Comrade Ally Maftah
Member
- Nov 6, 2016
- 65
- 166
MFARIJI MKUU WA TAIFA DR SAMIA SULUHU HASAN
Na Comrade Ally Maftah
Dr. Samia Suluhu Hasan akiwa katika wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara, akiwafariji walioathiriwa na janga la Mafuriko
Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, amefanya jambo kubwa sana na la kiungwana kama ilivyo kawaida yake kuwajali wagonjwa, na walio kwenye changamoto kama mtakumbuka Dr. Samia akiwa Makamu wa Rais alikuwa akiwatembelea viongozi wa upinzani waliokuwa katika changamoto mbalimbali hadi mahospitalini, pasipo kujali kwamba pengine viongozi wenzake wa chama watamchukuliaje, yeye alitanguliza utu kwanza masuala ya vyama hakuyaweka mbele.
Dr. Samia amewatembelea waathiriwa wa janga la mafuriko pasipo kujali itikadi za vyama vyao. kwa kuzingatia kwamba ilani inayotimizwa sasa ni ilani ya Chama cha Mapinduzi na msimamizi mkuu wa Ilani ni Dr. Samia.
Nawaomba ndugu zetu wapinzani msichukulie hili janga la watanzania wenzetu kama mtaji wa kisiasa, nchi yetu inapaswa kuwa katika utulivu na mshikamano kama ambavyo Rais Dr. Samia anavyosisitiza na kutuunganisha watanzania wote.
Comrade Ally Maftah
-Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
-Mjumbe Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam