Rais Samia Suluhu pamoja na kutokujibu adhima ya watumishi, lakini hotuba yake ilijaa hekima

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
PAMOJA NA KUTOKUTIMIZA ADHIMA YA WAFANYAKAZI, HOTUBA YA MHE RAIS IMEJAA HEKIMA KUBWA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo kilikuwa kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani. Nchini Tanzania sherehe hiyo imefanyika Mkoani Mwanza na Rais wa JMT kuwa Mgeni Rasimi.

Mhe Samia ametumia muda huo kuwapongeza Watumishi na kujibu changamoto zao. Mategemeo makubwa ya Watumishi wengi ilikuwa ni kupandishwa mishahara na kupunguza Baadhi ya kodi ambazo zimekuwa kero kwa Watumishi.

Mhe Rais amesema ktk maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani nchini Tanzania amesema licha ya matamanio yake ya kuongeza mishahara lakini inamuwia vigumu kufanya hivyo kwa sasa. Inawezekana ni neno ambalo halikutarajiwa na Watumishi wengi ambao kwa miaka 6 sasa wamekuwa kwenye kilio hicho.

Mhe Rais Samia Suluhu HASSAN alianza kwa kusema "Ndugu zangu mimi ni mama na mama ni mlezi ila kuna msemo usemao kuwa masikini huwa anapenda mwanae apendeze lakini shida ni uwezo."

Rais Samia amesema ameshindwa kutimiza matamanio ya wafanyakazi mwaka huu kwa kuwa kasi ya uchumi imeshuka kutokana na janga la ugonjwa wa Corona. Amesema uchumi wa nchi umeshuka kutoka asilimia 6.9 mpaka asilimia 4.7.

Lakini amehaidi kupunguza kodi na tozo mbalimbali za serikali kwa wafanyakazi. Aidha amesema imekuwa ngumu kuongeza mshahara kwa kuwa ndio kwanza anaanza kazi lakini mwakani ataweza kutimiza dai hilo ambalo ni mhimu kwa wafanyakazi. Amesema kutokana na Madeni anayotarajia kulipa Watumishi, kuajiri na kupunguza Baadhi ya kodi itakuwa ngumu kwa serikali kubeba tena hili la mishahara.

Mhe Rais amesistiza kuwa wanaenda kupandisha vyeo vya wafanyakazi 85,000 mpaka 91,000 ambao wataigharimu serikali milioni , wanakusudia kulipa malimbikizo ya mishahara, kuboresha miundo ya kiutumishi na kuongeza ajira mpya takribani elfu arobaini.

Vilevile wataongeza jitihada za kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa, hivyo anatumaini kwa jitihada hizo zitasaidia maisha ya watanzania.

Mhe Rais amesistiza kuwa wanaenda kupandisha vyeo vya wafanyakazi 85,000 mpaka 91,000 ambao wataigharimu serikali milioni , wanakusudia kulipa malimbikizo ya mishahara, kuboresha miundo ya kiutumishi na kuongeza ajira mpya takribani elfu arobaini.

Vilevile wataongeza jitihada za kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa, hivyo anatumaini kwa jitihada hizo zitasaidia maisha ya watanzania.

Wachambuzi wengi wa maswala ya kisiasa wanasema hotuba ya Mhe Rais pamoja na kuto kujibu kiu ya Watumishi, lakini IMEJAA HEKIMA na matumaini makubwa, kwani amesema mwakani atalitekeleza.

Mhe Rais pia kitendo Cha kuanza kuwaomba Wafanyakazi msamaha yeye akiwa ni Raia namba Moja kinaonyesha namna hekima ya Mama inavyopaswa kuwa kwenye dhamira ya ulezi.
 
Lugha njema nayo ni dawa.Mimi ni miongoni mwa watumishi ambao tangu siku nyingi nilikuwa nasema:

1:Mshahara kutopanda kwa miaka mingi siyo tatizo,ilimradi tu mtu apandishwe madaraja yake kwa wakati na madeni na stahiki zake za kiutumishi kama ile annual incrementi iliyoko kisheria apewe

2:Huduma na miundo mbinu mipya na huduma za jamii vionekana vinaboreshwa

3:Kodi za wananchi zionekane jinsi zinavyotumika kama vile tunapoona kasi ya usambazaji wa umeme,barabara,shule nk

4:Kuwe na lugha ya staha kwa watumishi kama alivyosema leo mama kuwa hali ya uchumi imeshuka kidogo,lakini pia ameangalia hata wale watoto wetu wasio na ajira kwakuwa vyote hivyo tunavitaji

5: Kujibu kwa haraka matatizo yale ambayo watu wanayalalamikia mfano suala la Bima ya Afya kwa vijana wa miaka 18,Retention fee kwenye Loarn Board nk kilikuwa kilio cha watu wengi.

Kwa maoni yangu kwa sasa aangalie sana suala la maji.Mamlaka za maji kwakweli sehemu nyingi bado ni tatizo.Mfano Mji kama Songea Mjini kuna vyanzo vya Maji kibao tofauti na Mikoa kama Iringa,Tabora nk,lakini kasi ya kusambaza maji katika Manispaa hii ni ndogo sana.

Mfano haiwezekani eneo kama la Mshangano,lenye maji kidogo sana,Shule ya Tanga ambako ndiyo Stand Kuu ya Mabasi nk watu bado wanatumia maji ya Visima.Kwakweli sekta hii wanatakiwa kujitathimini.
 
Back
Top Bottom