Rais Samia Suluhu imulike NHIF

Rais Samia Suluhu imulike NHIF

Tatizo la NHIF lipo Sana mikoa ambayo ofisi za NHIF ni uozo mtupu. Mfano ni Geita ,, ofisi za NHIF tangu naprocess Kadi yangu nilijua tu ni ubabaishaji.

Lakin NHIF Mwanza wapo vizur mno,, yaan hata ukienda Pharmacy na fomu zako hakuna longo longo
 
Kumbuka kuna Mkurugenzi wakaati wa Kikwete (iliandikwa sana humu) alituhumiwa kumhonga shangingi Waziri mwenye dhamana ya tiba ili amteue tena kusimamia hiyo bima
Hayo mambo yalishaoita kitambo mkuu,tuikosea NHIF kwa hoja!sio porojo.
 
Mimi Binafsi jambo ninalojivunia kuwa Mtanzania ni kusomeshwa na Serikali na hii Bima ya Afya ! Bima Kuna changamoto lakini ,sisi ambao shetani was Ugonjwa anatuqndama Bima ,hii ni lulu!
 
Hakuna kitu kinakera,kinaumiza wachangiaji kama hiki hasa unapofika hosptali na kuambiwa gharama fulani hazilipiwi na BIMA.
Mbaya zaidi unapofika hosptali gharama ulizotumia Kwenye form ya BIMA huzioni kwa ujumla ni wizi mtupu juu ya wizi.Serikali itupie macho huku.
Ushauri form za matibabu tunazotibiwa zionyeshe malipo ya huduma mchangiaji anayopewa.Pili huduma zisiwe za kubagua bagua.pili BIMA inapotumika mchangiaji atumiwe sms kuonyesha gharama alizotumia badala ya kutishia kutuma sms ya kuonyesha kadi ya BIMA imetumika
Mkuu Hapo kwenye Wanafaika una hoja ,ila tatizo lilianza pale Waswahili tulipoanza ujanja 2,ili.kuepuka hayo wewe kachikue Cheri Cha Ndoa!
Gharama take sio kubwa ...by the way ,kama mna ndoa yenye amani na utulivu na mlofunga Kimila!
Serikali ikikuambia katafute Cheti kuna shida Gani...haiathiri chochote!
Kimyume chake ,Kuna kitu ndani ya hiyo Ndoa ya Kimila unakificha🤫
 
Kutokana na ukirindimba uliojaa NHIF imekuwa hata fedheha sasa kutumia kadi zao mahospitali.
Watoa huduma wakiona unatoa kadi NHIF sura inabadilika unaonekana kama dhalili wa mwisho duniani usiejimudu kwa chochote.

Kuonyesha uduni wa huduma wenye kadi za NHIF wanapaswa kupewa, baadhi ya vituo vya afya wameweka section maalum kabisa kwa ajili ya wenyewe NHIF. Upande huo kuanzia anaepokea kadi mapokezi mpaka daktari wanakuchukulia kama umeenda kuomba msaada.

Ukitaka sasa kujua kuwa hiyo kadi ni uoza mtupu nenda hospitali za vijijini, hata kuziona hawataki.

Hili shirika na bomu kubwa mno linalosubiri kubutuka tu.
Huu ni udhoefu "wa Wapi Mkuu...Mbona kutumiia NHIF siku Hizi ni Ufahari sio Fedheha....kila Mtu anatamani !?
Hebu tupe mfano tusaidiane!
 
Hayo mambo yalishaoita kitambo mkuu,tuikosea NHIF kwa hoja!sio porojo.
Hoja ni pamoja na kutazama mentalitty ya wanaopewa dhamana ya kusimamia huo mfuko, bila hilo tutahangaika
 
Nimekuwa mdau muhimu kwenye hii taasisi inayojihusisha na huduma muhimu za Afya yetu watanzania. Kuna mengi yamejificha nyuma ya pazia inayopelekea hii NHIF kuwa chaka la kupiga fedha za Serikali,nikimaanisha michango ya wanachana kuwa ni pombe ya ngomani kila mmoja anajichotea tu.

Kuna malalamiko mengi yanayojitokeza kati wa Mwanachama mchangiaji anapopata huduma,Mfuko wenyewe NHIF kama mlipaji, na watoa huruma. Huu ni utatu mchafu.

Mwanachama anapoenda kupata huduma za kiafya sehemu husika kuna huduma anazozipata hazilingani kabisa na gharama NHIF itakazolipa kwa mtoa huduma. Yaani hapa mgonjwa Mwanachama wa NHIF anaweza tibiwa kwa gharama anazoweza kuziona labda Tsh 9000. Lakini kinachopelekwa NHIF ni tofauti na hiyo gharama aliyoiona mteja.

Mtoa huduma naye akishapeleka hizo gharama zake alizozitoa kwa huyu Mwanachama wa NHIF,sizo atakazolipwa na NHIF.

Huyu anaweza kupeleka madai ya Tsh 9000 ile na akalipwa Tsh 6000 kama si 5000. Na NHIF hutoa sababu mbalimbali za hayo makato ikiwa ni pamoja na Mdai kuambia kuwa kuna dawa au vipimo kavitoa kimakosa au bila usahihi

Mtoa huduma akirudi kwenye mwongozo unaomtaka ahudumieje,anakuta yuko sahihi kabisa.

Sasa hapa ndipo tatizo linapoanzia, Mtoa huduma anajikuta anaingia kwenye ukurasa mwingine wa kujaza form tofauti na aliyoitoa kwa Mteja aliyemtibu na kujaza nyingine yenye gharama za juu ili kufidia hayo makato yasiyo na tija wayafanyayo NHIF. Wizi unaanzia hapa.

NHIF naye anapopelekewa hizo gharama zisizo sahihi kama kawaida yake atakata anavyojisikia na kurejesha kwa mtoa huduma anachoona kinamfaa.

Huko NHIF haijulikani kama wanavyompa mtoa huduma ndivyo vinavyokuwa sahihi na kwao!!!!? Hilo ni jambo la huko. Nako kwa kumulika.

Huu utatu mchafu unamuumiza zaidi huyu mchangiaji maana hii sio NSSF ambako atakuja kupigiana hesabu na mwajili apate chake sahihi.

Ushauri
NHIF ikiwezekana wajenge vituo vyao vya kutolea huduma hizi kwa wanachama wao ili kusiwe na hili la Mwanachama kupata huduma zisizoendana na uhalisia wa alichohudumiwa maana imekuwa ni tatizo kwelikweli.

Kama wanakusanya michango ya kutosha isiyo na rejesho kwa Mwanachama.,Basi wanao uwezo wa kujenga vituo na wanachama tukapata huduma sahihi kwao kuliko tunayofanyiwa huku walikotoa tenda za kutibiwa ambako ni upigaji mwanzo mwisho.

Wanaajiri Madaktari na kuwezesha kukopesha vituo vya kutolea huduma hivyo wanaweza kuyafanya haya yoote wao wenyewe NHIF. Waige kwa NSSF nk wanaojiwekezea kwenye miradi mingi kwa manufaa ya mfuko na wanachama wao.
Preliminary code ya ugonjwa hujazi
Final code ya ugonjwa hujazi
Dawa huandiki dosage,strength,formulation wala duration
Practioner aliesaini form sio aliyeko kwenye mfumo
Namba ya simu ya mteja ulimpatia huduma haipo kwenye form ya matibabu
Madai huja claim kwa wakati

To be honest,hata hicho kidogo ulicholipwa huoni kama umefikiriwa tu
 
Wewe ndo haswaa mtu wa NHIF....

Kwenye hayo mapungufu mnamchukuliaje huyo mtoa huduma?

Miingozo anayo au hana?
Ni kweli mtoa huduma anaweza fanya huo usanii ili apoteze fedha zake?
Au ndo kumkomoa tu atajaza mwenyewe?
Na hicho unachosema analipwa kama huruma unamlimpa kwa wakati?
Analeta madai yake hayo yenye mapungufu unamlipa baada ya miezi 3....bado huyu atakuwa na hamu tena ya kuwahudumia wagonjwa wa NHIF???

Wewe NHIF servant ndiye unasababisha mteja wa NHIF akifika hospital or any facility aonekane ni kichefuchefu tu.

Inafikia hatua mteja wa NHIF kuficha hiyo kadi kwenye baadhi ya facility ili angalau apokelewe kwa bashasha...maana akiionyesha tu hiyo kadi ya NHIF mapema ni shida....

Yaani kuwa na hiyo kadi medical attendant akikuona reception sura yake hubadirika na kuwa kama binadamu aliyeona kisichostahili kuwa hapo mbele ya uso wake.

Hamjui jinsi mnavyoishusha thamani hii kadi ya NHIF tu. Chanzo ni ninyi kumfanya mteja asithaminiwe kwa usumbufu anaoupata mtoa huduma kuona hapa sasa kaingia kibaka tu wa kumpotezea pesa zake kwenye uwekezaji.

Jitafakarini sana.
Hata haya maelezo yako yanaonyesha kiburi halisi mlichonacho na pesa za bure za mfuko!!!!
 
Tunashukuru kwa maoni haya kwa Mfuko na kuthamini ushirika wenu katika kuimarisha taasisi hii ya muhimu kwa watanzania wote. Mfuko unayachukua, kuyatathmini na kuyafanyia kazi.

Aidha, taasisi hii inaongozwa kwa sheria, kanuni na miongozo na inasimamiwa na mamlaka husika ikiwa ni pamoja na kukaguliwa. Mfuko unaingia makubaliano maalum na watoa huduma katika kuwahudumia wanachama wake ambayo yanahitajika kufuatwa ili kuleta ufanisi pande zote na kuepusha malalamiko.

Endapo kuna changamoto au lalamiko lolote mahsusi ni vema kuliwasilisha kwa Mfuko au kwa Mamlaka zinazosimamia Mfuko ili liweze kutatuliwa.

Mfuko unaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha wengi zaidi wanaendelea kunufaika.
 
Wewe ndo haswaa mtu wa NHIF....

Kwenye hayo mapungufu mnamchukuliaje huyo mtoa huduma?

Miingozo anayo au hana?
Ni kweli mtoa huduma anaweza fanya huo usanii ili apoteze fedha zake?
Au ndo kumkomoa tu atajaza mwenyewe?
Na hicho unachosema analipwa kama huruma unamlimpa kwa wakati?
Analeta madai yake hayo yenye mapungufu unamlipa baada ya miezi 3....bado huyu atakuwa na hamu tena ya kuwahudumia wagonjwa wa NHIF???

Wewe NHIF servant ndiye unasababisha mteja wa NHIF akifika hospital or any facility aonekane ni kichefuchefu tu.

Inafikia hatua mteja wa NHIF kuficha hiyo kadi kwenye baadhi ya facility ili angalau apokelewe kwa bashasha...maana akiionyesha tu hiyo kadi ya NHIF mapema ni shida....

Yaani kuwa na hiyo kadi medical attendant akikuona reception sura yake hubadirika na kuwa kama binadamu aliyeona kisichostahili kuwa hapo mbele ya uso wake.

Hamjui jinsi mnavyoishusha thamani hii kadi ya NHIF tu. Chanzo ni ninyi kumfanya mteja asithaminiwe kwa usumbufu anaoupata mtoa huduma kuona hapa sasa kaingia kibaka tu wa kumpotezea pesa zake kwenye uwekezaji.

Jitafakarini sana.
Hata haya maelezo yako yanaonyesha kiburi halisi mlichonacho na pesa za bure za mfuko!!!!
Wapo wanaoclaim 20m na ikalipwa hivohivo lkn sbb ni kua wanafata taratibu

Usipofuata taratibu utaonekana msanii tu,utasema nimemuhudumia huyu kumbe hujamuhudumia
 
Kula kwa urefu wa kamba, ila usivimbewe!
 
Word!
Nimekuwa mdau muhimu kwenye hii taasisi inayojihusisha na huduma muhimu za Afya yetu watanzania. Kuna mengi yamejificha nyuma ya pazia inayopelekea hii NHIF kuwa chaka la kupiga fedha za Serikali,nikimaanisha michango ya wanachana kuwa ni pombe ya ngomani kila mmoja anajichotea tu.

Kuna malalamiko mengi yanayojitokeza kati wa Mwanachama mchangiaji anapopata huduma,Mfuko wenyewe NHIF kama mlipaji, na watoa huruma. Huu ni utatu mchafu.

Mwanachama anapoenda kupata huduma za kiafya sehemu husika kuna huduma anazozipata hazilingani kabisa na gharama NHIF itakazolipa kwa mtoa huduma. Yaani hapa mgonjwa Mwanachama wa NHIF anaweza tibiwa kwa gharama anazoweza kuziona labda Tsh 9000. Lakini kinachopelekwa NHIF ni tofauti na hiyo gharama aliyoiona mteja.

Mtoa huduma naye akishapeleka hizo gharama zake alizozitoa kwa huyu Mwanachama wa NHIF,sizo atakazolipwa na NHIF.

Huyu anaweza kupeleka madai ya Tsh 9000 ile na akalipwa Tsh 6000 kama si 5000. Na NHIF hutoa sababu mbalimbali za hayo makato ikiwa ni pamoja na Mdai kuambia kuwa kuna dawa au vipimo kavitoa kimakosa au bila usahihi

Mtoa huduma akirudi kwenye mwongozo unaomtaka ahudumieje,anakuta yuko sahihi kabisa.

Sasa hapa ndipo tatizo linapoanzia, Mtoa huduma anajikuta anaingia kwenye ukurasa mwingine wa kujaza form tofauti na aliyoitoa kwa Mteja aliyemtibu na kujaza nyingine yenye gharama za juu ili kufidia hayo makato yasiyo na tija wayafanyayo NHIF. Wizi unaanzia hapa.

NHIF naye anapopelekewa hizo gharama zisizo sahihi kama kawaida yake atakata anavyojisikia na kurejesha kwa mtoa huduma anachoona kinamfaa.

Huko NHIF haijulikani kama wanavyompa mtoa huduma ndivyo vinavyokuwa sahihi na kwao!!!!? Hilo ni jambo la huko. Nako kwa kumulika.

Huu utatu mchafu unamuumiza zaidi huyu mchangiaji maana hii sio NSSF ambako atakuja kupigiana hesabu na mwajili apate chake sahihi.

Ushauri
NHIF ikiwezekana wajenge vituo vyao vya kutolea huduma hizi kwa wanachama wao ili kusiwe na hili la Mwanachama kupata huduma zisizoendana na uhalisia wa alichohudumiwa maana imekuwa ni tatizo kwelikweli.

Kama wanakusanya michango ya kutosha isiyo na rejesho kwa Mwanachama.,Basi wanao uwezo wa kujenga vituo na wanachama tukapata huduma sahihi kwao kuliko tunayofanyiwa huku walikotoa tenda za kutibiwa ambako ni upigaji mwanzo mwisho.

Wanaajiri Madaktari na kuwezesha kukopesha vituo vya kutolea huduma hivyo wanaweza kuyafanya haya yoote wao wenyewe NHIF. Waige kwa NSSF nk wanaojiwekezea kwenye miradi mingi kwa manufaa ya mfuko na wanachama wao.
 
Cha ajabu hakuna jambo amabalo serikali hailijui hapa.
 
Tunashukuru kwa maoni haya kwa Mfuko na kuthamini ushirika wenu katika kuimarisha taasisi hii ya muhimu kwa watanzania wote. Mfuko unayachukua, kuyatathmini na kuyafanyia kazi.
Lipeni kwa wakati hao wadau wenu ili wanachama wa NHIF tusionekane vituko tufikapo kwenye vituo vya kutolea huduma. Maana kadi zetu za NHIF zinachukuliwa na watoa huduma kama MUFILISI tumeingia vituoni mwao.

Kama ipo miongozo mnayowapatia hao watoa huduma inakuwaje wao kukengeuka kuifata mpaka wafikie kujaza ndivyo sivyo? Mnakaa nao kuwasahihisha? Au ndio acha wajaze vibaya tuwachanje tuu!!?? Tunaumia sisi...wanachachama kwa kutegana kwenu.

Fanyeni utaratibu wa kuingiza kwenye mfumo wenu wa taarifa,ninapopata sms ya kuthibitisha huduma nnazozipata niendane sambamba na gharama zake ambozo zitafanya nijue Mimi mteje nimetibiwa kwa kiwango ambacho kitakuwa wazi kwenu NHIF,Mtoa huduma,na Mimi mteja ili kuepusha hili jambo la ukokotoaji siku mtoa huduma anapowasilisha madai yake huko iwe mwezi au miezi kwa kadri mlivyokubaliana. Maana hapa kwenye mchakato wa maandalizi ndipo tunakoumia wateja, NHIF, na huyo mtoa huduma. Anaweza kufanya awezalo iwe kubadiri taarifa halisi za niliyehudumiwa ili kufidia huo muda wa malipo yake ikiwemo kujiandaa na hayo makato yenu kwenye hizo errors mnazowafanyia kwenye ukokotoaji kwa kuwakata.

Hii itasaidia uhalali kwetu na kwenu pia.

Mfuko unapigwa sana hapa kwenye MUDA wa uchakataji wa mtoa huduma baada ya Mimi mteje kuondoka pale kituoni naye anapojiandaa kuwaletea madai.

Mnao watendaji kwenye mifumo ya IT hivyo ni rahisi kuyafanya hayo kuepusha hizi sintofahamu zinazotufanya wateja tuknekane kama vituko huko kwa watoa huduma wenu.
 
Hospital ya Ben Mkapa kila huduma unayopewa na gharama ipo kwenye risiti na hata msg ikija kwenye simu inakuja na jumla ya gharama ulizotumia
 
Tatizo la NHIF lipo Sana mikoa ambayo ofisi za NHIF ni uozo mtupu. Mfano ni Geita ,, ofisi za NHIF tangu naprocess Kadi yangu nilijua tu ni ubabaishaji.

Lakin NHIF Mwanza wapo vizur mno,, yaan hata ukienda Pharmacy na fomu zako hakuna longo longo
Sasa wote tutaenda Mwanza mkuu?
 
Lipeni kwa wakati hao wadau wenu ili wanachama wa NHIF tusionekane vituko tufikapo kwenye vituo vya kutolea huduma. Maana kadi zetu za NHIF zinachukuliwa na watoa huduma kama MUFILISI tumeingia vituoni mwao.

Kama ipo miongozo mnayowapatia hao watoa huduma inakuwaje wao kukengeuka kuifata mpaka wafikie kujaza ndivyo sivyo? Mnakaa nao kuwasahihisha? Au ndio acha wajaze vibaya tuwachanje tuu!!?? Tunaumia sisi...wanachachama kwa kutegana kwenu.

Fanyeni utaratibu wa kuingiza kwenye mfumo wenu wa taarifa,ninapopata sms ya kuthibitisha huduma nnazozipata niendane sambamba na gharama zake ambozo zitafanya nijue Mimi mteje nimetibiwa kwa kiwango ambacho kitakuwa wazi kwenu NHIF,Mtoa huduma,na Mimi mteja ili kuepusha hili jambo la ukokotoaji siku mtoa huduma anapowasilisha madai yake huko iwe mwezi au miezi kwa kadri mlivyokubaliana. Maana hapa kwenye mchakato wa maandalizi ndipo tunakoumia wateja, NHIF, na huyo mtoa huduma. Anaweza kufanya awezalo iwe kubadiri taarifa halisi za niliyehudumiwa ili kufidia huo muda wa malipo yake ikiwemo kujiandaa na hayo makato yenu kwenye hizo errors mnazowafanyia kwenye ukokotoaji kwa kuwakata.

Hii itasaidia uhalali kwetu na kwenu pia.

Mfuko unapigwa sana hapa kwenye MUDA wa uchakataji wa mtoa huduma baada ya Mimi mteje kuondoka pale kituoni naye anapojiandaa kuwaletea madai.

Mnao watendaji kwenye mifumo ya IT hivyo ni rahisi kuyafanya hayo kuepusha hizi sintofahamu zinazotufanya wateja tuknekane kama vituko huko kwa watoa huduma wenu.
Hawa jamaa siyo kwamba hawajui haya matatizo ni wanajua na wao si wanaugua na kutibiwa? kwa nini hawataki mfumo wa NHIF uunganishwe na mifumo mingine iwe online service? jibu ni moja tu wanalipa pesa ndefu sn ajili ya kufanya uhakiki wa form na huo ni mradi wao mkubwa wa kulipana posho n.k
 
Back
Top Bottom