Rais Samia wewe ndio chanzo cha matatizo ya umeme nchini

Rais Samia wewe ndio chanzo cha matatizo ya umeme nchini

Viongozi wa CCM wanadhani kukata umeme ili majenereta na solar wanazouza zitoke Ni ujanja. Ukweli Ni kwamba suala la umeme wasipoangalia litawatoa kwenye uchaguzi ujao.
Mvua zipo za kumwaga, gesi ya kumwaga shida Ni menejimenti tu.
 
Ni sawa lakini na watendaji tanesco wanapaswa kubeba lawama kwa kutoweka mbele professionalism na badala yake wanahofia kufukuzwa kazi tu basi.
Ni wao haohao waliambiwa msikate umeme hawakukata na wao haohao wameambiwa kata umeme wanakata, inamaana wanasiasa ndio wataalamu wa uzalishaji na ugawaji umeme na sio wataalamu wetu wa tanesco?!

Kwanini asitokee jasiri mmoja akamwambia waziri, bwana mkubwa; situation ya sasa hairuhusu kukata umeme kwa sababu upo wa kutosha hivyo HATUKATI, kisha akafukuzwa kazi kwa kulinda profession yake akaenda kuomba kazi hata nchi za nje na hiyo cv yake ambayo inakuwa imepanda abrutly?
Ukibeba profession unafukuzwa kazi!!

Ile ishu ya kufungulia maji bwawa la Mtera ili mgao utokee wale waliojaribu kukataa kwani walifanywa nini?
 
Unamlaumu Bure TU mkuu!!

Hivi mtu anaetaka urais 2025 ataruhusu haha yatokee!!?

Hana uhakika na kesho yake!

Wanaoimiliki Tanesco ni wakubwa kuliko yeye!

Hana Cha kufanya zaidi ya kusafiri na kula bata!!
Sio kweli mkuu kila kitu mnamuonaga innocent huyo ajuza kipi anachoweza kukifanya?
 
Lawama za kipumbavu sana hizi. Moderator futa hii. Wewe mleta uzi elewa umeme wa Tanzania hautoshi na pia tayari kuanzia awamu ya 3 TANESCO imehujumiwa mno.... imekuwa ikilipa fedha nyingi kwa kuingia mikataba mibovu iliyosababishwa na watanzania wenzetu. Hata angekuwepo Magufuli bado tatizo lingeendelea. Tusubiri bwawa likamilike tujiondoe kwenye hili tatizo.
Hahahaha

Awamu ya tano ulikua haukatiki hapo jee?
 
Rais wangu bila kupepesa macho wala kuona haya wewe ndo chanzo cha matatizo ya umeme nchini yote haya yana baraka zako na chanzo ni wewe

Mama aliingia akakuka shirika la Tanesco na umeme ulikua umetengamaa kwa kiasi kikubwa.

Akaanza kubadilisha watu wa Tanesco na kuweka watu aliyowaona yeye....Hapa anaulaumiwa yeye.

Akaja kumtumbua Kalemani, kosa la kumtoa kalemani hakulitoa, lakini za chini chini zinadai ni personal issues, kuogopa legacy ya mwendazake, na mambo ya ukabila, akamuweka makamba, makamba kaingia matatizo yakaanza....Hapa Rais ni wa kulaumiwa hadi Akhera

Hakuishia hapo tu, umeme ulipoanza kuharibiwa na makamba hakukemea wala kuhoji au kumgombeza makamba alitulia kama "halimuhusu vile"....,Samia unastahili lawama.

Gesi ikapanda, wakati huo huo waziri anazunguka kugawa mitungi ya Taifa gesi na Mihan kwa kutumia pesa za umma huku hiyo kampuni waziri ana hisa humo....Rais hakuongea chochote zaidi ya kuacha yaendelee.

Tanesco wakakodi app kutoka India kwa bilioni 69 Rais kimyaaa

Makamba akaanza kuivuruga Tanesco yeye na maharage wakaja na matengenezo yasiyokwisha pesa zikiwa hazijulikani.zinapokwenda Rais kimyaaa

Maharage akaingiza kitengo cha kampuni yake ya huduma kwa Wateja rais kimyaa

Nchi ikarudi Gizani Rais kimyaaa

Halafu mnasema Rais asilaumiwe kwenye hili la umeme kwani yakiwa yanatokea si yalikua na baraka zake?Au mnataka kusema wakati yote yakijiri yeye alikua usingizini?

Tunazunguka sana kuwalaumu wengine huku tukisahau mtu anayestahili kulaumiwa na kunyooshewa kidole ni "SAMIA SULUHU HASSAN" huyu ndo chanzo cha matatizo yote na yeye ndo aliyewapa "greenlight" kina Makamba wafanye wanavyotaka.

Mnawalaumu Tanesco wakati wao wanafata tu wanachoambiwa?Au mmesahau Tanesco ni watu wa "ndio mzee" wanafata maagizo ya wakubwa? Kipindi cha magufuli waliambiwa hamna kukata umeme au migao na wakatii sasa tuwalaumu Tanesco wakati wao wanafuata maagizo ya "Samia na Makamba?"

Ingekua nchi nyingine huyu Samia angejiuzulu tu na kuwajibishwa pamoja na Makamba na Maharage lakini bahati tunatawaliwa na mfumo na bunge ambalo ni la chama kimoja tu.

Kuhusu umeme wakulaumiwa na Rais Samia kwa 100%
Akitokea Rais jasiri, akasema kwamba endapo umeme utakatika kwa zaidi ya masaa 2 mara 5 kwa mwezi, mkurugenzi wa TANESCO, wakuu wa idara, Katibu mkuu na Waziri, wataondolewa, itakuwa mwisho wa mgao.

Hayati Magufuli alisema kuwa majambazi hayawezi kutupangia muda wa kusafiri. Magari yasafiri wakati wote. Majambazi yakiteka gari, ndiyo mwisho wa kibarua cha RPC wa mkoa huo. Toka wakati huo mpaka leo magari yanatembea masaa 24, na hakuna gari limewahi kutekwa na majambazi
 
100% agree ..Tatizo linaanzia juu .yaani makamba anapojaza wapiga Dili na kuvuruga tanesco yeye anamwangalia tu..Hichi cha umeme kinaochoendelea ndio mavuno yake
Fact 100%
 
Akitokea Rais jasiri, akasema kwamba endapo umeme utakatika kwa zaidi ya masaa 2 mara 5 kwa mwezi, mkurugenzi wa TANESCO, wakuu wa idara, Katibu mkuu na Waziri, wataondolewa, itakuwa mwisho wa mgao.

Hayati Magufuli alisema kuwa majambazi hayawezi kutupangia muda wa kusafiri. Magari yasafiri wakati wote. Majambazi yakiteka gari, ndiyo mwisho wa kibarua cha RPC wa mkoa huo. Toka wakati huo mpaka leo magari yanatembea masaa 24, na hakuna gari limewahi kutekwa na majambazi
Kabisa
 
Viongozi wa CCM wanadhani kukata umeme ili majenereta na solar wanazouza zitoke Ni ujanja. Ukweli Ni kwamba suala la umeme wasipoangalia litawatoa kwenye uchaguzi ujao.
Mvua zipo za kumwaga, gesi ya kumwaga shida Ni menejimenti tu.

CCM kutafuta pesa za kampeni kupitia hii njia ya kuwanyima watu umeme ili tu matajiri wakusanye pesa ya kampeni kwa CCM, ni uharamia.
 
Japokuwa huwa sikubaliani na mfumo wa utawala uliopo hapa Tz, lakini ukweli ni kwamba Unamuonea bure huyu mama. Janga la mgawo wa umeme ulikuwepo tangu enzi za utawala wa Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Nyerere. Kiini cha Tatizo hili ni utawala mbovu wa Ccm pamoja na sisi wananchi wenyewe.
Wewe unazungumzia kiini ila watu wanalalamika huku kuzidi kwa hili tatizo la umeme hali ya kuwa hadi sasa hakuna sababu ya kueleweka iliyoelezwa, wakati kipindi cha Magu hakukuwa na shida kubwa ya umeme kiasi hiki.

Hatuwezi kukaa kimya na kusubiri hadi ccm itoke madarakani ndio tufikiri kila kitu kitakaa sawa.
 
Back
Top Bottom