Rais Samia kama hujamtoa Sabaya hayo maridhiano yako hayana maana yoyote kwa wana CCM

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Rais sijui ana nongwa gani na kijana Sabaya. Kazi aliyofanya Sabaya kwa CCM halafu anakomolewa na Serikali ya CCM ni jambo la kushangaza. Anachokitafuta Rais Samia ndani ya CCM ni kukiangamiza chama tu.

Mtu kama Lema na itikadi zake za ubinafsi unajidai kumpenda ili alete nini CCM? Watu wabinafsi wenye sera ya ulafi ujambazi wana faida gani CCM? Sabaya amepambana kuimarisha chama kwa vitendo. Ameonesha kutetea maslahi ya umma hadi kuhatarisha maisha yake.

Nani anabisha kama jimbo la hai mbowe alikuwa analishikilia kwa vitisho na hila dhidi ya wapinzani wake. Aligeuza kama mali yake na yeye ndio Sultani. Leo hii Sabaya anateseka kwa kulipwa kisasi na hao mafisadi kwa kusaidiwa na dola.

Licha ya Mahakama kumkuta hana kosa dola ya Rais Samia bado inaendelea kumshikilia kijana mfia CCM huku ikiwakumbatia wenye sera na itikadi za ubinafsi na juzi lema ameanza kuwakejeri vijana kwa ajira zao halali za bodaboda.

Urafiki na wahuni na wababaishaji hauwezi kumsaidia kwenye siasa za Tanzania. CCM msingi wake ni kutetea maslahi ya umma na sio kuwafutia kesi wakimbizi bandia na vibaraka wa mabeberu.

Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kwa kiongozi anayetokana na chama cha mapinduzi.

#Aliyekutwa na kesi ya kujibu na mahakama yuko nje ,aliyekutwa hana hatia na mahakama yuko ndani! Only in Tanzania.
 
Nakijua haka kakikundi ka kumtetea Sabaya,kimejaa vijana ambao wana mihemko ya kipumbavu na wengi wao walikuwa wanalipwa buku saba enzi zile za Polepole..kuna muda walisakwa wote wakaswekwa ndani naona wametolewa wanarudirudi sasa
 
Uzi wa ovyo kabisa huu kuwai kutokea, uyo sabaya unayemtetea kaumiza watu wangapi, yeye na wakina makonda walikuwa wanajua watakaa kwenye uongozi milele na walikuwa wanajua jiwe atakuwepo pale milele kama alpha na omega!! Sabaya anavuna alichopanda na kama anazo akili vizuri siku akitoka atakuwa amejifunza mengi na sidhani kama atakuja kurudia kufanya ushenzi aliowafanyia watu wasiokuwa na hatia.

Atakuwa amejifunza kwamba madaraka ni kama koti la kuazima uwezi kukaa nalo milele. Ivyo ukiwa nayo fanya yale yanayompendeza mwenyezi mungu utopungukiwa na kitu. Na wewe mtoa mada ni miongoni mwa wale wahafidhina aliowasema Mama Samia leo, na ni miongoni mwa wale wapuuzi waliokuwa wananufaika na utawala wa jiwe kwa namna moja ama nyingine. Uwexi kusimama bila aibu eti unamtetea Sabaya.

Anawajibika yeye mwenyewe kwa aliyoyafanya. Kama alikuwa anatumwa na jiwe au chama chake, alitakiwa kujiongeza akili za kuambiwa unachanganya na za kwako. Wacha afundishwe kwanza kuheshimu watu.
 
Sabaya kafungwa na wafanyabiashara aliowaibia mali zao samia hausiki.
Sabaya hajafungwa na yeyote. Mahakama imemkuta hana hatia kwanini awe jela? Kama kesi ya gaidi mbowe aliyekutwa na kesi ya kujibu na mahakama pia na ya muhuni lema zimefutwa kinyume na katiba ya sabaya ina tatizo gani? Huyu rais wa mpito atavuna anachopanda
 
Back
Top Bottom