PostGE2025 Rais Samia: Kheri ya miaka 64 ya uhuru wa nchi yetu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,493
Reaction score
14,907
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatakia kheri ya sikukuu ya Uhuru Watanzania kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii.

1765277338547.png
Rais Samia amesema 'Kheri ya Miaka 64 ya Uhuru wa nchi yetuTunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hatua hii kubwa. Tunapoadhimisha siku hii muhimu, tukumbushane umuhimu wa kuendelea kulinda tunu za Taifa letu za amani, umoja na mshikamano. Tunu hizi ndizo msingi wa mafanikio ya safari yetu ambayo ni mfano wa kipekee Afrika na dunia kwa ujumla' - Rais Samia.

Rais Samia ameongeza kwa kusema 'Matunda ya Uhuru wetu yanaendelea kudhihirika katika uwezo wetu wa kuamua, kupanga na kutekeleza mipango yenye manufaa kwa wananchi na yenye kulinda maslahi ya Taifa letu. Haya ndiyo matunda ambayo waasisi wa Taifa letu waliyapigania na ambayo daima tutayalinda'

Na mwisho amesema 'Tuufurahie, tujivunie, tuulinde na tuuthamini Uhuru wetu. Mungu Ibariki Tanzania.' - Rais Samia.

1765277373014.png
 
Puuzeni hizo salamu hiyo picha yupo juu ya gari ni ya zamani😏
 
Comments ipo wazi au kafunga, nika msalimie mama mzuri mzuri
 
Wametuzuia hata kusogelea Mnazi Mmoja, sehemu tuliyopokea na kuadhimisha uhuru wetu kwa mara ya kwanza.

Tunaambiwa Heri ya Uhuru wakati jina la Tanganyika, nchi iliyopata huo uhuru, hawataki hata kulitaja.

Maisha ya kinafki sijawahi kuyakubali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatakia kheri ya sikukuu ya Uhuru Watanzania kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii.

Rais Samia amesema 'Kheri ya Miaka 64 ya Uhuru wa nchi yetuTunamshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hatua hii kubwa. Tunapoadhimisha siku hii muhimu, tukumbushane umuhimu wa kuendelea kulinda tunu za Taifa letu za amani, umoja na mshikamano. Tunu hizi ndizo msingi wa mafanikio ya safari yetu ambayo ni mfano wa kipekee Afrika na dunia kwa ujumla' - Rais Samia.

Rais Samia ameongeza kwa kusema 'Matunda ya Uhuru wetu yanaendelea kudhihirika katika uwezo wetu wa kuamua, kupanga na kutekeleza mipango yenye manufaa kwa wananchi na yenye kulinda maslahi ya Taifa letu. Haya ndiyo matunda ambayo waasisi wa Taifa letu waliyapigania na ambayo daima tutayalinda'

Na mwisho amesema 'Tuufurahie, tujivunie, tuulinde na tuuthamini Uhuru wetu. Mungu Ibariki Tanzania.' - Rais Samia.

Mbona mnatumia nguvu nyingi sana kuposti picha za zamani,tunaomba atuutubie hata kwa dakika 5 tu
 
Kama kwenye hizo tunu hakuna HAKI mwambie akampikie mumewe kama anaye.
Mtawala wa kwanza katika historia ya Tanganyika kuwafungia raia ndani siku ya kumbukumbu ya uhuru wa tanganyika!
Aibu
 
Back
Top Bottom