Rais Samia ni mbobevu katika siasa, msimchukulie poa

Rais Samia ni mbobevu katika siasa, msimchukulie poa

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,886
Reaction score
5,623
Nilikuwa naangalia "poster" yenye Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya 2002 ambapo Hayati Benjamin W.Mkapa akiwa Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (Mjumbe), na Mhe. Samia Suluhu Hassan (Mjumbe) nikajisemea CCM hii wewe ione hivi tu! lakini nikwambieni CCM haiko kama unavyoiona wewe bali CCM iko kama jinsi ilivyo.

Hiki Chama Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Karume walikisuka kwelikweli kimfumo!

CCM si kama hivi vyama tunavyoviona hapa Nchini vinalipukalipuka tu.

Sasa hivi karibuni Rais Samia amefanya makubwa yenye kuthibitisha yeye ni mbobevu na ni AKILI KUBWA.

Kwanza, amemng'oa Job Ndugai kwenye Uspika bila nguvu kubwa. Huwezi kuwa na Spika mropokaji mkaenda sawa.

Pili, kumrudisha barazani Nape Nnauye na kumwingiza Ridhiwani alijua vizabinazabina watapiga kelele lakini akaamua kulipa gharama kwa kumtoa Mohammed Mchengerwa kwenye Wizara Nyeti ya Utawala Bora na Utumishi na kumpeleka " inferior docket" ya Utamaduni na Michezo! Sote tunajua Mchengerwa ni " Mkwirima" wa Mama.

Nadhani mnaona watu wanavyomlaumu Mama kumtoa Mchengerwa pale ! " that is the game! na ame- win 100%

Tatu, amemzuia tayari William Vangimembe Lukuvi kuwa Spika, HAMTAKI ,period.

Kauli ya Mama iko clear kabisa, "najua hatachukua fomu ya Uspika" maana yake alishanusha harakati zake.

Hivyo anamuepushia shari ili asijekuchukua fomu akamkata jina kwenye vikao vya chama akathibitisha bifu lake kwake.

Tuna Rais makini na muungwana sana !Sasa Lukuvi jiheshimishe kwa hilo.

Acha watu wasiojitambua kama akina Dr. Kigwangalla wakachukue fomu walie vichwa.

Bravo Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Sawa, lakini sisi hatuhitaji hayo yote, tunataka Umeme, Maji, ajira, usalama wetu na Mali zetu na siyo mipasho, hii ni nchi na siyo dating site!
 
Sawa, lakini sisi hatuhitaji hayo yote, tunataka Umeme, Maji, ajira, usalama wetu na Mali zetu na siyo mipasho, hii ni nchi na siyo dating site!
Magoli yanapatikana baada ya kupeleka timu uwanjani! Unataka magoli huku hutaki timu! Ni sawa unasubiru Meli pale Airport
 
Kweli mama fundi sana wa siasa. Kama ni mpira amecheza kama pele . Aliowatoa ameona wananguvu kisiasa akaamua kufinyia ndani hali iko shwari
 
Mama Atawapelekesha sana vichwa maji, wale kina Kitila wao hawana madhara yoyote wanaweza kurudi ata chadema mana waliingia ccm kwa mshindo beni nadhan kadi ya Chadema anayo mpaka leo
 
Back
Top Bottom