Rais Samia kuongoza zoezi maalum la upandaji miti Zanzibar katika Kuadhimisha Siku yake ya kuzaliwa Januari 27,2026

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
260
Reaction score
199
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ataongoza zoezi maalum la upandaji miti litakalofanyika tarehe 27 Januari, 2026, maeneo ya Bungi Kilimo na Kizimkazi, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Zoezi hili lenye kaulimbiu “Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Shiriki Kupanda Miti” linaakisi dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia katika kuendeleza ajenda ya Taifa ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira, ikiwemo upandaji miti, ulinzi wa vyanzo vya maji, kuimarisha uoto wa asili, na kuchangia kwa vitendo juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, zoezi hili ni ishara ya uwajibikaji wa pamoja na linatoa fursa kwa kila mmoja, kwa nafasi yake na mahali alipo, kushiriki katika kulinda na kuenzi mazingira kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.

Mheshimiwa Rais anatoa wito kwa Watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa hiari, wakitambua kuwa ulinzi wa mazingira ni msingi wa uhai, maendeleo, na usalama wa Taifa.

HalikaDhalika, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inawahimiza wananchi, taasisi na wadau wa mazingira kuunga mkono dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuendeleza ajenda ya uhifadhi wa mazingira, ikiwemo kupanda angalau mti mmoja nyumbani, shuleni, kazini, au kwenye maeneo ya jamii.
IMG-20260122-WA0015.jpg

Kwa nini awamu hii samia anatumia muda mwingi kujifungia huko zanzibar had tunapata hisia kwamba nchi ameachiwa mwigulu.
 
Mama wa shughuli,kwake hamna jambo dogo.hata siku ya kuzaliwa ni jambo la kitaifa?kweli ni kupatwa kwa Tanganyika
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ataongoza zoezi maalum la upandaji miti litakalofanyika tarehe 27 Januari, 2026, maeneo ya Bungi Kilimo na Kizimkazi, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Zoezi hili lenye kaulimbiu “Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Shiriki Kupanda Miti” linaakisi dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia katika kuendeleza ajenda ya Taifa ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira, ikiwemo upandaji miti, ulinzi wa vyanzo vya maji, kuimarisha uoto wa asili, na kuchangia kwa vitendo juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, zoezi hili ni ishara ya uwajibikaji wa pamoja na linatoa fursa kwa kila mmoja, kwa nafasi yake na mahali alipo, kushiriki katika kulinda na kuenzi mazingira kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho.

Mheshimiwa Rais anatoa wito kwa Watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa hiari, wakitambua kuwa ulinzi wa mazingira ni msingi wa uhai, maendeleo, na usalama wa Taifa.

HalikaDhalika, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inawahimiza wananchi, taasisi na wadau wa mazingira kuunga mkono dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuendeleza ajenda ya uhifadhi wa mazingira, ikiwemo kupanda angalau mti mmoja nyumbani, shuleni, kazini, au kwenye maeneo ya jamii.

Ili kuokoa matumizi, Ikulu ihamishiwe Kizimkazi au Unguja kwa muda mpaka atakapoondoka madarakani.
 
Chama cha kizalendo kinazuiwa huko napo zuio lihusike
 
Ameanza kupoka madaraka ya Mwinyi. Akumbushwe akapande hiyo miti Chamwino.
 
Mama wa shughuli,kwake hamna jambo dogo.hata siku ya kuzaliwa ni jambo la kitaifa?kweli ni kupatwa kwa Tanganyika
Akapande ofisini kwake Dodoma ikulu, vinginevyo ni matumizi ovyo ya kodi zetu. Huko anakotaka kupanda amwachie Mwinyi
 
Back
Top Bottom