Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 710
- 1,610
Ya kweli haya ndugu zangu?
Kila kitu pipo shwari baada ya uchaguzi? Mambo yamerejea kama kawaida na uchumi umekua?
=====
"Tanzania tuko watulivu na tuko sawa. Kisiasa, kila kitu kiko chini ya udhibiti baada ya uchaguzi wetu wa Oktoba. Sasa nchi imerejea katika hali ya kawaida na tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida.
Kama mnavyoweza kuona hapa Arusha, kila kitu kiko sawa. Baada ya matukio yale, niliunda Tume ya Uchunguzi ambayo tunasubiri ripoti na mapendekezo yake. Hii itatuongoza kuunda Tume ya Maridhiano itakayotekeleza mapendekezo hayo, na baadaye tutafanya mapitio ya Katiba yetu.
Kiuchumi, tunafanya vizuri sana. Mwaka jana tulikua kwa asilimia 6% na mfumuko wa bei umebaki katika tarakimu moja, tukiwa tunacheza kati ya asilimia 3.5% hadi 4%. Bado hatujafika asilimia 5%.
Lengo letu kuu kiuchumi ni kuleta mabadiliko kupitia kuongeza thamani ya bidhaa na ukuaji wa viwanda. Pia, tunajikita katika kuendeleza rasilimali watu, tukizingatia kuwa asilimia 60% ya nguvu kazi ya taifa letu ni vijana. Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili yao."
Rais Samia amesema hayo wakati wa majadiliano kuhusu ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Ghana yaliyofanyika katika Ikulu Ndogo mkoani Arusha.