Rais Samia karibu Nchini Malawi Ujifunze Demokrasia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,755
218,369
Rais wa Tanzania yuko Nchini Malawi kwa ziara ya kikazi , ni bahati nzuri kwake kwamba kwenye nchi hiyo tumo siye Watanzania ambao ni Wafanyabiashara wa miaka mingi nchini humo , kwa kifupi ni kwamba Mgeni huyu amepata wenyeji wake.

Ni bahati nzuri kwamba Rais huyu ametembelea Malawi katika kipindi hiki ambacho nchini mwake (Tanzania ) kuna matatizo makubwa ya kidemokrasia yanayochagizwa na KATIBA MBOVU, tunaamini kwamba ujio wake kwenye nchi hii yenye Demokrasia ya kutukuka kutambadilisha na kumsukuma ili wiki ijayo atangaze kuitambua Rasimu ya Warioba iliyotokana na maoni ya Wananchi wakena kuirasimisha ili iwe Katiba ya Tanzania .

Labda kwa faida ya Wanajf na wengine ni kwamba , Nchini Malawi hakuna mungu mtu , wala hakuna Maagizo kutoka juu , hii nchi haina kamati ya Mizengo Pinda wala kikosi kazi cha Mukandara , hakuna watu wasiojulikana wala Polisi wanaohifadhi kura za watawala kwenye mabegi kama alivyofanya Lazaro Mambosasa na kutunukiwa Ukuu wa Chuo cha Polisi Kurasini , hii ni nchi ya kidemokrasia haswa ambayo mamlaka yake inatokana na Raia wenyewe , kwa Malawi Ukishachaguliwa ukiona Chama chako kimejaa wezi Unaruhusiwa kuhama chama na Urais Wako , hii ni kwa sababu Wamalawi hawachagui Vitambaa vyenye nembo za Jembe na Nyundo , Wanachagua mtu anayefaa .

Demokrasia ya Malawi ni pana sana kiasi cha kuwasahaulisha hata wananchi wake dhiki walizonazo , Tunaamini Rais wetu utarudi nchini kwako na kitu fulani .

Mungu Ibariki Malawi .
 
Kuondolewa kwa Humphrey Polepole kwenye Ubalozi nchini Malawi , angalau inaonyesha kwamba Malawi imeheshimiwa
 
Malawi asili ya kina Karume.

Wazanzibari wanaipenda Malawi kuliko Tanzania.

Miaka ile JK alitaka kuzipiga na Malawi zenji ilijiandaa kuwa upande wa Malawi japo propaganda ilikuwa hivyo au japo wangepenyeza humo humo kuvunja Muungano. (Nuneni tu).
 
Kama mnasema mnafanya ziara za kimkakati basi mkakati wa ziara hii uwe Demokrasia
 
Back
Top Bottom