Rais Samia USA, na Faida za Safari Yake

Rais Samia USA, na Faida za Safari Yake

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Rais Samia amefanya safari USA kwaajili ya uzinduzi wa filamu yake ya kuhamasisha watalii kuja Tanzania. Lakini, bila shaka, pamoja na jambo hili atakuwa ameitumia safari hiyo, kufanya mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mkutano wa World Bank, kama tulivyoambiwa.

Wapo wanaohoji kwa nini amekaa muda mrefu nje ya nchi?

Kilicho muhimu siyo kukaa muda mrefu au mfupi, bali ni kile alichokipata na kitakachopatikana kwa yeye kukaa huko muda mrefu.

Moja ya matatizo makubwa ya nchi nyingi za Afrika, ni uongozi/utawala mbaya. Kila mtu, katika nafasi yake, anayo fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine, hasa wale wanaofanya vizuri kuliko yeye. Nina imani, na namsihi, Rais Samia atumie muda huu pia kujifunza masuala ya utawala kutoka kwa mataifa kama Marekani yaliyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na katika kuwa na mifumo imara ya uongozi unaozingatia haki, demokrasia, uhuru wa watu na vyombo vya habari, uhuru wa Bunge, Mahakama inayojitegemea, na mifumo ya kuwajibishana.

Kuna faida zinazotokana na kujifunza, japo haiwekwi wazi, tunaziona. Rais Samia alipokwenda Ulaya, ndipo alipoweza kwenda kuonana na kiongozi mmojawapo wa upinzani, Tundu Lisu (akiwa hapa, waliomba kukutana naye, hakuwapa hiyo nafasi). Aliporudi toka Ulaya, Mbowe alifutiwa kesi ya kubambikiziwa ya ugaidi (akiwa hapa alipigiwa kelele nyingi sana, hakufanya chochote). Mbowe alipotolewa gerezani, Samia alimwalika ikulu (kabla yake, waliomba kukutana naye bila mafanikio). Naaamini, akienda huko nje, kuna kitu anajifunza kutoka kwa viongozi wenzake pia.

Safari hii akirudi, sijui atachukua hatua gani katika mambo ambayo wananchi wanayalalamikia. Huenda akaanzisha mchakato wa kupata katiba mpya nzuri yenye faida kwa Taifa letu, itakayokuwa msingi wa mifumo mizuri ya utawala.

Awamu ya 5, nadhani kila mmoja anafahamu ilivyoweza kuharibu mambo mengi, na kuleta madhira mengi kwa Taifa na watu wake. Tutambue kuwa, awamu hiyo ya 5 ilikiwa ni utawala wa kujifungia. Ni utawala uliokuwa umekosa exposure, uliokosa civilisation na uliokuwa umekosa vision. Kwa vyovyote, kutochangamana na viongozi wengine wa Dunia, lazima kulikuwa na mchango wake kuweza kuwa na utawala wa namna ile.

Kama kukaa kwake Rais Samia nje, kutaleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu, wacha akae huko, hata kama ni miezi miwili. Mbona wafanyakazi wengine, kwaajili ya kuketa ufanisi kwenye organization mbalimbali, huwa tunawapeleka hata nje kwaajili ya mafunzo ya muda mfupi? Rais hawezi kwenda kwenye mafunzo rasmi ya namna hiyo kwa sababu hakuna chuo cha kufunza uongozi kwa Marais, lakini haiondoi nafasi kwa Rais mmoja kujifunza toka kwa wengine, kama ambavyo wengine wanaweza kujifunza toka kwake kwenye jambo ambalo anafanya vizuri kuliko wao.
 
Kama kukaa kwake Rais Samia nje, kutaleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu, wacha akae huko, hata kama ni miezi miwili.
Matatizo yanaanzia hapa. Kwa mawazo kama haya bado tunasafari ndefu.

Asante kwa mawazo mkuu
 
NYIE WARUSI WEUSI KWA NINIMAMA SAMIA HAKWENDA KUZINDUA FILAMU YAKE URUSI AMA CHINA??? KWANINI AENDE KWA HAO MNAWAITA MABEBERU??? 😂😂😂
 
Rais Samia amefanya safari USA kwaajili ya uzinduzi wa filamu yake ya kuhamasisha watalii kuja Tanzania. Lakini, bila shaka, pamoja na jambo hili atakuwa ameitumia safari hiyo, kufanya mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mkutano wa World Bank, kama tulivyoambiwa.
Kwanza, naunga mkono hoja, pili ni hii next post yangu.
P
 
Ukiwahi kuona wapi rais wa nchi anaacha nchi yake anahamia nchi nyingine kukaa?

Kama safari za nje za rais zingekua zinafaida basi zile za Kikwete Tanzania ingeshakua kama New York. Maana kikwete kila siku alikua anaishi kwenye ndege.

Mawazo ya viongozi wetu bado wanaamini wazungu ndio watakaotuletea maendeleo kila siku kwenda kuzurula kwenye nchi zao.

Rais badala ashughulikie mahitaji ya muhimu ya nchi hii anaenda kushughulikia Paramount pictures, kwani sisi tulimwambia tuna shida na movies?

Kilimo kimeajiri zaidi ya 90% ya watanzania, badala ushugulikie sekta ya muhimu ya uchumi unaenda kushughulikia movies, hivi sekta ya uigizaji Tanzania inachangia ngapi kwenye pato la taifa hadi ipewe kipaumbele hivyo na Rais wetu nchini Marekani?

Watu mazao hayana masoko na ndio shughuli kuu ya kiuchumi badala utafte masoko, viwanda vya kuongeza thamani, mbolea imepanda bei zaidi ya 100% na wakati mwingine haipatikani rais unaenda kutembelea sijui baba yake Rihana, anatusaidia nini huyo mzee?

Hii nchi alietulaani alituweza.
 
Awamu ya 5, nadhani kila mmoja anafahamu ilivyoweza kuharibu mambo mengi, na kuleta madhira mengi kwa Taifa na watu wake. Tutambue kuwa, awamu hiyo ya 5 ilikiwa ni utawala wa kujifungia. Ni utawala uliokuwa umekosa exposure, uliokosa civilisation na uliokuwa umekosa vision. Kwa vyovyote, kutochangamana na viongozi wengine wa Dunia, lazima kulikuwa na mchango wake kuweza kuwa na utawala wa namna ile.
Pili: Hivi hatuwezi kusifu awamu ya 6 bila kuiponda awamu ya 5?.
P
 
NYIE WARUSI WEUSI KWA NINIMAMA SAMIA HAKWENDA KUZINDUA FILAMU YAKE URUSI AMA CHINA??? KWANINI AENDE KWA HAO MNAWAITA MABEBERU??? [emoji23][emoji23][emoji23]
Urusi na China, labda kama unataka kuimarisha siasa za mwendazake.

Mataifa yote hayo mawili, hayakustahili kuwepo hapo yalipo. Yapo hapo kwa sababu ya siasa zisizoheshimu utu.

Leo hii China, pamoja na uwingi mkubwa wa watu, uchumi wake unategemea kwa kiasi kikubwa uwekezaji mkubwa waliofanya mataifa ya Magharibi. Zaidi ya makampuni 1000 ya nchi za Magharibi, yamewekeza China. Leo hii makampuni hayo yakiondoka, China itarudi ilikokuwa.

Urusi nayo kwa maiaka mingi inahangaika na kutengeneza mabomu huku uchumi wake ukiwa hauendi kokote. Kuanzia miaka ya 2000 ikabidi iyaangukie mataifa ya Magharibi ili makampuni yake yakawekeze huko. Zaidi ya kampuni 1000 za mataifa ya Magharibi yamewekeza China. Kwenye mgogoro wa sasa, zaidi ya makampuni 600 ya nchi za Magharibi yamefunga Russia.
 
Rais Samia amefanya safari USA kwaajili ya uzinduzi wa filamu yake ya kuhamasisha watalii kuja Tanzania. Lakini, bila shaka, pamoja na jambo hili atakuwa ameitumia safari hiyo, kufanya mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mkutano wa World Bank, kama tulivyoambiwa.

Wapo wanaohoji kwa nini amekaa muda mrefu nje ya nchi?

Kilicho muhimu siyo kukaa muda mrefu au mfupi, bali ni kile alichokipata na kitakachopatikana kwa yeye kukaa huko muda mrefu.

Moja ya matatizo makubwa ya nchi nyingi za Afrika, ni uongozi/utawala mbaya. Kila mtu, katika nafasi yake, anayo fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine, hasa wale wanaofanya vizuri kuliko yeye. Nina imani, na namsihi, Rais Samia atumie muda huu pia kujifunza masuala ya utawala kutoka kwa mataifa kama Marekani yaliyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na katika kuwa na mifumo imara ya uongozi unaozingatia haki, demokrasia, uhuru wa watu na vyombo vya habari, uhuru wa Bunge, Mahakama inayojitegemea, na mifumo ya kuwajibishana.

Kuna faida zinazotokana na kujifunza, japo haiwekwi wazi, tunaziona. Rais Samia alipokwenda Ulaya, ndipo alipoweza kwenda kuonana na kiongozi mmojawapo wa upinzani, Tundu Lisu (akiwa hapa, waliomba kukutana naye, hakuwapa hiyo nafasi). Aliporudi toka Ulaya, Mbowe alifutiwa kesi ya kubambikiziwa ya ugaidi (akiwa hapa alipigiwa kelele nyingi sana, hakufanya chochote). Mbowe alipotolewa gerezani, Samia alimwalika ikulu (kabla yake, waliomba kukutana naye bila mafanikio). Naaamini, akienda huko nje, kuna kitu anajifunza kutoka kwa viongozi wenzake pia.

Safari hii akirudi, sijui atachukua hatua gani katika mambo ambayo wananchi wanayalalamikia. Huenda akaanzisha mchakato wa kupata katiba mpya nzuri yenye faida kwa Taifa letu, itakayokuwa msingi wa mifumo mizuri ya utawala.

Awamu ya 5, nadhani kila mmoja anafahamu ilivyoweza kuharibu mambo mengi, na kuleta madhira mengi kwa Taifa na watu wake. Tutambue kuwa, awamu hiyo ya 5 ilikiwa ni utawala wa kujifungia. Ni utawala uliokuwa umekosa exposure, uliokosa civilisation na uliokuwa umekosa vision. Kwa vyovyote, kutochangamana na viongozi wengine wa Dunia, lazima kulikuwa na mchango wake kuweza kuwa na utawala wa namna ile.

Kama kukaa kwake Rais Samia nje, kutaleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu, wacha akae huko, hata kama ni miezi miwili. Mbona wafanyakazi wengine, kwaajili ya kuketa ufanisi kwenye organization mbalimbali, huwa tunawapeleka hata nje kwaajili ya mafunzo ya muda mfupi? Rais hawezi kwenda kwenye mafunzo rasmi ya namna hiyo kwa sababu hakuna chuo cha kufunza uongozi kwa Marais, lakini haiondoi nafasi kwa Rais mmoja kujifunza toka kwa wengine, kama ambavyo wengine wanaweza kujifunza toka kwake kwenye jambo ambalo anafanya vizuri kuliko wao.
😃😃😃😃😃😃😃PUMBA tu, bila kujitegemea nothing will happen brother. Tuendelee kulima tu Matikiti.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]PUMBA tu, bila kujitegemea nothing will happen brother. Tuendelee kulima tu Matikiti.
Kufahamu hoja na isiyo hoja, ni lazima uwe na akili, angalao hata ile ya kawaida.
 
Bila mifumo imara hakuna kitu atabadilisha, sahivi kuna report ya CAG pesa za umma zimetafunwa haswa lakini hata hahangaiki nayo wala PM wake.
 
Rais Samia amefanya safari USA kwaajili ya uzinduzi wa filamu yake ya kuhamasisha watalii kuja Tanzania. Lakini, bila shaka, pamoja na jambo hili atakuwa ameitumia safari hiyo, kufanya mambo mengine, ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mkutano wa World Bank, kama tulivyoambiwa.

Wapo wanaohoji kwa nini amekaa muda mrefu nje ya nchi?

Kilicho muhimu siyo kukaa muda mrefu au mfupi, bali ni kile alichokipata na kitakachopatikana kwa yeye kukaa huko muda mrefu.

Moja ya matatizo makubwa ya nchi nyingi za Afrika, ni uongozi/utawala mbaya. Kila mtu, katika nafasi yake, anayo fursa ya kujifunza kutoka kwa wengine, hasa wale wanaofanya vizuri kuliko yeye. Nina imani, na namsihi, Rais Samia atumie muda huu pia kujifunza masuala ya utawala kutoka kwa mataifa kama Marekani yaliyopiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na katika kuwa na mifumo imara ya uongozi unaozingatia haki, demokrasia, uhuru wa watu na vyombo vya habari, uhuru wa Bunge, Mahakama inayojitegemea, na mifumo ya kuwajibishana.

Kuna faida zinazotokana na kujifunza, japo haiwekwi wazi, tunaziona. Rais Samia alipokwenda Ulaya, ndipo alipoweza kwenda kuonana na kiongozi mmojawapo wa upinzani, Tundu Lisu (akiwa hapa, waliomba kukutana naye, hakuwapa hiyo nafasi). Aliporudi toka Ulaya, Mbowe alifutiwa kesi ya kubambikiziwa ya ugaidi (akiwa hapa alipigiwa kelele nyingi sana, hakufanya chochote). Mbowe alipotolewa gerezani, Samia alimwalika ikulu (kabla yake, waliomba kukutana naye bila mafanikio). Naaamini, akienda huko nje, kuna kitu anajifunza kutoka kwa viongozi wenzake pia.

Safari hii akirudi, sijui atachukua hatua gani katika mambo ambayo wananchi wanayalalamikia. Huenda akaanzisha mchakato wa kupata katiba mpya nzuri yenye faida kwa Taifa letu, itakayokuwa msingi wa mifumo mizuri ya utawala.

Awamu ya 5, nadhani kila mmoja anafahamu ilivyoweza kuharibu mambo mengi, na kuleta madhira mengi kwa Taifa na watu wake. Tutambue kuwa, awamu hiyo ya 5 ilikiwa ni utawala wa kujifungia. Ni utawala uliokuwa umekosa exposure, uliokosa civilisation na uliokuwa umekosa vision. Kwa vyovyote, kutochangamana na viongozi wengine wa Dunia, lazima kulikuwa na mchango wake kuweza kuwa na utawala wa namna ile.

Kama kukaa kwake Rais Samia nje, kutaleta mabadiliko chanya kwa nchi yetu, wacha akae huko, hata kama ni miezi miwili. Mbona wafanyakazi wengine, kwaajili ya kuketa ufanisi kwenye organization mbalimbali, huwa tunawapeleka hata nje kwaajili ya mafunzo ya muda mfupi? Rais hawezi kwenda kwenye mafunzo rasmi ya namna hiyo kwa sababu hakuna chuo cha kufunza uongozi kwa Marais, lakini haiondoi nafasi kwa Rais mmoja kujifunza toka kwa wengine, kama ambavyo wengine wanaweza kujifunza toka kwake kwenye jambo ambalo anafanya vizuri kuliko wao.
Hongera kwa bandiko zuri. Yule Magufuli siyo kwamba alikuwa anabana matumizi LA HASHA. Magufuli alikuwa na changamoto kubwa mbili zilizomfanya asitoke nje ya Tanzania mara kwa mara;

1. Kiafya alikuwa amewekewa kijibetri kifuani kinachongeza heart beat maarufu kama pacemaker au dedilbrator. Kifaa hicho aliwekewea mwaka 1992 hivyo kulikuwa kimechakaa. Asingeweza kuchukua risk ya kupanda ndege kwa masaa zaidi ya 3 hewani

2. Lugha ya English ilikuwa ni shida kwa Magufuli. Kile kiingereza chake cha "pipo were saying in ze rake" ni aibu tupu. Unaweza ukatumia mkalimani ukienda Nchi zinazoongea Portuguese, French, Spanish au Germany na Asia. Lakini kwa mtu unayetoka former British Colony na una PhD (japo fake), kuwa na interpretor ni aibu. Ndipo Magufuli akaamua kuwa wa hapa hapa.

Hoja za kubana matumizi na za uwongo tu
 
Bila mifumo imara hakuna kitu atabadilisha, sahivi kuna report ya CAG pesa za umma zimetafunwa haswa lakini hata hahangaiki nayo wala PM wake.
Ndiyo maana tunamtaka ajifunze kutoka mataifa yenye mifumo imara. Adiishie kuona tu na kustaajabu, bali arudi na kitu positive.
 
Hongera kwa bandiko zuri. Yule Magufuli siyo kwamba alikuwa anabana matumizi LA HASHA. Magufuli alikuwa na changamoto kubwa mbili zilizomfanya asitoke nje ya Tanzania mara kwa mara;

1. Kiafya alikuwa amewekewa kijibetri kifuani kinachongeza heart beat maarufu kama pacemaker au dedilbrator. Kifaa hicho aliwekewea mwaka 1992 hivyo kulikuwa kimechakaa. Asingeweza kuchukua risk ya kupanda ndege kwa masaa zaidi ya 3 hewani

2. Lugha ya English ilikuwa ni shida kwa Magufuli. Kile kiingereza chake cha "pipo were saying in ze rake" ni aibu tupu. Unaweza ukatumia mkalimani ukienda Nchi zinazoongea Portuguese, French, Spanish au Germany na Asia. Lakini kwa mtu unayetoka former British Colony na una PhD (japo fake), kuwa na interpretor ni aibu. Ndipo Magufuli akaamua kuwa wa hapa hapa.

Hoja za kubana matumizi na za uwongo tu
Watu wengi hawajui kuwa Tanzania ina two official languages. Ya kwanza ni English, na ya pili ni Swahili. Ndiyo maana hata sheria zetu zinatungwa kwa kitumia first official language. Kwenye Kiswahili inaenda tafsiri tu.

Sasa Rais ukaonekana hujui hata official language no. 1 ya nchi yako, unakuwa kituko cha Dunia.
 
Back
Top Bottom