Rais Samia: Kwenye ajira za Wizara ya Mambo ya Nje mnawabeba watoto wa viongozi, wafanye kazi au wasifanye mnawabeba

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,835
Ni jambo jema kama Rais Samia umeliona jambo hili la upendeleo Kwa Watoto wa Viongozi na Vigogo wakiwepo Watoto wako.

Hakuna mtu anasema Watoto wa Viongozi wasipate kazi ila kuwe na mazingira shindani na mtu apate kazi Kwa merit sio Kwa connection na jina la ukooo wake au Mzazi wake.

Hili swala kwa Tanzania hii limekuwa Sugu na Serikali ya Mwendazake ndio ililileta hasa kwenye nafasi za Uteuzi na wewe umeliendeleza.

Ushauri wangu, kwenye nafasi za Uteuzi mnazolenga kulinda chama chenu mnaweza endelea kuteuana Kwa sababu mnasababu za kufanya hivyo but kwenye nafasi zinazohitaji utaalamu Chonde Chonde vigezo, masharti na sifa zizingatiwe Ili walau Watoto wa Maskini wapate fursa na kiuhalisia walio wengi ndio wenye uwezo kuliko Watoto wa vigogo.

View: https://youtu.be/gmGtTmck-zQ?si=xYKT3n3lKl2e63Qm

My Take:
Kujirekebisha kusiishie Wizara ya mambo ya Nje tuu Bali nafasi zote ambazo ni nono kama Tanapa, TanRoads, BoT, NSSF, EWURA,TCRA nk.
 
Watoto wa Viongozi wanatakiwa wawe Jeshini ila Hapa Tanzania hilo limeshindikana liliishia kwa Makongoro na John tu!

Hapa utawakuta BoT na TRA 😂😂
Huko wanaogopa na hata wakiwepo wanakuwa kwenye nafasi za uafisa wa Juu ila huwezi wakuta kwenye oparesheni shenzi sana hao kinyume na Nchi zingine.

May be Kwa sababu Bado tuko kwenye njia ya kutafuta ustaarabu wa kweli.

Naunga mkono Katiba Mpya itoe fursa Kwa wote japo Machadomo wasidhani with Katiba Mpya wataitoa ccm kirahisi.
 
Nani ANATEUA/

HUYU BIBI AMESHAPOTEZA MWELEKEO WALA KUMBUKUMBU.
Watoto wa vigogo wameanza kuteuliwa na Samia au ni utamaduni wa ccm miaka na mikaka? Rais hafanyi vetting analetewa na timu ya vetting ndio yeye anateua kutoka humo.

So sio kazi ya mtu mmja hiyo na mtu mmja haiwezi.
 
Ni jambo jema kama Rais Samia umeliona jambo hili la upendeleo Kwa Watoto wa Viongozi na Vigogo wakiwepo Watoto wako.

Hakuna mtu anasema Watoto wa Viongozi wasipate kazi ila kuwe na mazingira shindani na mtu apate kazi Kwa merit sio Kwa connection na jina la ukooo wake au Mzazi wake.

Hili swala Kwa Tanzania hii limekuwa Sugu na Serikali ya Mwendazake ndio ililileta hasa kwenye nafasi za Uteuzi na wewe umeliendeleza.

Ushauri wangu, kwenye nafasi za Uteuzi mnazolenga kulinda chama chenu mnaweza endelea kuteuana Kwa sababu mnasababu za kufanya hivyo but kwenye nafasi zinazohitaji utaalamu Chonde Chonde vigezo, masharti na sifa zizingatiwe Ili walau Watoto wa Maskini wapate fursa na kiuhalisia walio wengi ndio wenye uwezo kuliko Watoto wa vigogo.

View: https://youtu.be/gmGtTmck-zQ?si=xYKT3n3lKl2e63Qm

My Take
Kujirekebisha kusiishie Wizara ya mambo ya Nje tuu Bali nafasi zote ambazo ni nono kama Tanapa, TanRoads,BoT,Nssf,Ewura,TCRA nk.

Nashukuru sana mama Samia kaliona hilo tatizo.
 
Back
Top Bottom