Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,362
- 4,816
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema, uchumi wa buluu ni fursa huku akiwataka wananchi kujipanga na kuweka mazingira muafaka ya uwekezaji ili waweze kunufaika kupitia rasilimali zinazopatikana katika sekta hiyo.
Dkt. Samia alisema hayo katika sherehe za Msimu wa Pili wa Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Sea Food Festival) lililofanyika katika ufukwe wa Kendwa, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.
Wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Rais, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega alisema maana halisi ya uchumi wa buluu ni matumizi endelevu ya rasilimali zilizomo kwenye bahari, maziwa na mito kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa, kutengeneza ajira na kuleta ustawi wa maisha ya watu na vilevile kutunza afya ya maumbile ya bahari.
Aliongeza kwa kusema kuwa ili fursa hizo ziweze kuwa endelevu ni muhimu kuhakikisha kunakuwa na mipango ya matumizi sahihi ya bahari, usimamizi bora wa ikolojia za bahari, kudhibiti uchafuzi wa bahari, kuimarisha uvuvi wa bahari kuu na kusimamia mnyororo wa thamani wa mazao ya baharini na kuimarisha mifumo ya kitaasisi ya usimamizi bora wa uchumi wa buluu na rasilimali zake.
"Hili sio suala la Kitaifa tu, bali la Kikanda na Kimataifa. kama mnavyofahamu pamoja na kwamba mabadiliko ya tabianchi yanaathiri maeneo yote ya nchi, maeneo ya visiwa yapo hatarini zaidi. Hivyo, hatuna budi kulisimamia vyema suala la uhifadhi wa mazingira," alifafanua