Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,510
- 7,755
Rais Samia leo wakati anazindua ujazwaji wa maji kwenye bwawa la kufua umeme la Mwl Nyerere amesema wakati wa awamu ya tano iliyokuwa inaongozwa na Hayati Magufuli pamoja na kwamba waliamua liwalo na liwe lakini akiwa makamu wa rais alishuhudia mikikimikiki mingi pamoja na hujuma mbalimbali zilizokuwa zinafanywa na watu ili kukwamisha mradi huo.!
Kwa kuwa taifa haliwezi kupona kwa kukaliana kimya na kusitiliana tunamuomba Rais Samia awataje hadharani wote waliokuwa wanashiriki kuhujumu mradi huo ili watanzania wawashughulikie na mbeleni isije ikajitokeza tena tabia kama hiyo. Haiwezekani tusomeshe watanzania kwa kodi zetu alafu wakishamaliza kusoma badala ya kuwasaidia watanzania wao wanaenda kuungana na mabeberu kuwanyonya na kuwaibia watanzania wenzao!!
Kuna shutuma mbalimbali kuwa akina Zito Kabwe, Mbowe, Lema ,John Heche, Nape Nauye, Tundu Lisu walikuwa wanahujumu mradi huu kwa lengo la kumkomoa Magufuli bila kujua kuwa huo ni mradi wa watanzania na siyo wa Magufuli.