Rais, Samia Suluhu Hassan amemaliza kazi majimboni, Wabunge wa sasa watapita kiulaini uchaguzi 2025. Tutegemee Wabunge wengi kupita bila kupingwa

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Ni Mwaka mmoja na miezi saba sasa inatimia toka Mh. Samia Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi kubwa aliyofanya kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja na miezi saba ya kuwa madarakani kinatoa taswira ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Wabunge wengi walio madarakani huwa wanadondoshwa katika majimbo yao katika awamu inayofuata ikiwa sababu kubwa ni kushindwa kusimamia miradi inayogusa Wananchi moja kwa moja ambayo ni miradi ya Elimu, Afya, Maji, Barabara etc.

Serikali ya awamu ya Sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan kwa muda wa mwaka mmoja na miezi saba imetekeleza kwa namna ya kipekee miradi ya Elimu, Afya, Maji, Barabara etc katika kila Jimbo la uchaguzi, bila kujali Jimbo hilo liko chini ya Mbunge wa Chadema , CUF, ACT au CCM.

Hakuna Mwananchi ambaye sasa anaweza lalamika kuwa watotot wake wanatembea umbali mrefu kufuata shule, Hakuna Mama anayelalamika kuwa anafuata huduma za Afya umbali mrefu, hakuna Mwananch anayelalamika kuwa katika Zahanati/Vituo vya Afya/Hospital hakuna dawa, Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kumtua mama ndoo kichwani, hakuna Mkulima anayelalamika kuwa anashindwa kusafirisha mazao yake kwa sababu ya ubovu wa barabara, hakuna Mtanzania anayelalamika mtoto wake ameshindwa kwenda shule kwa ukosefu wa ada. Malalamiko ya namna hii ndiyo yalikuwa yanawaangusha wabunge wengi na kufanya Wananchi kila awamu kuchagua mbunge mpya.

Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano, amewatatulia kero zote Wabunge wa Jamhuri ya Muungano katika majimbo yao, hivyo Wananchi kwa sasa hawana tatizo na Wabunge katika majimbo yao, Wabunge wengi watashinda tena katika uchaguzi wa 2025 na Wabunge wengi watapita bila kupingwa. Kazi imeshaisha ndani ya mwaka mmoja na miezi saba, je baada ya miaka miwili inayokuja kuna Mwananch atakuwa na lalamiko lolote? Jibu ni hapana. Data huwa hazidanganyi, kama ni upinzani umeshatepeta ndembendembe, kwa uchache hii ni baadhi ya miradi inayotekelezwa katika kila jimbo-:

1. Katika Kila jimbo, kuna shule mpya za Kata zimejengwa - Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ametoa bilion 10
2. Katika Kila jimbo, kuna zahanati/kituo cha afya /hospital mpya zimejengwa kwenye kata ( vimejengwa vituo vya Afya 352)
3. Katika Kila jimbo, katika shule zenye Wanafunzi wenye mahitaji maalum shule za Msingi na Sekondari zimejengewa mabweni - Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ametoa bilioni 54.
4. Katika Kila jimbo, umaliziaji wa miundo mbinu ya Shule umefanyika (Madarasa) -Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ametoa bilioni 43
5. Katika kila jimbo - zimepelekwa fedha kwa ajili ya ununuaji wa vitabu Shule za Msingi-Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ametoa bilioni 50
6. Katika kila jimbo - Watoto wa Watanzania wanendelea kusoma bila ada -Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano anatoa kila mwezi bilioni 26 kwa ajili ya Elimu bila ada.
7. Katika Kila jimbo, zimetolewa fedha za umaliziaji maabara za masomo ya sayansi katika shule za Sekondari
8. Kuna majimbo, yamejengewa shule maalumu za Sayansi kwa ajili ya Wanafunzi wa kike- Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano ametoa bilioni 30.
9. Katika Kila jimbo, kila mwezi zinapelekwa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
10. Katika Kila jimbo , Mh. Rais wa Jamhuri wa ya Muungano ametoa fedha za ujenzi wa barabara za mtaani
11. Katika Kila jimbo kuna mradi wa maji unaotekelezwa
12. Etc

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Wale wa Baraza la Mapinduzi kazi kwenu kuhakikisha matilioni ya Fedha yanayopelekwa Majimboni yanatumika kutekeleza miradi ya maendelo kwa manufaa ya Watanzania ili kukidhi nia njema ya Mh Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha maendeleo yanawafikia Watanzania.

Wakurugenzi wa Halmashauri hawajawaangusha Wabunge, usiku na mchana wanahangaika kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa Wakati lakini pia ubora na viwango vikizingatiwa, Mungu awabariki DEDs.

Ukisema unaimani na utendaji kazi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wala unakuwa hujafanya kosa lolote bali utakuwa umesema ukweli, na ukisema ukweli hata Mungu wako anakupa baraka.

Mungu ibariki Tanzania.
Mungu Mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Kazi iendeleee.
 
Acha kupiga mayowe bali waache watu watakupa majibu.Deejay,tuletee ule wimbo wa ..."Maji na umeme imeshakuwa kero"...!
 
Hivi hivi na hizi shida za maji, umeme na matozo?
Kambaku unategemea kila siku kila kitu kitakuwa stable? Hata Ulaya kwenye mifumo imara vita ya Russia na Ukrn imewashake kwenye nishati.

Saizi kuna changamoto ya maji kutokana na uhaba wa mvua, kuna muda tuwe wa kweli sio kila kitu ni kutoa lawama tu, Serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa
 
Back
Top Bottom