mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Rais SSH akihitimisha mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC) uliofanyika jijini Dar es Salaam, amewaomba waandishi wa habari, na Taasisi zingine, wajipange kuwapokea waandishi wa habari wa kimataifa, kuanzia Septemba mwaka huu (2021).
Waandishi wa habari wa kimataifa wanakuja kumtangaza mama Samia pamoja na Taifa lake. Wamevutiwa Tanzania kwa kuwa na rais mwanamke.
Kuhusu mama Samia, Rais wa kwanza mwanamke Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa kauli yake mwenyewe, amenukuliwa akisema Wanataka kuiambia dunia kuwa kuna huyu (Rais Samia) maisha yake kaanza hivi kafika hadi hapa. Lakini changamoto anazokabiliana nazo katika kuongoza ni hizi, tukiwasaidia hapa na hapa hii nchi itafika hapa.
Kuhusu kuitangaza Tanzania, amewaomba watendaji wa taasisi na sekta ya habari nchini, ikiwemo ya usafiri na usafirishaji kuwa kazi yao iwe ni kutoa taarifa namna walivyojipanga na mipango ikoje. Pia, sekta biashara nayo ieleze ikoje, mipango yao, maeneo wanayotakiwa kuwekeza na malighafi inayopatikana.
Naamini kuna mengi ya kuiambia na kuionesha dunia. Hivyo basi, hata sisi wana mitandao ya kijamii tuandae mada za kuitangaza Tanzania wakati huo.