GE2025 Rais Samia: Rushwa imepungua nchini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali nchini yametokana na usimamizi imara wa mapato ya serikali yanayotokana na kodi za wananchi na mikopo kutoka vyanzo mbalimbali.

“Tumesimamia matumizi mazuri, na watumishi wetu tumeweza kuwaweka kwenye mstari wa kusimamia matumizi na kuepuka rushwa, ndugu zangu,” amesema Dkt. Samia.

Amefafanua kuwa bila usimamizi huo madhubuti, mafanikio yaliyoshuhudiwa hivi sasa yasingekuwepo, huku akibainisha kuwa serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma inalindwa.

Huyu kuna siku atasema yesu amesharudi
 
Anaongea na kujijibu mwenyewe maskini...
 
Wasaidizi wa rais hawamuambii ukweli.
Rushwa ndio kwanza imefikia kiwango cha juu zaidi tangu tupate uhuru.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alikaa masaa manne bila huduma pale Mawenzi Hosp kwasababu hakutoa chai.
Just imagine mkuu wa mkoa kwenye mkoa wake.
Angekuja Dar si angejuta kuzaliwa.
 
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali nchini yametokana na usimamizi imara wa mapato ya serikali yanayotokana na kodi za wananchi na mikopo kutoka vyanzo mbalimbali.

“Tumesimamia matumizi mazuri, na watumishi wetu tumeweza kuwaweka kwenye mstari wa kusimamia matumizi na kuepuka rushwa, ndugu zangu,” amesema Dkt. Samia.

Amefafanua kuwa bila usimamizi huo madhubuti, mafanikio yaliyoshuhudiwa hivi sasa yasingekuwepo, huku akibainisha kuwa serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma inalindwa.

Rushwa imepunguaje? Wakati Abdul na wengine serikalini wanachukua fedha zetu. Haijawahi kupungua wewe mama. Tumeona unaendelea kukopa wala hakuna kinachofanyika
 
Back
Top Bottom