Rais Samia,kuwa makini na wasaidizi wako.

Rais Samia,kuwa makini na wasaidizi wako.

Huu mtandao wa X ufungwe tu. Watanzania Tumezidi umbea na uvivu. Hata JF ifungwe tu. Ifike wakati tuache uvivu na umbea twende tukafanye kazi. Uwezo wetu hupo kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi hivyo vitatatu tunaweza na kutuinua kiuchumi.
Hivi mnaosemaga mtandao Fulani ufungwe watu wafanye kazi huko mnapofanyia kazi nynyi huwa mnafanya 24hrs hakuna muda wa kurefresh ?

Let say mtu anafanya kazi ofisini kwake 8hrs hayo 16hrs unataka awe amelala? Hali yakuwa Hata ushauri wa Dr kulala ni 8hrs

Huwa Napata maswali magumu na kuguess kazi ya muhusika nikimuona mtu anadai watu hawafanyi kazi kisa mtandao.
 
Zimetapakaa Taarifa kuwa mtandao wa X zamani Twitter utafungiwa na Serikali.
Yumkini chokochoko hizo zinatengenezwa na vijana wa UVCCM pamoja na wasaidizi wako wachache wanaopenda kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili waendelee kubakia kwenye nafasi zao.
Rais Samia,ni vyema utambue kuwa nafasi uliyonayo ni ngumu na nzito sana.
Unapokuwa kiongozi mkuu,unageuka kuwa jalala,kila mtu anatupia uchafu kwa kadri anavyojisikia.
Hakuna kiongozi asiyetukanwa Duniani,awe mwema au mwovu, sasa hao wana CCM kama wanaona mtandao wa X unakukosoa au kukutukana eti ufungiwe watakuharibia kabisa.
Utaonekana kiongozi wa hovyo anayechukia Uhuru wa Habari.
Wanataka usifiwe tu Eti usikosolewe kwani wewe umekuwa Mungu?
Kumbuka walivyokuwa wakimsifia Magufuli na baada ya kuondoka Duniani wanamzodoa sasa hivi.
Rais Samia, wewe ni mwanadamu,una mazuri yako na mabaya yako.
Epuka machawa watakupeleka pabaya sana.
ni vizuri kuwa wakweli ndrugu zango....
na ni vizuri kutetea mambo muhimu na yenye tija. haina maana kulinda uhuru unaodhalilisha utu na heshima ya Taifa kwa ujumla 🐒

mh.Rais Comrade Dr Samia Suluhu Hassan, hachukii, hakatazi wala hakatai kukosolewa na mTanzania yeyote yule hata kidogo, iwe kwa hoja au bila hata hoja.....

Ila matusi ya nguoni kwa viongozi binafsi tena wazi wazi kabisa. hiyo siyo sawa, tabia hiyo haivumiliki, haiana maana wala nafasi yoyote kwa Taifa letu lililostaarabika sana....

na nadhani Lazima kuchukua hatua za makusudi, kali sana kudhibiti utovu huo wa kimaadili unaoutetea.

vyombo vya kitaifa na kimataifa vinavyo intertain hali hiyo humu nchini, vidhibitiwe, ili kulinda mila, desturi, utamaduni na heshima kwa viongozi wa nchi na ustaarabu miongoni mwa waTanzania 🐒

viongozi na mamlaka za nchi ziendelee kutathimini mienendo ya mitandao ya kijamii inayokiuka maadili ya kistaarabu na kumshauri Rais hatua muhimu za kuchukua ili tuendelee kua wamoja kama Taifa la wastaarabu 🐒
 
Back
Top Bottom