Rais Samia, wewe pia hauko juu ya Sheria

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,944
Hakuna aliye juu ya sheria, maana yake ni kuwa si "Kiongozi","Mtawala" na wala si "Mtawaliwa" au "Mwananchi" wa kawaida aliye juu ya sheria. Kwa maana kwamba hata pale kiongozi akisigina katiba, akivunja katiba awajibishwe na sheria.

Watawala wa kiafrika na serikali zao,Wanaitumia sheria hii vibaya. Sheria ni msumeno, unakata pande zote.
Rais Samia na serikali yake wanapaswa kuelewa hivyo, tunapaswa kuanzia hapoo!

Watawala wajuwe kwamba nchi inao watu na watu hao pia wana akili kama hizo walizo nazo wao, kulingana na maumbile ya kibinadamu tuliyopewa na mwenyezi Mungu tunazo fikra na tafakuri zinazotuwezeasha kujua mema na mabaya.

Tatizo ni kwamba ukiwa mtawala unakuwa umeweka daraja kati yako na wananchi. Na hivyo kudhania kwamba wewe na waliokuzunguka pekee ndio mnao wajibu wa kuwaza kwa niaba ya watanzania woote milioni zaidi ya sitini.

Watawala mnapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi.

VIONGOZI:
Viongozi wazuri ni waamuzi na wawazi katika michakato yao ya mawazo. Wanafahamu matokeo ya maamuzi yao na wanahakikisha yanafanywa kwa uangalifu. Ingawa matokeo yanafikiriwa vyema, hufanywa bila kuathiri kwa wakati.

Uongozi wenye maamuzi pia unajumuisha ujuzi wa kutatua matatizo na jicho pevu la kuchanganua hali mbalimbali katika nyakati husika. Huongozwa na hekima badala ya Jazba, Kiburi na Dharau. Wanatambua na kufafanua matatizo kwa usahihi.

Kisha wanaweza kutoa suluhisho zinazofaa! isikilizeni jamii, sauti ya umma ni sauti ya Mungu.
JamiiForums1873917028.jpg
 
Tusidanganyane,

Kama HAKI hupatikana mahakamani, na wapo watu wamepewa Kinga ya kutoshtakiwa,

Ni dhahiri watu hao wapo juu ya sheria.

Kinga ya kutoshtakiwa iondolewe Kwa wote Ili tuwe sawa mbele ya SHERIA.

KATIBA mpya ni sasa kabla ya Uchaguzi wowote!!
 
tatizo kuna watu wanajiona kutokana na vyeo wapo juu ya sheria ndio maana wanadiriki kuuza raslimali za nchi wao na familia zao watakavyo.
Wanatakiwa kuwa wa kwanza kuzilinda na sio kuuza!
 
Sio wanajiona,

Wamepewa mamlaka hayo kikatiba kabisa.

Tuandike KATIBA mpya tuondoe Kinga Ili nao washtakiwe maana wanaotumia vibaya Kinga waliyopewa kuuza Raslimali walizoapa kuzilinda Kwa wageni.
 
Na huo ndio uhalisia wa mambo ulivyo.Ingawa wanajifanya kuvaa miwani ya Mbao!,Lakini waelewe kwamba muda ni shahidi mkubwa na wa ukweli.
Iko siku na saa inakuja...
 
Sio wanajiona,

Wamepewa mamlaka hayo kikatiba kabisa.

Tuandike KATIBA mpya tuondoe Kinga Ili nao washtakiwe maana wanaotumia vibaya Kinga waliyopewa kuuza Raslimali walizoapa kuzilinda Kwa wageni.
Hakika kabisaaa!
 
Hakuna aliye juu ya sheria, maana yake ni kuwa si "Kiongozi","Mtawala" na wala si "Mtawaliwa" au "Mwananchi" wa kawaida aliye juu ya sheria. Kwa maana kwamba hata pale kiongozi akisigina katiba, akivunja katiba awajibishwe na sheria.

Watawala wa kiafrika na serikali zao,Wanaitumia sheria hii vibaya. Sheria ni msumeno, unakata pande zote.
Rais Samia na serikali yake wanapaswa kuelewa hivyo, tunapaswa kuanzia hapoo!

Watawala wajuwe kwamba nchi inao watu na watu hao pia wana akili kama hizo walizo nazo wao, kulingana na maumbile ya kibinadamu tuliyopewa na mwenyezi Mungu tunazo fikra na tafakuri zinazotuwezeasha kujua mema na mabaya.

Tatizo ni kwamba ukiwa mtawala unakuwa umeweka daraja kati yako na wananchi. Na hivyo kudhania kwamba wewe na waliokuzunguka pekee ndio mnao wajibu wa kuwaza kwa niaba ya watanzania woote milioni zaidi ya sitini.

Watawala mnapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi.

VIONGOZI:
Viongozi wazuri ni waamuzi na wawazi katika michakato yao ya mawazo. Wanafahamu matokeo ya maamuzi yao na wanahakikisha yanafanywa kwa uangalifu. Ingawa matokeo yanafikiriwa vyema, hufanywa bila kuathiri kwa wakati.

Uongozi wenye maamuzi pia unajumuisha ujuzi wa kutatua matatizo na jicho pevu la kuchanganua hali mbalimbali katika nyakati husika. Huongozwa na hekima badala ya Jazba, Kiburi na Dharau. Wanatambua na kufafanua matatizo kwa usahihi.

Kisha wanaweza kutoa suluhisho zinazofaa! isikilizeni jamii, sauti ya umma ni sauti ya Mungu.View attachment 2746548
Kwa taarifa yako rais wa Tanzania yuko juu ya sheria, katiba iliyopo inamlinda dhidi ya mashitaka toka anapopigiwa kura ashinde asishinde hauwezi kuhoji, na hauwezi kumshitaki kwa kosa lolote hata akimaliza muda wake wa urais.
 
Ninaelewa hilo,lakini ila nimeweka andiko hili kuwajulisha watawala na pia mtawala Samia!
Ya kwamba iko siku haya yote yatakuwa na mwisho..
waelewe kwamba hawatakuwa milele hivyo kadri siku zinavyo songa mbele.mambo sasa yanakwenda kwa kasi sana....
Hili vuguvugu linaloongezeka sasa ni ujumbe tosha kwao kuanza kujitafakari.mabavu yana mwisho.
 
Sijui kama itawezekana kupenya kwenye ukuta wa Rapid Force( uvccm), Mwenyekiti wa CCM aliposema "sijui kama chawa wangu watakubali mkinishambulia" inawezekana wengi hatukumuelewa, ni kwamba CCM inacho kikosi cha kuilinda kwa lolote lile, hii ni hatari iliyoko mbele kwani yataweza kutokea ya Sudani.
 
Uko sahihi,ila ninachokishuhudia kwa sasa ni kwamba kuna mambo ambayo CCM inayafanya na kuzidi kuchochea chuki kubwa kutoka kwa Umma.
Hivyo huenda kulingana na kasi ya teknolojia ya mawasiliano.
Kuna tofauti kubwa itakuja ikiwepo wabunge wengi wa CCM kudondoshwa na hivyo kuongeza mbinyo Bungeni.
Na kuanzia huko lolote litawezekana pia!
Kwa sasa tatizo ni hili hapo
[emoji116]
20230911_114816.jpg
 
[emoji116]View attachment 2746674
CCM waliposema hatuwezi kukupa serikali kwa vijikaratasi walidhamilia hilo wakijua wanacho kikosi imara kikisaidiana na polisi japo Kikwete aliwahi kuishauri isiendelee kuitegemea sana polisi.
 
Uelewa wa Raia ongeza shubiri wanayolamba wananchi huko mitaani...
Itawezesha kupiga kura za hasira pamoja na kulinda kura kwa nguvu zaidi dhidi ya Poli-CCM.
Hivyo kuleta mageuzi makubwa huko Bungeni ambako ndio hasa chimbuko la uovu wote wa hii CCM.
 
Hakuna aliye juu ya sheria, maana yake ni kuwa si "Kiongozi","Mtawala" na wala si "Mtawaliwa" au "Mwananchi" wa kawaida aliye juu ya sheria. Kwa maana kwamba hata pale kiongozi akisigina katiba, akivunja katiba awajibishwe na sheria.

Watawala wa kiafrika na serikali zao,Wanaitumia sheria hii vibaya. Sheria ni msumeno, unakata pande zote.
Rais Samia na serikali yake wanapaswa kuelewa hivyo, tunapaswa kuanzia hapoo!

Watawala wajuwe kwamba nchi inao watu na watu hao pia wana akili kama hizo walizo nazo wao, kulingana na maumbile ya kibinadamu tuliyopewa na mwenyezi Mungu tunazo fikra na tafakuri zinazotuwezeasha kujua mema na mabaya.

Tatizo ni kwamba ukiwa mtawala unakuwa umeweka daraja kati yako na wananchi. Na hivyo kudhania kwamba wewe na waliokuzunguka pekee ndio mnao wajibu wa kuwaza kwa niaba ya watanzania woote milioni zaidi ya sitini.

Watawala mnapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi.

VIONGOZI:
Viongozi wazuri ni waamuzi na wawazi katika michakato yao ya mawazo. Wanafahamu matokeo ya maamuzi yao na wanahakikisha yanafanywa kwa uangalifu. Ingawa matokeo yanafikiriwa vyema, hufanywa bila kuathiri kwa wakati.

Uongozi wenye maamuzi pia unajumuisha ujuzi wa kutatua matatizo na jicho pevu la kuchanganua hali mbalimbali katika nyakati husika. Huongozwa na hekima badala ya Jazba, Kiburi na Dharau. Wanatambua na kufafanua matatizo kwa usahihi.

Kisha wanaweza kutoa suluhisho zinazofaa! isikilizeni jamii, sauti ya umma ni sauti ya Mungu.View attachment 2746548
Sifa kuu ya Kiongozi pia ni kusikiliza!
 
Uko sahihi,ila ninachokishuhudia kwa sasa ni kwamba kuna mambo ambayo CCM inayafanya na kuzidi kuchochea chuki kubwa kutoka kwa Umma.
Hivyo huenda kulingana na kasi ya teknolojia ya mawasiliano.
Kuna tofauti kubwa itakuja ikiwepo wabunge wengi wa CCM kudondoshwa na hivyo kuongeza mbinyo Bungeni.
Na kuanzia huko lolote litawezekana pia!
Kwa sasa tatizo ni hili hapo
[emoji116]View attachment 2746674

Hao wabunge watadondoshwa na nani?

Kuna thread humu imenifanya nijiulize kuhusu ule uchaguzi wa 2020, Kama Magufuli ndio alikua kweli Master planner?

Maana kwa mambo yanavyoenda sasa ni Kama tukio zima la uchaguzi wa 2020 alielipanga alijua kabisa outcome na alifanya makusudi ili kujiandaa na haya ya sasa?!

Uchaguzi 2020 -

Wabunge 99.9% CCM.

Wabunge wanawake watupu 19 kutoka upinzani wanaingizwa bungeni wengine wakitokea gerezani.

Waliingizwa na nani? Kwa makubaliano/malengo Yapi?

2021 March Rais alieshinda anapoteza Maisha akiwa ni miezi 5 tu tangu aapishwe.

Baada ya hapo Samia anaupiga mwingi mpaka anatua goli la nyumbani ….

2022 March Vilio vinaanza sikika Ngorongoro wamasai wanaambiwa waondoke kwenye ardhi walioishi zaidi ya karne 1 sababu wanaharibu mazingira na kutishia utalii…..

…2022 June Jumuiya ya Maridhiano na Amani inapongeza Serikali kuhamisha wamaasai Ngorongoro…

2023 May Rais Samia anatoa maagizo ya Mchakato wa Katiba mpya kuanza….

….2023 June linaibuka sakata la Bandari za Tanganyika na mwekezaji DP World…

….2023 August waarabu wa Dubai wanaonekana Ngorongoro wakiwa na Mzee Kinana…

2023 August Doctor Slaa anaibuka kupinga mkataba wa uwekezaji Bandari za Tanganyika na kutangaza mapinduzi….

….12 August anawekwa kizuizini na kupewa kesi ya Uhaini…..

18 August anaachiwa kwa dhamana…

….28 August mchakato wa Katiba mpya unawekwa pause kwa muda wa miaka 3 Serikali ielimishe wananchi Katiba iliyopo sasa ….

… 1 September Doctor Slaa anavuliwa title ya Ubalozi na sasa ni raia wa kawaida…

Matukio ni mengi ndani ya muda mfupi tena kwa haraka sana.

Key Master Mind ni nani? Na kwanini? Ana malengo gani? Anakusudia kufanikisha nini?

Maana siuoni kabisa wino wa Rais Samia kwenye hii blueprint, ni kweli ndio dereva? Ama nae abiria Kama wengine?

Sijamsikia Rostam Aziz muda mrefu sana. Sijui yuko wapi?
 
Hakuna aliye juu ya sheria, maana yake ni kuwa si "Kiongozi","Mtawala" na wala si "Mtawaliwa" au "Mwananchi" wa kawaida aliye juu ya sheria. Kwa maana kwamba hata pale kiongozi akisigina katiba, akivunja katiba awajibishwe na sheria.

Watawala wa kiafrika na serikali zao,Wanaitumia sheria hii vibaya. Sheria ni msumeno, unakata pande zote.
Rais Samia na serikali yake wanapaswa kuelewa hivyo, tunapaswa kuanzia hapoo!

Watawala wajuwe kwamba nchi inao watu na watu hao pia wana akili kama hizo walizo nazo wao, kulingana na maumbile ya kibinadamu tuliyopewa na mwenyezi Mungu tunazo fikra na tafakuri zinazotuwezeasha kujua mema na mabaya.

Tatizo ni kwamba ukiwa mtawala unakuwa umeweka daraja kati yako na wananchi. Na hivyo kudhania kwamba wewe na waliokuzunguka pekee ndio mnao wajibu wa kuwaza kwa niaba ya watanzania woote milioni zaidi ya sitini.

Watawala mnapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi.

VIONGOZI:
Viongozi wazuri ni waamuzi na wawazi katika michakato yao ya mawazo. Wanafahamu matokeo ya maamuzi yao na wanahakikisha yanafanywa kwa uangalifu. Ingawa matokeo yanafikiriwa vyema, hufanywa bila kuathiri kwa wakati.

Uongozi wenye maamuzi pia unajumuisha ujuzi wa kutatua matatizo na jicho pevu la kuchanganua hali mbalimbali katika nyakati husika. Huongozwa na hekima badala ya Jazba, Kiburi na Dharau. Wanatambua na kufafanua matatizo kwa usahihi.

Kisha wanaweza kutoa suluhisho zinazofaa! isikilizeni jamii, sauti ya umma ni sauti ya Mungu.View attachment 2746548
Kwa Katiba ya sasa Rais wa Tanzania yuko juu ya sheria,na kwa usahihi zaidi Rais wa Tanzania ni Mungumtu ndiyo maana kamwe haitapatikana Katiba mpya kwa njia ya maridhiano. Katiba mpya inaweza kupatikana kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi tu. CCM wako radhi nchi iingie kwenye machafuko na umwagaji damu lakini kamwe hawataruhusu uwepo wa Katiba mpya kwani ndiyo itakuwa mwisho wao kutawala na kuifukarisha nchi hii.
 
Hao wabunge watadondoshwa na nani?

Kuna thread humu imenifanya nijiulize kuhusu ule uchaguzi wa 2020, Kama Magufuli ndio alikua kweli Master planner?

Maana kwa mambo yanavyoenda sasa ni Kama tukio zima la uchaguzi wa 2020 alielipanga alijua kabisa outcome na alifanya makusudi ili kujiandaa na haya ya sasa?!

Uchaguzi 2020 -

Wabunge 99.9% CCM.

Wabunge wanawake watupu 19 kutoka upinzani wanaingizwa bungeni wengine wakitokea gerezani.

Waliingizwa na nani? Kwa makubaliano/malengo Yapi?

2021 March Rais alieshinda anapoteza Maisha akiwa ni miezi 5 tu tangu aapishwe.

Baada ya hapo Samia anaupiga mwingi mpaka anatua goli la nyumbani ….

2022 March Vilio vinaanza sikika Ngorongoro wamasai wanaambiwa waondoke kwenye ardhi walioishi zaidi ya karne 1 sababu wanaharibu mazingira na kutishia utalii…..

…2022 June Jumuiya ya Maridhiano na Amani inapongeza Serikali kuhamisha wamaasai Ngorongoro…

2023 May Rais Samia anatoa maagizo ya Mchakato wa Katiba mpya kuanza….

….2023 June linaibuka sakata la Bandari za Tanganyika na mwekezaji DP World…

….2023 August waarabu wa Dubai wanaonekana Ngorongoro wakiwa na Mzee Kinana…

2023 August Doctor Slaa anaibuka kupinga mkataba wa uwekezaji Bandari za Tanganyika na kutangaza mapinduzi….

….12 August anawekwa kizuizini na kupewa kesi ya Uhaini…..

18 August anaachiwa kwa dhamana…

….28 August mchakato wa Katiba mpya unawekwa pause kwa muda wa miaka 3 Serikali ielimishe wananchi Katiba iliyopo sasa ….

… 1 September Doctor Slaa anavuliwa title ya Ubalozi na sasa ni raia wa kawaida…

Matukio ni mengi ndani ya muda mfupi tena kwa haraka sana.

Key Master Mind ni nani? Na kwanini? Ana malengo gani? Anakusudia kufanikisha nini?

Maana siuoni kabisa wino wa Rais Samia kwenye hii blueprint, ni kweli ndio dereva? Ama nae abiria Kama wengine?

Sijamsikia Rostam Aziz muda mrefu sana. Sijui yuko wapi?
Mbona umeingia ndani ya nyumba kasoro tu umeogopa chumba kimoja hapo na utawakuta watu wawili wakiwa wamejifungia ndani huku wakiwa na Remote mbili kubwa kabisa....
Humo chumbani yumo JK na Mwingine ni R A.
Hao ndio wameshikilia na ku command kila action ya movie!
 
Hakuna aliye juu ya sheria, maana yake ni kuwa si "Kiongozi","Mtawala" na wala si "Mtawaliwa" au "Mwananchi" wa kawaida aliye juu ya sheria. Kwa maana kwamba hata pale kiongozi akisigina katiba, akivunja katiba awajibishwe na sheria.

Watawala wa kiafrika na serikali zao,Wanaitumia sheria hii vibaya. Sheria ni msumeno, unakata pande zote.
Rais Samia na serikali yake wanapaswa kuelewa hivyo, tunapaswa kuanzia hapoo!

Watawala wajuwe kwamba nchi inao watu na watu hao pia wana akili kama hizo walizo nazo wao, kulingana na maumbile ya kibinadamu tuliyopewa na mwenyezi Mungu tunazo fikra na tafakuri zinazotuwezeasha kujua mema na mabaya.

Tatizo ni kwamba ukiwa mtawala unakuwa umeweka daraja kati yako na wananchi. Na hivyo kudhania kwamba wewe na waliokuzunguka pekee ndio mnao wajibu wa kuwaza kwa niaba ya watanzania woote milioni zaidi ya sitini.

Watawala mnapaswa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi.

VIONGOZI:
Viongozi wazuri ni waamuzi na wawazi katika michakato yao ya mawazo. Wanafahamu matokeo ya maamuzi yao na wanahakikisha yanafanywa kwa uangalifu. Ingawa matokeo yanafikiriwa vyema, hufanywa bila kuathiri kwa wakati.

Uongozi wenye maamuzi pia unajumuisha ujuzi wa kutatua matatizo na jicho pevu la kuchanganua hali mbalimbali katika nyakati husika. Huongozwa na hekima badala ya Jazba, Kiburi na Dharau. Wanatambua na kufafanua matatizo kwa usahihi.

Kisha wanaweza kutoa suluhisho zinazofaa! isikilizeni jamii, sauti ya umma ni sauti ya Mungu.View attachment 2746548
Yeye ndiyo kila kitu yaani ana haki kuliko mtu mwingine
 
Back
Top Bottom