnapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi.

VIONGOZI:
Viongozi wazuri ni waamuzi na wawazi katika michakato yao ya mawazo. Wanafahamu matokeo ya maamuzi yao na wanahakikisha yanafanywa kwa uangalifu. Ingawa matokeo yanafikiriwa vyema, hufanywa bila kuathiri kwa wakati.

Uongozi wenye maamuzi pia unajumuisha ujuzi wa kutatua matatizo na jicho pevu la kuchanganua hali mbalimbali katika nyakati husika. Huongozwa na hekima badala ya Jazba, Kiburi na Dharau. Wanatambua na kufafanua matatizo kwa usahihi.

Kisha wanaweza kutoa suluhisho zinazofaa! isikilizeni jamii, sauti ya umma ni sauti ya Mungu.View attachment 2746548
Ni ngumu sana kusimama imara kama uoga utatawala. Rais si muumini wa katiba ndiyo maana yeye ndiye sheria,anatengeneza mabavu kumlinda kuonyesha nguvu ya mipasho yake.

Tukisema hakuna aliye juu ya sheria tunajidanganya,kutojali mgawanyo wa madaraka katika mhimili yetu ni tatizo linalo ufanya mhimili mmoja kuwa juu ya sheria.

Kuwa na DDP-,MUNGU asiyeingiliwa na yeyote yule ni kuwa juu ya sheria ndiyo maana akisema unatakatisha fedha kumlinda aliye mteua asibugudhiwe.
 
Tutawasikilizia.....
Yule Gerson Msigwa amekera sana kule X zamani Twitter!
Unasema rais hayuko juu ya sheria wakati hashitakiwi akiwa au ametoka madarakani?! Ni katiba ipi unaongelea boss. Kwa katiba hii rais ni Mungu, kasoro moja tu ni kuwa anakufa.
 
Tusidanganyane,

Kama HAKI hupatikana mahakamani, na wapo watu wamepewa Kinga ya kutoshtakiwa,

Ni dhahiri watu hao wapo juu ya sheria.

Kinga ya kutoshtakiwa iondolewe Kwa wote Ili tuwe sawa mbele ya SHERIA.

KATIBA mpya ni sasa kabla ya Uchaguzi wowote!!
Hawa watu hawako sawa na sisi mbele ya sheria
 
Back
Top Bottom