PostGE2025 Rais Samia: Tumeambiwa vijana walioingia barabarani kudai haki walilipwa fedha kwanza

PostGE2025 Rais Samia: Tumeambiwa vijana walioingia barabarani kudai haki walilipwa fedha kwanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Rais Samia amesema "Tunaambiwa kwamba vijana wale walioingia kudai haki walilipwa fedha kwanza ndiyo wakaingia barabarani, na wengi wao waliingia barabarani kutokana na hizo fedha walizopewa. Je, fedha hizo zilitoka wapi?" wakati akizindua Tume huru ya uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Oktoba 29, 2025


 
Rais Samia amesema "Tumeambiwa vijana walioingia barabarani kudai haki walilipwa kwanza" wakati akizindua Tume huru ya uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Oktoba 29, 2025
Yaani ni bora hata angekaa kimya tu. Kila akifungua mdomo wake anazidi kuharibu na kuzidisha hasira.
 
Kwanza yeye mwenyewe ni haramu na anayoyafanya kwa sasa ni haramu. Huwezi jisimika madaraka kwa njia haramu halafu uwe halali. Mbaya zaidi anazidi kuwajaza Wahanga hasira. Hata tume yenyewe nina uhakika ime paralize kwa matamshi yale.

Watu wote waliohudhuria kwenye uharamishaji ule nyuso zao zinaonyesha hawakuwa tayari kufanya kazi naye. Ila kwa sababu ya kuhofia maisha yao basi wamekosa namna. Hofu imewatawala kwenye nyuso zao.

Huyu Rais kwasasa asaidiwe kisaikolojia ana msongo mkubwa wa mawazo. Kwa kifupi kwa sasa yeye anafahamu kuwa ameshalikoroga kwa uzembe wake mwenyewe kwa tamaa ya madaraka. Sasa ni ule semi " nimekosa tukose wote". Waliomzunguka wamueleze ukweli. Ameshazeeka nothing to lose awaache vijana wa watu wanaopambania maisha yao ya kesho.
 
mimi sikulipwa na yeyote ni kwa hiari yangu mwenyewe niliingia barabarani na kukinukisha
Kuna mwl mwenzako kama ww naye alijifanya anatafuta haki wakati nae kutwa anatoroka kazini yaani saa 7 TU yupo kitaa...now walimdaka kwenye maandamano yupo segerea now...sasa unajiuliza ni haki Gani alikuwa anaidai wakati yy ndo alikuwa haitimizii haki nchi
 
Ningekuwa Mimi lakini, Kuna vitu sensitive nisingekuwa navitolea maelezo au kufanya jitihada vieleweke kwa urahisi...

Maana kuna msemo wa washenga kuwa kama umekosea au hauko sawa na unahitaji kueleweka.... JITAHIDI KUEPEUKA KUJIELEZEA ELEZEA AU KUTENGENEZA EXPLANATION kwasababu utaharibu zaidi

Maana navyokumbuka mama yangu wa kunizaa wakati anatoa maelezo siku ya kukalia kiti alichokipata, kwa maelezo yake alidai wale watoto hawakuwa wa Taifa teule na ndio maana hakukua na haja ya kuwapa pole kwa yaliyotokea.... Paap week moja baadae, Mama yangu akaunda Kamati ya kutatua na kufuatilia mienendo ya kilichotokea paap Ikatolewa POLE kwa waliokumbwa na madhira... Natafakari vingi, ngoja nikikaa naye Jioni nitaomba niwe naandika Mimi maelezo kwenye karatasi ili kupunguza mama yangu asiendelee kujikanganya...

Hello Tanzania..

See you 🤗

Tuonane tena 2026, February.. tukipewa uzima na Afya

Wazee wangu wa Diaspora tukutane huko majuu
 
Back
Top Bottom