Rais Samia mwanzo mzuri anga za kimataifa

Ojuolegbha

Member
Sep 6, 2020
22
75
RAIS SAMIA MWANZO MZURI ANGA ZA KIMATAIFA

Na Malya Ngumu Charles

Ilisemwa huko zamani na wahenga na wahenguzi kwamba, “It’s not how you are, but what people thinks how you are that counts”. Kwa tafsiri isiyo rasmi, hoja siyo jinsi ulivyo isipokuwa jinsi watu wanavyofikiri ulivyo ndiyo watakavyo kuchukulia.

Kanuni hii inahusika na maisha yetu moja kwa moja kama mtu mmoja mmoja, familia na hata taifa.

Kwamba maisha ni watu ni ukweli ambao wengi wetu tunaukubali, ukichukulia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja au familia,

anayeshirikiana na wenzake katika hali zote, wanamjua na wanafahamiana, hivyo siku akihitaji washikaji zake wamashike mkono kwenye suala lolote iwe tatizo la ugonjwa au msiba, au jambo la furaha kama sherehe za harusi, kama ubatizo, kipaimara na mengine, au hata anataka mkopo wa ada na kujikwamua kwa changamoto yoyote ile, rafiki zake watakuwepo kushikamana naye,

wanaweza wasiwe wote lakini maadam anao wa kutosha, wapo watakaojitokeza katika hali zote, ndiyo maana wahenga wakasisitiza, “Make friends before you need them, ” kwamba tengeneza marafiki sasa ili hata ukipata shida uwe tayari na watu wakukusaidia.

Ndivyo ilivyo katika diplomasia ya kimataifa, Rais akijuana na wakubwa wa Dunia, wakawa wanapata muda wakuzugumza na kujadiliana mambo mbalimbali ana kwa ana, inajenga ‘rapport’ maelewano mazuri kati ya taifa na taifa, taifa na Taasisi zozote muhimu ambazo kwakweli zinahitajiana sana.

Rais SAMIA Suluhu Hassana, akiwa NewYork tayari amekutana na Rais wa Benki ya Dunia, Mkuu wa World Trade Organization–WTO na UNHCR na wengine,

malengo ya msingi katika mikutano ya viognozi kama hii ni kujenga kwanza maelewano na uhusiano na Taasisi kubwa kubwa Duniani zenye maamuzi ambayo mara nyingi huathiri namna tunavyoendesha uchumi wetu, lakini Zaidi sana ni kujenga na kuimraisha ushawishi wa Tanzania katika uga wa kimataifa.

Nchi ikiwa na ushawishi mkubwa kimataifa, ziko faida nyingi ambazo taifa linapata lakini hazionekani moja kwa moja kwamba zimetokana na ushawishi huo, ingawa kutoonekana kwake moja kwa moja hakuondoi ukweli kwamba zimetokana na ushawishi wa viongozi wa nchi husika.

Viongozi wanao onana na kuzungumza ana kwa ana hujenga hali ya kuaminiana na kushawishiana, ili siku ya siku ukiwa na jambo lako unataka lifanikiwe, ni rahisi kupigia simu viongozi kadhaa Duniani ambao Rais ana fahamiana nao kushawishi jambo lake na hapo nchi inafaidika kutokana na mahusiano yaliyojengwa kabla.

Ni kwamuktadha huohuo, ndiyo maana viongozi wa Mataifa makubwa kama Marekani na China, wanatembea Duniani kote kujenga ushawishi wa kimataifa kwa manufaa ya nchi zao hata kama wana uchumi mkubwa, lakini wanajua nguvu ya mahusiano kimataifa.

Rais SAMIA kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Tanzania, anatumia nafasi hii kuiambia Dunia kwamba ustaarabu wetu umefika kiwango cha juu kiasi kwamba Mwanamke leo yuko katika ofisi ya juu kabisa nchini kuliko zote kitu ambacho mataifa mengine badot wanapambana kupata rais Mwanamke.

Hilo tu peke yake linaweza kujenga ushawishi mkubwa hasa kwa wanaharakati wa haki za jinsia Duniani kuiweka Tanznaia katika mizani tofauti na hivyo kuongeza ushawishi wetu kamataifa katika masuala mbalimbali Duniani.

Diplomasia wakati wote ni suala la kujenga wasifu wako (brand) ili wakati wote watu waaamini kwamba wewe ni bora na muungwana zaidi, na kwakufanya hivyo unaweza kupata ukitakacho bila kutoa jasho la ziada.

Hiki ndicho anachokifanya Rais SAMIA, anajenga mahusiano, anatengeneza marafiki, anachomeka kwenye akili za wakubwa wa Dunia fikra mpya kuhusu Tanzania, na wakianza kutuona kama wenzao, bila shaka itaturahisishia mambo mengi kama Taifa.


Kongole Rais SAMIA
IMG-20210924-WA0002.jpg
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,815
2,000
'Kwa aibu'. Unafikiri hata issue ya Mange walipenda?

Walifanya Kwa sababu wako kwenye macho ya viumbe first class.

Mange kama mwanamke ajichanganye ashuke JK Nyerere.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom