Rais Samia umeanza kuelemewa, tunaomba 2025 upinzani tukusaidie

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Mwanzo naona alianza vizuri ila kadri siku zinavyoenda anaanza kuboronga sana.

Mama hayupo makini kuteua wasaidizi wake, either hana washauri au ni yeye tu hajui tena afanyaje.

Ukikosea Mara ya kwanza tunasema bahati mbaya, ukikosea mara ya pili jambo lile lile tunasema umeteleza ila ukikosea mara ya 3, mara ya 4 mara ya 5 ,hapo Kuna kitu hakipo sawa.

Kwenye teuzi hadi sasa ni kama mama kishapoteana, ni vile bado tuna machungu ya ubaya wa awamu iliyopita.

Uteuzi wa mkurugenzi wa TPDC ulikosea, ukatengua ndani ya saa 24, hakuwa na sifa ila ulipaswa ujue hili kabla hujafanya uteuzi.

Ukakosea uteuzi wa RAS wa Simiyu bi Azza, ukatengua ndani ya saa 24 baada ya kugundua hana sifa, Ila ulipaswa ujue kabla hujamteua.

Ukakosea uteuzi wa RC Kafulila, ukabadilisha hapohapo wakiwa wanaapishwa.

Leo tena vilevile, unateua mtu juzi, jana anaapishwa, leo unamteua nafasi nyingine alafu ile ya juzi ambayo ameapa jana unatengua.

Hii sio kawaida, ni kwamba umezidiwa. Wala usipate shida wa kukusaidia wapo na wamejipanga waachie nao waongoze.

Tunashukuru hauna maneno ya kukera ila kwenye uraisi bado hautoshi. Uraisi ni taasisi sasa iweje haya makosa ya aina moja yanajirudia kila siku. Hautoshi

Road to 2025
 
Mm nnavyojua wamama kwny kuendesha gari huwa wanapoteana sana.

Mfano:

Yaan kipande cha kurudi reverse mara moja na kuondoka,yeye anaeza akaenda mble na kurudi nyuma hata mara saba, mpk anatoka hapo sheeeee utachoka kwa hasira. Lkn akitoka hapo usalama upo thabiti.

Ndivyo nnavyoona kwa Mama, anachokifanya ni kama madereva wa kike.

Anaendesha mbele nyuma vya kutosha lkn ndo anaondoka huyo.
 
Kweli bwana, Mama anaacha wasiwasi kwa watu wenye uelewa kwamba kwanini anateua baada ya hapo muda mfupi anatengua tena, labda anafanya hivo kwa nia fulani ngoja tuone!
 
Hakuna watu wanaish kwa tabu sasa hivi kama upinzani, sanasana chadema.yaan hawaelew wanamkosoaje mama. Hahah, yaan wanamuamzaje kumkosoa mama yao, na vile mama ki africa huwa hakosei. Weee wana hal mbaya
 
Kwahiyo mnamchomekea majina kwny faili ili kesho yake mje mumsimange kuwa hatoshi?

hivi mama na yule aliyeokota vichwa vya treni visivyo na mtu bandarini, yule alieweka ndgu zake kila kona nani ana afadhali?

Uzuri wa mama akigundua amechomekewa, anarekebisha fasta na kazi inaendelea kwa jina la jamuhuri ya tanzania.

mama atake asitake, tutamwongezea muda wa kutawala bila kikomo.
 
Binafsi nimepata kizunguzungu mpaka sasa, sijui nitoe hii avatar yangu au nisubiri kidogo. Mpaka hapa sina uhakika kama nilichagua upande sahihi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom