Rais Samia, kuna Fursa nyingine huko 'Kazungula Bridge'

Pamoja na kwamba umewaza mambo ya kimaendeleo lakini mengi ya uliyowaza kiuchumi hayana tija kwa nchi..kwanza si rahisi kuzifanya Botswana hata malawi kutegemea port za Tz eti kwa kupokea bidhaa zinazotoka mashariki ya kati, south afrika ina kila kitu ambacho nchi hizi zinahitaji, lkn hata tu mila, desturi na utamaduni wa watu wa nchi hizi wanajisikia vzr zaidi kushirikiana na south africa kuliko kutegemea east africa.

Daraja la kazungula limejengwa kuziwezesha nchi za kusini zishirikiane zaidi kibiashara, itakuwa ni kupoteza rasilimali za nchi kutaka kushindania soko la nchi za kusini. Tz inazungukwa na nchi 8 je tayari fursa zilizopo kwny nchi hizo imezitumia kikamilifu? Kama bado basi vyema nguvu kubwa ielekezwe huko na si kucheza pata potea unayopendekeza wewe.

Hii ni biashara. Kama biashara itaonekana inawalipa wanaokuja Dar, kwanini isiwezekane? Sasa hivi Durban ndio reliable port. Ni mbali kweli kweli. Beira ugaidi na mapigano ya ndani yanaifanya isiwe rafiki sana
 
Samahani ndugu, hiv unavyoaddress haya uliyoandika kwa Rais una uhakika yanamfikia au unajua kuwa humu kuna chawa wake au umemtumia physical letter ama kivipi vipi.

Na sio wewe tu naona watu wengi wanapenda kuandika humu kwa kuaddress public figures as if wanaongea nao muda huo huo, hapo hapo au kama wanacomment kwenye posts zao, au mimi ndio sijui mnachomaanisha?

Naomba mnieleweshe!

Thanks!
Humu JF ndio home of all ngazi za maamuzi..hata usiogope wapo wengi tu nanasoma na kuchukua taarifa..hata kwenye uzi wa kula kimasihala wapo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni biashara. Kama biashara itaonekana inawalipa wanaokuja Dar, kwanini isiwezekane? Sasa hivi Durban ndio reliable port. Ni mbali kweli kweli. Beira ugaidi na mapigano ya ndani yanaifanya isiwe rafiki sana
Unaemuelewesha sidhani kama anajua lolote juu ya biashara hasa baina ya mataifa
 
Naunga mkono daraja kwa malengo ya baadae, lakini kwa sasa hivi tunachelewa sana kujihusisha kati yetu na DRC.

Inatubidi tuweke juhudi kubwa kufanya biashara na nchi hii kwa karibu zaidi kuliko ilivyo sasa.

Mimi napendekeza, kwa malengo ya muda mfupi (5 years); pawepo na meli na bandari kadhaa, tokea kusini na mpaka na Zambia hadi mpakani na Burundi.

Sambamba na kuwa na meli kadhaa na bandari, tutumie njia kavu inayopitia Burundi na Rwanda, na hata Uganda kuingia kwenye soko la DRC.

Hii ina maana kwamba, lazima tuwe na Bandari zinazofanya kazi vizuri na Barabara pamoja na reli.

Bandari ya Dar es Salaam pekee haitamudu.

Nchi yetu inayofursa hii adhimu sana tuliyopewa na Mwenyezi Mungu; sasa ni wakati tuitumie ili itusaidie kuleta mabadiliko chanya kwetu.
Hapo mwishoni nakubaliana na wewe kuhusu Bandari ya Dar es Salaam kutomudu changamoto tulizo nazo kwa sasa!

Msisitizo uwekwe Bandari ya Bagamoyo ili tuweze ku dominate biashara katika ukanda wetu huu na investiment kubwa ifanywe zaidi kwenye kujenga Bandari kubwa za kisasa mikoa ya mipakani na kuboresha miundombinu hasa ya reli na barabara kuelekea nchi jirani
 
Kama MWENDAZAKE alikuwa anaifuatilia hadi "SHILAWADU" sembuse Mama iwe ngumu kuingia Jamiiforum ?!

Kwa wasiyojua "JAMIIFORUM" ni miongoni mwa vyanzo muhimu sana vya taarifa vinavyotegemewa na serikali .

Humu kuna zaidi ya 89.3% ya viongozi wakuu wa serikali .

Kwamuhitimisha na bila kujali itikadi na mlengo wa KISIASA wa mtoa mada naomba tu niseme kuwa jamaa amewaza kwa upana sana na kwa nyongeza nikwamba jamaa ameiwasirisha mada kwa viwango vya kimataifa na nimtie moyo kwamba yeye ni miongoni mwa watu wanauoutumia vyema sana ufahamu wao kwenye eneo zima la kufikiri .

Kwakifupi tu :-
Tanzania inauwezo wa kuyatekeleza hayo yote aliyoyaeleza hata tu ndani ya miaka mitano kama tu tutaamua kwa pamoja kuyatekeleza .

Japo siyo kwa umuhimu .

Mzeebaba ndani ya miaka mitano na miezi sita na siku ishirini na tisa alizokaa ikulu ameongeza deni la Taifa kwa kiasi cha Tsh Trillion 30.8 according to CAG report ,hiki kiasi ni mara sita ya viongozi wenzake wote waliyomtangulia , tusipanic , hebu turelax maana ndiyo ishakuwa hivyo , hebu jengeni picture tena kwa utulivu wenu wa chooni tu unadhani maendeleo anayoyaeleza mwamba hapo yanagharimu kiasi gani cha pesa? Unadhani maendeleo yanayohubiriwa kutendwa na mzeebaba yanamaliza hata trillion 10? Let's wake up guys tusijichukulie poa , Taifa imara linajengwa na mipango na sera imara na dhamira mashubuti .

Don't understimate yourself and limit your thinking .

Hata inzi anaweza kutengeneza asali siku atakayoacha ufala .
Asante Ndugu
 
Hapo mwishoni nakubaliana na wewe kuhusu Bandari ya Dar es Salaam kutomudu changamoto tulizo nazo kwa sasa!

Msisitizo uwekwe Bandari ya Bagamoyo ili tuweze ku dominate biashara katika ukanda wetu huu na investiment kubwa ifanywe zaidi kwenye kujenga Bandari kubwa za kisasa mikoa ya mipakani na kuboresha miundombinu hasa ya reli na barabara kuelekea nchi jirani
Huu ni utajiri uliopo wazi kwa nchi yetu, lakini hatuuchangamkii ipasavyo sijui kwa nini!
 
Mambo mazuri na ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya nchi yanapangwa na kuchagizwa na sheria zilizo bora kabisa. Mambo yote haya yanapangwa na viongozi wa kisiasa kwa kufuata ushauri wa wataalam.

Badly enough; kule Bungeni viongozi wapo bize kuwarushia Mbowe na CDM vijembe na kusahau kilichowapeleka Bungeni.
Unakaa unajiuliza kwanini Mizigo mingi inapitia Zambia kuingia Congo? kwamba miaka yote serikali inashindwa kujenga Bandari na kuweka Meli kubwa hapo ziwa Tanganyika?
Miaka mingi barabara ya TABORA-SIKONGE-MPANDA imekua tabu kwelikweli.
Barabara ya TABORA-KALIUA-NJIAPANDA YA UVINZA-MPANDA nako tabu tupu.

Alafu wengine wakaenda mbali zaidi wanajenga daraja la Salander kweli? wakajenga uwanja wa ndege pale Chato kweli?
Wakajenga Lami kutoka Namanyerere adi kibaoni kwao Pinda kweli? na umuhimu wa kuunganisha Katavi..Tabora na Congo inazidi umuhimu wa Salander na Chato Airpot.

Majuzi nilikua pale boarder Kasumulu Kyela na Malawi; sasa unajiuliza boarder inajengwa alafu barabara imebaki nyembamba kama mkia wa kiboko.
Viongozi wetu jirekebisheni muangalie kinachoweza kuungamisha fursa kwa wananchi wetu.
Chato ata mabasi ya abiria yenyewe hawapati wasafiri itakua ndege?
 
Naunga mkono daraja kwa malengo ya baadae, lakini kwa sasa hivi tunachelewa sana kujihusisha kati yetu na DRC.

Inatubidi tuweke juhudi kubwa kufanya biashara na nchi hii kwa karibu zaidi kuliko ilivyo sasa.

Mimi napendekeza, kwa malengo ya muda mfupi (5 years); pawepo na meli na bandari kadhaa, tokea kusini na mpaka na Zambia hadi mpakani na Burundi.

Sambamba na kuwa na meli kadhaa na bandari, tutumie njia kavu inayopitia Burundi na Rwanda, na hata Uganda kuingia kwenye soko la DRC.

Hii ina maana kwamba, lazima tuwe na Bandari zinazofanya kazi vizuri na Barabara pamoja na reli.

Bandari ya Dar es Salaam pekee haitamudu.

Nchi yetu inayofursa hii adhimu sana tuliyopewa na Mwenyezi Mungu; sasa ni wakati tuitumie ili itusaidie kuleta mabadiliko chanya kwetu.
Good analysis

Umeeleza vyema Sana na nafurahi kuona ukiwa na mawazo chanya kwa mustakabali wa Taifa letu .

Nimefurahi kuona ulichokuwa unakipinga kule ndicho ulichokiungamkono huku ,kule niliamua kusitisha mjadala Baada ya kubaini kuwa wewe ni mkongwe mwenzangu humu ,much kudos jombaa.

Wewe jamaa uko na akili sana basi tu vile unaamuaga
 
Unaonekana hukuelewa chochote nilichokuwa napinga kule.
Lakini najua kwa nini ulizima ubongo wako ili usinielewe, kwa sababu mada ile uliyoianzisha ilikuwa inaeleza kila kitu juu ya ulikonadisha akili yako.
 
Mkoa wa Mbeya umelaza sana damu kwani hawajaweza kucapitalize economic potential ya kufanya biashara na Malawi!!
Uchumi wa Tanzania unashikwa na biashara na nchi za Zambia, Malawi, Congo na Zimbabwe. Huku ndo mizigo Mingi inaenda alafu ukiangalia kwa kina hii ndo mikoa iliyosahaulika zaidi kimiundombinu pamoja na Tabora na Kigoma.

Kusema kweli ukifikiria kwa kina Reli ya TAZARA ndo ilitakiwa kuboreshwa zaidi na kufanywa kuwa SGR huku ikiwekewa umeme kutokana na hii reli ndo inayoenda kwenye njia yenye uchumi wa Tanzania.

Napendekeza Mama Samia aiangalia sana hasa kwenye kuiboresha kimiundombinu mikoa ya Mbeya na Songwe kuanzia kwenye barabara hadi kwenye reli.

Hii ni mikoa ambayo hata serikali ikiamua kufanya ujenzi wa miundombinu kwa mfumo wa PPP kuna uhakika wa faida kurudi mapema na kwa wakati kwa sababu huku uchumi ni usafirishaji na biashara.
 
Mambo mazuri na ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya nchi yanapangwa na kuchagizwa na sheria zilizo bora kabisa. Mambo yote haya yanapangwa na viongozi wa kisiasa kwa kufuata ushauri wa wataalam.

Badly enough; kule Bungeni viongozi wapo bize kuwarushia Mbowe na CDM vijembe na kusahau kilichowapeleka Bungeni.
Unakaa unajiuliza kwanini Mizigo mingi inapitia Zambia kuingia Congo? kwamba miaka yote serikali inashindwa kujenga Bandari na kuweka Meli kubwa hapo ziwa Tanganyika?
Miaka mingi barabara ya TABORA-SIKONGE-MPANDA imekua tabu kwelikweli.
Barabara ya TABORA-KALIUA-NJIAPANDA YA UVINZA-MPANDA nako tabu tupu.

Alafu wengine wakaenda mbali zaidi wanajenga daraja la Salander kweli? wakajenga uwanja wa ndege pale Chato kweli?
Wakajenga Lami kutoka Namanyerere adi kibaoni kwao Pinda kweli? na umuhimu wa kuunganisha Katavi..Tabora na Congo inazidi umuhimu wa Salander na Chato Airpot.

Majuzi nilikua pale boarder Kasumulu Kyela na Malawi; sasa unajiuliza boarder inajengwa alafu barabara imebaki nyembamba kama mkia wa kiboko.
Viongozi wetu jirekebisheni muangalie kinachoweza kuungamisha fursa kwa wananchi wetu.
Chato ata mabasi ya abiria yenyewe hawapati wasafiri itakua ndege?
Umeongea maneno mazito sana ndugu yangu. Malawi kwa walipo kijiografia kila kitu wanatakiwa kutegemea kutoka Tanzania. Kwa sababu hiyo sisi ndo tunatakiwa kulionesha Hilo na kulisimamia kwa kuhakikisha Kuna miundombinu Bora na ya kisasa zaidi kuingia Malawi. Barabara kuwa na viwango vya ubora, upana mzuri na wa uhakika bila kusahau miundombinu mingine.

Kwa mpaka wa Tunduma hali inatakiwa kuwa ivyo ivyo. Barabara zoote za kuingia Mbeya hadi Songwe zinatakiwa ziwe na Upana unaotakiwa na ubora unaotakiwa, reli ya TAZARA inatakiwa kuwa kiwango cha SGR na iwekewe kabisa umeme. Tukifanya hivi ndo Kweli tutakuwa serious kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania.
 
Amani iwe nawe Mama yangu.

Heri ya sikukuu ya Eid! Na Polee na uchovu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Kama nilivyotoa commitment ya kukuunga mkono Mara tu ulipochukua kiti cha kuongoza nchi yetu, leo napenda kuleta mada nyingine ya ushauri kwako ili tuutumie katika kuijenga na kuipeleka mbele kimaendeleo Tanzania yetu.

Hivi Karibuni, Botswana na Zambia wamezindua daraja la kuunganisha nchi zao linalojulikana kama Daraja la Kazungula. Daraja hili lililojengwa katika Mto Zambezi Lina njia za Magari kwa ajiri ya Magari na Pia wameweka sehemu ya kupitisha reli kwenye njia hii.

kukamilika kwa Daraja hili inaelezwa kuwa ni fursa adhimu ya kiuchumi kwa nchi zenye Bandari kuu za bahari hasa South Africa, Namibia na Tanzania kwa sababu daraja hili litazifanya hizi nchi kufanya biashara kwa kiwango kikubwa sana na kwa urahisi sana.

Tukiacha Namibia na South Africa , kwa Tanzania , nimeona kukamilika kwa daraja hili ni fursa kubwa sana ya kukua kiuchumi kwa Taifa letu endapo tu tutatumia hii kama fursa na kujitengeneza ki strategically hasa ukizingatia tukijipanga vizuri, mizigo yote ya Botswana na Zambia kutoka Middle East na Mashariki ya Mbali hasa Ulaya Mashariki na Asia( China na Japan) inaweza kuwa inapitishiwa Bandari zetu( Dar es Salaam na Bagamoyo Kama itajengwa) na kupelekwa kwao.

Hivyo kutokana na hii fursa, naomba serikali yako ianze kujipanga kufanya yafuatayo either yenyewe kama yenyewe au kwa kushirikiana na sekta binafsi.

1. Kujenga Bandari kubwa Kavu katika Mkoa wa Mbeya au Songwe, itakayokuwa inapokea mizigo yote Kwa ajiri ya nchi za DRC, Zambia, Zimbabwe na Botswana. Bandari hii itapokea mizigo hiyo kwa njia zote( Barabara na Reli kutoka Dar es Salaaam na Bagamoyo hapo badae

2. Kujenga upya miondombinu ya Mikoa ya Songwe na Mbeya. Naomba kwenye kufanikisha hili Mama yetu, angalia hata Kwa kufanya kupitia PPP( Kushirikiana na sekta binafsi) miundombinu ya kuingia Mbeya na Songwe hasa barabara ifumuliwe na kujengwa upya kwa viwango vya kisasa. Miji hii ina barabara nyembamba sana. Kuanzia Makambako hadi Mbeya na Songwe. Naomba mipango na utekelezaji uanze kufumua na kuzijenga kisasa katika viwango vipya vya ubora barabara hizi. Kwenye upana kuanzia makambako hadi songwe( Tunduma) na kuweka barabara zenye njia 3-4 kila line kwenye miji ya Mbeya na Tunduma ili kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo. Kumbuka Mama njia hii ndo imeshika uchumi wa usafirishaji kwa Tanzania.

3. Mpango wa kuibadilisha reli ya TAZARA kutoka ilivyo kuwa SGR inayotumia umeme. Naomba kwa mipango ya badae reli hii inayofika Hadi Zambia iangaliwe kubadilishwa iwe kwenye mfumo wa SGR. Iboreshwe na kujengwa upya kisasa kwa viwango vipya vya ubora (SGR)

Mwisho ingawa wazo hili linaweza kuonekana la kufikirika zaidi kuliko uhalisia naomba Serikali yako ianze kufanya mipango ya kujenga daraja linalokatisha Ziwa Tanganyika na kuingia Congo Moja kwa Moja. Ninajua Kuna changamoto kubwa sana hasa kwenye kina cha lile ziwa Ila kwa kiwango cha teknolojia kilivyofika duniani Nina uhakika wapo watu wanaoweza kufanikisha hili. Ikiwa tutajenga kwa upande wa Rukwa sawa na ikiwa tutajenga kwa upande wa Kigoma sawa Ila naomba iyo mipango ianze sasa. Hata usipokuja kujenga wewe kama Rais wa Awamu ya Sita ila siku moja Rais mwingine atajenga tu. Kikubwa naomba uanzishe hiyo mipango kwa hata kufanyika feasibility studies na kuangalia ni watu gani wataweza kufanya hivyo huko mbeleni. Nasema hivi Kwa sababu, kama Tanzania, tukiweza kupata direct access ya kuingia Congo kibiashara itakuwa na faida kubwa sana kiuchumi kwa Taifa letu kuliko kutegemea kuingia kule kupitia nchi zingine jirani.

Naomba kuwasilisha.

View attachment 1786878View attachment 1786879View attachment 1786880

Sahihisho dogo: kigezo rasmi cha SGR (Standard Gauge Railway) ni urefu kati ya reli ya kushoto na kulia (gauge) ambayo ni sentimita 1,435. Unaweza kufananisha na urefu wa axle ya magurudumu ya treni. Njia inaweza kuwa au isiwe ya umeme.

TAZARA imejengwa kwa kigezo cha Cape Gauge (sentimeta 1,067). Hii ndiyo gauge ya mtandao wote wa reli kusini mwa Afrika kuanzia Zambia hadi Cape Town. TAZARA iliunganishwa na mtandao huu kwa kusudi maalum. Ni kampuni binafsi ya GAUTRAIN ya Afrika ya Kusini pekee ndio yenye mtandao wake wa SGR ndani ya nchi hiyo kwa huduma ya abiria.

Bila shaka naamini ulitaka kusema miundombinu ya TAZARA iimarishwe na njia kuwekewa umeme lakini si kuibadilisha kuwa SGR. Lengo la uzi lingepotea.
 
Mambo mazuri na ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya nchi yanapangwa na kuchagizwa na sheria zilizo bora kabisa. Mambo yote haya yanapangwa na viongozi wa kisiasa kwa kufuata ushauri wa wataalam.

Badly enough; kule Bungeni viongozi wapo bize kuwarushia Mbowe na CDM vijembe na kusahau kilichowapeleka Bungeni.
Unakaa unajiuliza kwanini Mizigo mingi inapitia Zambia kuingia Congo? kwamba miaka yote serikali inashindwa kujenga Bandari na kuweka Meli kubwa hapo ziwa Tanganyika?
Miaka mingi barabara ya TABORA-SIKONGE-MPANDA imekua tabu kwelikweli.
Barabara ya TABORA-KALIUA-NJIAPANDA YA UVINZA-MPANDA nako tabu tupu.

Alafu wengine wakaenda mbali zaidi wanajenga daraja la Salander kweli? wakajenga uwanja wa ndege pale Chato kweli?
Wakajenga Lami kutoka Namanyerere adi kibaoni kwao Pinda kweli? na umuhimu wa kuunganisha Katavi..Tabora na Congo inazidi umuhimu wa Salander na Chato Airpot.

Majuzi nilikua pale boarder Kasumulu Kyela na Malawi; sasa unajiuliza boarder inajengwa alafu barabara imebaki nyembamba kama mkia wa kiboko.
Viongozi wetu jirekebisheni muangalie kinachoweza kuungamisha fursa kwa wananchi wetu.
Chato ata mabasi ya abiria yenyewe hawapati wasafiri itakua ndege?
👏👏👏 Ulivyoanza kulizungumzia hili kwa kulinganisha ndio umenifumbua macho, mitazamo yenye fikra pana namna hii ndio inayobadilisha mambo makubwa kuwa mazuri na kwa muda mfupi, inshallah natamani uzi huu uonwe na wenye vyeo vyao.
 
Ebu fikiria Lami inayoishia Kibaoni kwao Pinda unaweza kukaa bale barabarani masaa zaidi ya matatu bila kuona gari wala pikipiki ikipita kwenye hiyo barabara...unajiukiza ilijengwa kwasababu Pinda ni Waziri mkuu?

Je barabara na daraja lililokua linaunganisha Tabora na Katavi imelaza watu njiani miaka mingi sana. Sehemu ya masaa matano watu wanakaa siku mbili barabarani na ni njia ya kufungua uchumi wa nchi na nchi achilia mbali mkoa kwa mkoa.
Ukibahatika kutembea ndani ya nchi hii unaweza kushangaa mengi sana.

Chukulia ile boarder ya kuunganisha Kenya na Tanzania upande wa Rorya - Shirati. Upande wa Kenya wamejenga majengo yao vizuri na wanakusanya mapato ila upande wa Tanzania shida kwelikweli. Licha ya ushauri uliokwisha tolea na ofisi ya CAG kuhusu ujenzi wa hizi boarder.
 
Sometimes nafikiria soln ni radical amendment kwenye utawala mzima, yaan nchi izaliwe upyaaaa!
Maana madudu yapo mengi mnoo na kwa viongozi dawa yao ndio hiyo fyeka fyeka kila kitu ila kwa wananchi sio sana coz baadh hawana elimu ambapo wakielimishwa mambo yanakuwa sawa ila kwa wasomi-viongozi ambao ni stiff-necked na waroho soln ni radical eradication shenz, mi nachukiaga kabisa!
 
Back
Top Bottom