Rais Samia na Ronald Reagan ni same stereo types?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,906
Kama kuna Rais Mmarekani aliwahi kukejeliwa basi hakuna aliemzidi Ronald Reagan.

Nakumbuka hata Nyerere katika hotuba zake aliwahi sema kuhusu Reagan."jitu kimekaa Tu pale linawakilisha maslahi ya mabeberu" hata halina akili".

Nyerere alikuja kuongea haya baadae Sana miaka ambayo tayari Marekani washabadilisha Sana Marais.

Sababu kubwa Sana ya kukejeliwa Kwa Ronald Reagan ilikuwa sababu Ronald Reagan hakuwa "traditional" Rais kama wengine ...waliokuwa na CV zilizoshiba zinazo onesha uhodari wao walikopita.

Ronald Reagan alikuwa muigizaji wa filam Hollywood kabla ya kuingia siasa...alishinda Ugavana...kabla ya scandal kubwa Sana kumkumba Rais Jimmy Carter akiwa madarakani kule Iran...ndo Ronald Reagan akagombea Urais akashinda.

Ronald Reagan alikuwa anaonekana kama kibaraka Tu wa kundi lililokula njama za kuhakikisha Jimmy carter anashindwa Urais....kejeli zilikuwa nyingi sana na kejeli ziliendelea hata alipomaliza Urais cha ajabu ukiangalia mafanikio Reagan anatajwa kama mmoja wa Marais waliofanikiwa Sana kuindeleza USA alibadili sheria nyingi

Sana .. kiuchumi alifanya mabadiliko makubwa Sana yeye na Margaret Thatcher wa Uingereza ndo waasisi wakubwa wa Sera za kuitoa serikali Kwenye biashara za kila siku na kuacha private sector zishike biashara hizo... Margaret Thatcher nae alipingwa mno huku jinsia yake nayo ikiguswa ..alikuja kusifiwa baadae Sana Akiwa keshatoka Madarakani.

Samia kuwa Rais wa kwanza mwanamke... katika Taifa lenye mfumo dume sugu .. Taifa lenye ushirikina sugu wa kuanzia kuua albino hadi wa kukesha makanisa ya maombi..usitegemee atapata safari yenye Urais wa chochote atakacho fanya...stereo types zitafanya baadhi wahoji kila kitu na wasiamini chochote.

Wapo wanaotaka waziwazi wasikie Kikwete anasemaje ndo waamini Samia ana maamuzi sahihi...kwao Kikwete au Kiongozi wa kiume yeyote level ya Urais ndo "kigezo" cha kuwa Samia kafanya sahihi au la ...mfumo dume unafanya kiongozi wa upinzani asihoji akili za mwanaume mwenzie mwenye PhD ambae ni waziri husika lakini anaenda moja Kwa moja kumshambulia Rais na akili ya Rais huku akijua Rais sio Mtaalam wa mikataba...hata hao kina Kikwete na Magufuli ama Kwa kushauriwa sahihi au la walisaini mikataba iliyokuja kuleta shida mbele ya safari...lakini Mradi Rais ni mwanamke na wanaomkosoa wanachapa Hadi vibao na fimbo wake zao basi Rais lazima atatukanwa hadi akili yake.

Ronald Reagan alitukanwa Kwa kupenda sherehe white house za kila mara ... Wengine walimuona ni "muigizaji Tu kutoka Hollywood" anaepewa maelekezo na "wajuzi".

Lakini hata hao wajuzi walikuja kukubali very late kuwa Reagan alikuwa Rais alieweza fanikisha Mengi mno kuliko Marais walionekana "wajuzi" kumzidi.... kuanzia kuiangusha Russia...na kumaliza cold war Hadi kuitoa Serikali kwenye biashara na kuacha sekta binafsi inawiri.

Mmoja wa wasaidizi wake alieonekana kama mjuzi kumzidi George H Bush alipokuja kumrithi alifanikiwa Jambo moja Tu kukamilisha la kumaliza cold war na kuiunganisha German...lakini alishindwa vibaya mno kwenye uchumi Hadi akaibuka jamaa anaitwa Bill Clinton akaja kuchukua Urais.

Sometimes Urais ni zaidi ya akili na ujuzi, sometimes Urais au uongozi ni "baraka tu" wakristo wanaita "Kibali" Mungu anakupa.

Tuache fitina na kejeli..na kumshambulia Kwa jinsia yake.

Tusije kuja kumthamini very very late...
 
Uzuri wanaoongozwa wanaoongozwa kweli
FB_IMG_16898532174464364.jpg
 
Sidhani kama Samia anakosolewa kwasababu ni Mwanamke, ni kwasababu ni Rais. Samia sio mtaalam wa Mikataba yes Sasa kwanini asaini kitu asichokijua? Magufuli alishutumiwa sana kwasababu watu walikuwa wakiuawa kimyakimya , lakini Magufuli asingeachwa kushutumiwa eti kisa tu yeye sio mtaalam wa matukio ya mauaji yaani kisa sio mtaalam wa ujasusi basi asilaumiwe.

Samia hashutumiwi kwasababu ni Mwanamke, anashutumiwa kwasababu ni Rais. Urais ni Taasisi, sio Samia.
 
Ronald Reagan?

Huyo naye ni mfano wa kupotezea muda kuwaeleza watu juu yake?

Kweli watu mmekosa pa kushikia na project zenu hizi zisizokuwa na mwelekeo kabisa!

Au kwa vile alitamka tu: "Mr Gobarchef Tear Down this Wall"?
Hiyo ndiyo iwe sifa ya kumzungumzia hadi hapa JF?
 
Ni kweli wabongo tuna kelele nyingi kweli lakini me naona asee kwa samia sioni kuzuka kwa mfumo dume wowote zaidi kuu ni watu kupishana kwenye maslahi anayeguswa maslahi yake anashangilia anayesahaulika analalamika !!
Hakuna anayemsema vibaya Madam kwa sababu ya Jinsia !! Ni kila mtu anatetea machaguo yake ! Na sio rahisi kuyafanya yote atafanikisha baadhi ! Mengine yataendelezwa na wengine !!
Halafu mtu akishakua mkuu wa nchi lazima lazima tutafute udhaifu tu hata angenyoosha kiasi gani tutatafuta nyufa tu ! Ni moja ya kumkumbusha majukumu yake na wapi pa kuziba ! Ndo maana ya Demokrasia
 
Kuna mambo umeandika ni mazuri boss hongera.

Napinga unapotuchukulia tunaompinga katika misingi kuwa tunampinga eti kwa sababu aliyefanya maamuzi ni 'mwanamke' hivyo ni kana kwamba hafit kwa mujibu wa mindset zetu za mfumo dume.

Ishu si kuwa ana washauri ambao ni maphd na yeye hana PhD, ishu yeye ni rais wa nchi. For good for sake atakachofanya tutasema yeye ndio amefanya apatie ama akosee.

Hili la bandari rais ametukosea sana kwasabu alishauriwa na akaingia, je kama alishauriwa kwa maslahi ya watoa ushauri??

Huu ndio mzizi wa yote haya.
 
Hapa unataka kusema tuwe na subra kwamba kuna maajabu anawezafanya katika taifa hili au ni kitu gani unataka tujifunze?

Hakuna namna huyu kiongozi anaweza fanya maajabu if actors ndio sisi(praise and worship team).Unapataka kuleta hoja ya raisi wa Marekani hapa kulinda hoja au kueleza kitu jaribu kuona,who were actors(people),when(time).Rais anaweza kuwa kituko lakini kama watu wake ni makini unaweza usione mapungufu yake.Muda pia ni jambo la msingi but the good news is-rais wako hana maajabu ata akipewa muda aongoze mpaka ujio wa bwana
 
Kumfananisha reagan na huyu mama ni kumkosea heshima reagan

Reagan alikuwa mchumi mbobevu sasa uyu mama yetu bwana basi tu
 
Watu wanapinga kitu very specific kwa Samia, kama ambavyo walipinga kwa Magufuli.

Mbona wengi tu walimsifia hapa alipofanya vizuri. Mkataba ule ni wa hovyo!!! Na hiyo ndio hoja ya watu, sio uanamke wake au kitu kingine chochote.

Wakati wa JPM kulikuwa na ukatili na ujambazi wa kidola, mbona alipigwa spana kila kona. Pamoja na kubinya uhuru lakini watu walikuwa wanapinga tu.

Akina Mdude ni walewale, wamepinga sana na kupitia mengi wakati wa JPM. Akila Lissu, vipi tuseme na yeye walikuwa wanampinga kwa sababu binafsi au ni sera na matendo yake??
 
Back
Top Bottom