Rais Samia, fedha za tozo ziundie chombo maalum cha kuendesha ujenzi -- achana na maono finyu ya wasaidizi wako

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Serikali imekusanya tozo ikatuambia kiasi kimefikia bilioni 48. Ni mwanzo mzuri. Lakini kilichonishtua ni namna zinavyokwenda kutumika; inauma Sana.

Matumizi yake katika ujenzi wa shule na zahanati yameelezwa yatajikita kwenye mfumo wa force account, naamini hapa ndipo tatizo la kupanga na kuchagua kwa maslahi ya Taifa lilipokosewa. Ntaomba niwawekea ufafanunuzi wa kina juu ya ninachoona mbele kuhusu mfumo huu.

Force account Ni mfumo wa ujenzi ambao Mwenye mradi (serikali) utoa fedha na rasilimali alizonazo kukamilisha ujenzi bila kuwapa tenda makampuni na bila kupita kwenye urasimu wa kisheria uliopo kwenye mfumo wa utangazaji tenda. Lengo kubwa la mfumo huu nikufanikisha mradi kwa muda mfupi na kwa kiasi kidogo Cha fedha.

Madhara ya mfumo huu nikukosekana kwa uwazi wa upatikanaji wa wataalamu na wakandarasi,kukosekana kwa mfumo wakupata suppliers, kukosekana kwa wataalamu wanaoweza kusimamia ubora na badala yake hoja kubwa huwa ni gharama ndogo kwa muda mfupi.

Katika nchi za ulimwengu wa tatu hasa nchi yetu Tanzania huu mfumo siyo mfumo sahihi kwa sababu zifuatazo:

1. Halmashauri zetu hazina wataalamu wakusimamia miradi hii
2. Wakurugenzi hawana utaaalamu wakusimamia miradi hii katika ubora ila wanaweza kusimamia katika gharama ndogo na muda mfupi bila kujali uimara wa mradi kwa miaka ijayo.

Lakini labda tujiulize Nini jukumu la serikali katika matumizi ya fedha za umma? Jukumu kubwa la serikali nikusimamia thamani ya fedha, ubora , muda, mchakato wa kisheria na kuepusha serikali kutumia fedha katika miradi ileile iliyokamilika muda mfupi katika eneo la matengenezo na ukarabati. Tanzania kwa miaka mingi tumeshindwa kusimamia standard katika miradi badala yake tumejificha kwenye kigezo Cha muda na gharama ndogo za mradi na hapa ndipo ilipozaliwa mtizamo wa force akaunti.

Labda Sasa nieleze Ni katika mazingira gani nakubaliana na mfumo wa force account na mazingira gani nakubaliana nao.
Napingana na mfumo huu kwa kuzingatia utumaji fedha kwa wakurugenzi ambao hawana uwezo wakuifanya kazi hii kitaalamu ikawa na ufanisi kwa miaka hamsini mbele. Napingana na mfumo huu pale ninaposoma tangazo la serikali kuhusu components za kituo Cha afya kinachojengwa.

Napingana na utaratibu wa serikali kwa kuangalia aina ya uadilifu walionao Watumishi wa umma katika nchi hii, lakini napingana na utaratibu kwa kuangalia nguvu ya wanasiasa kuamua Nani apewe mradi gani.Mwisho napingana na utaratibu uliotangazwa na serikali kutokana na kuona fedha zinatawanywa nchi nzima at once na si kwa maeneo machache na kwa awamu ambapo awamu hii ikikamilika tunahamia awamu nyingine.

Nakubalina na utaratibu wa force akaunti endapo tutafuata kidogo wazo la TANROADs au TARURA au REA katika kutekeleza miradi hii tunayotaka kuanza ya shule na vituo vya afya.

Nini maoni yangu
1. Naomba serikali isipeleke fedha kwa wakurugenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi tutatumia fedha hizi vibaya.

2. Kwa kuwa fedha tunazo na tutazidi kuzikusanya, tusijikite kujenga shule na vituo vya afya kwa kusambaza pesa nchi nzima. Tuunde chombo chakitaaluma chakusimia miradi ya ujenzi ya shule na vituo vya afya nchini ambacho chombo hicho kitahusika kupanga, kufanya tathimini na kuratibu ujenzi kwa kuzingatia kiasi Cha fedha kilichopo.

3. Endapo kuunda chombo hiki itachukua muda na kwa ajili ya kupunguza gharama za tenda na muda wa mradi niombe wizara iwape miradi hii shirika la nyumba la Taifa au JKT wasimamie ujenzi na wasiende halmashauri zote waende halmshauri chache na wakikamilisha waende sehemu nyingine. Hi plan imesaidia Sana ujenzi wa barabara nchini, tungewaachia wakurugenzi wakujenga barabara Leo tusingekuwa hapa tulipo lakini kupitia TARURA NA TANROADS tunaona mipango ya ujenzi kwa miaka mia mbele.

4. Chondechonde, tuondoe kabisa utaratibu wakujenga majengo badala yakujenga kituo Cha afya au shule. Tunapozungua kituo Cha afya tunazungumzia jengo la huduma lenye kiwango na sifa,tunazungumzia kichomea taka chenye ubora na tunazungumzia makazi ya wafanyakazi. Mwalimu nyerere alijenga miaka ya 1960, wakoloni walitujengea vituo vya afya, nyumba za reli na vituo vya polisi nadhani tujifunze. Kama mwaka 1960 watu waliona thamani yakuunganisha huduma na makazi ya watoa huduma Leo hii hizi mentality zakujenga vituo vya afya kwa viwango vya nyumba za watu huku tukitumia fedha za umma tunatoa wapi? Tujenge majengo ya serikali kitaalamu tuachane na masuala yakutumia fedha za umma kwa wishes na maono binafsi.

5. Baada ya kuunda chombo, au kutumia NHIC, au kutumia JKT miradi hii usimamiwe na wakurugenzi, wakuu wa Mikoa lakini ikaguliwe na CAG kusimamia ubora.

6. Mhe. Rais pls waelekeze mawaziri wako waache miemko na fedha za umma. Mtamaliza miaka kumi majengo haya yote yamebomoka tutaanza kujenga upya. Tujenge majengo kwa standard za miradi ya Kitaifa tuache maono ya kutoa milioni Mia mia kwa wakurugenzi kwa malengo yakisiasa yakuwaambia wananchi tumejenga majengo mia tujikite kwenye quality.

Mnaosimamia kususa pigeni kelele kuzuia fedha hizi kupelekwa kwa watu wasio na taaluma za ujenzi kwa malengo ya kisiasa.
 
Wakikusikia na wakachukua point hata moja, mshukuru Mungu kwa hilo, kwani Hadi sasa wapo walioanza kunoa matumbo yao kwa ajili ya ulaji wanaotarajia kupata kutoka mo, kwenye miradi na mahela tajwa.
 
CAG akikagua kinachofuata no kumwona miongo anabambika, ana ajenda ya Siri, anawalima watawala alafi Mambo yanatupwa kule
 
Umefafanua vyema Sana, kwa Miaka mingi tumekuwa tunatumia fedha za umma kwa kuzitawanya tawwnya na hakuna tija. Nakubaliana na wazo lakuunda chombo Cha kusimamia ujenzi wa majengo ya vituo vya afya na hospitali chenye meonekano wa kitaifa na kitakachopimwa kwa malengo ya kitaifa yaliyowekwa Kama ambavyo Leo hii TANROADS wanafanya......wana mpango wa barabara nchi nzima na hata wakitokea wafadhili au tukitaka kukopa tunajua tunakopa kwa ajili ya Nini.

Wabunge wachukue wazo lako wasimamishe usambazaji wa fedha kwa Wakurugenzi Hadi kiwepo chombo Cha kusimamia hizo fedha, chombo hicho kitakuwa na wataalamu na washauri. ..waalimu na watu wa afya watakuwa wanakabidhiwa majengo tu na kuanza kutoa huduma...lakini pia hata wabunge itawasaidia kukupiga debe kwa sababu watajua ujenzi au mpangokazi wa Jimbo upo vipi.

Great idea
 
Serikali imekusanya tozo ikatuambia kiasi kimefikia bilioni 48. Ni mwanzo mzuri. Lakini kilichonishtua ni namna zinavyokwenda kutumika; inauma Sana.

Matumizi yake katika ujenzi wa shule na zahanati yameelezwa yatajikita kwenye mfumo wa force account, naamini hapa ndipo tatizo la kupanga na kuchagua kwa maslahi ya Taifa lilipokosewa. Ntaomba niwawekea ufafanunuzi wa kina juu ya ninachoona mbele kuhusu mfumo huu.

Force account Ni mfumo wa ujenzi ambao Mwenye mradi (serikali) utoa fedha na rasilimali alizonazo kukamilisha ujenzi bila kuwapa tenda makampuni na bila kupita kwenye urasimu wa kisheria uliopo kwenye mfumo wa utangazaji tenda. Lengo kubwa la mfumo huu nikufanikisha mradi kwa muda mfupi na kwa kiasi kidogo Cha fedha.

Madhara ya mfumo huu nikukosekana kwa uwazi wa upatikanaji wa wataalamu na wakandarasi,kukosekana kwa mfumo wakupata suppliers, kukosekana kwa wataalamu wanaoweza kusimamia ubora na badala yake hoja kubwa huwa ni gharama ndogo kwa muda mfupi.

Katika nchi za ulimwengu wa tatu hasa nchi yetu Tanzania huu mfumo siyo mfumo sahihi kwa sababu zifuatazo:

1. Halmashauri zetu hazina wataalamu wakusimamia miradi hii
2. Wakurugenzi hawana utaaalamu wakusimamia miradi hii katika ubora ila wanaweza kusimamia katika gharama ndogo na muda mfupi bila kujali uimara wa mradi kwa miaka ijayo.

Lakini labda tujiulize Nini jukumu la serikali katika matumizi ya fedha za umma? Jukumu kubwa la serikali nikusimamia thamani ya fedha, ubora , muda, mchakato wa kisheria na kuepusha serikali kutumia fedha katika miradi ileile iliyokamilika muda mfupi katika eneo la matengenezo na ukarabati. Tanzania kwa miaka mingi tumeshindwa kusimamia standard katika miradi badala yake tumejificha kwenye kigezo Cha muda na gharama ndogo za mradi na hapa ndipo ilipozaliwa mtizamo wa force akaunti.

Labda Sasa nieleze Ni katika mazingira gani nakubaliana na mfumo wa force account na mazingira gani nakubaliana nao.
Napingana na mfumo huu kwa kuzingatia utumaji fedha kwa wakurugenzi ambao hawana uwezo wakuifanya kazi hii kitaalamu ikawa na ufanisi kwa miaka hamsini mbele. Napingana na mfumo huu pale ninaposoma tangazo la serikali kuhusu components za kituo Cha afya kinachojengwa.

Napingana na utaratibu wa serikali kwa kuangalia aina ya uadilifu walionao Watumishi wa umma katika nchi hii, lakini napingana na utaratibu kwa kuangalia nguvu ya wanasiasa kuamua Nani apewe mradi gani.Mwisho napingana na utaratibu uliotangazwa na serikali kutokana na kuona fedha zinatawanywa nchi nzima at once na si kwa maeneo machache na kwa awamu ambapo awamu hii ikikamilika tunahamia awamu nyingine.

Nakubalina na utaratibu wa force akaunti endapo tutafuata kidogo wazo la TANROADs au TARURA au REA katika kutekeleza miradi hii tunayotaka kuanza ya shule na vituo vya afya.

Nini maoni yangu
1. Naomba serikali isipeleke fedha kwa wakurugenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi tutatumia fedha hizi vibaya.

2. Kwa kuwa fedha tunazo na tutazidi kuzikusanya, tusijikite kujenga shule na vituo vya afya kwa kusambaza pesa nchi nzima. Tuunde chombo chakitaaluma chakusimia miradi ya ujenzi ya shule na vituo vya afya nchini ambacho chombo hicho kitahusika kupanga, kufanya tathimini na kuratibu ujenzi kwa kuzingatia kiasi Cha fedha kilichopo.

3. Endapo kuunda chombo hiki itachukua muda na kwa ajili ya kupunguza gharama za tenda na muda wa mradi niombe wizara iwape miradi hii shirika la nyumba la Taifa au JKT wasimamie ujenzi na wasiende halmashauri zote waende halmshauri chache na wakikamilisha waende sehemu nyingine. Hi plan imesaidia Sana ujenzi wa barabara nchini, tungewaachia wakurugenzi wakujenga barabara Leo tusingekuwa hapa tulipo lakini kupitia TARURA NA TANROADS tunaona mipango ya ujenzi kwa miaka mia mbele.

4. Chondechonde, tuondoe kabisa utaratibu wakujenga majengo badala yakujenga kituo Cha afya au shule. Tunapozungua kituo Cha afya tunazungumzia jengo la huduma lenye kiwango na sifa,tunazungumzia kichomea taka chenye ubora na tunazungumzia makazi ya wafanyakazi. Mwalimu nyerere alijenga miaka ya 1960, wakoloni walitujengea vituo vya afya, nyumba za reli na vituo vya polisi nadhani tujifunze. Kama mwaka 1960 watu waliona thamani yakuunganisha huduma na makazi ya watoa huduma Leo hii hizi mentality zakujenga vituo vya afya kwa viwango vya nyumba za watu huku tukitumia fedha za umma tunatoa wapi? Tujenge majengo ya serikali kitaalamu tuachane na masuala yakutumia fedha za umma kwa wishes na maono binafsi.

5. Baada ya kuunda chombo, au kutumia NHIC, au kutumia JKT miradi hii usimamiwe na wakurugenzi, wakuu wa Mikoa lakini ikaguliwe na CAG kusimamia ubora.

6. Mhe. Rais pls waelekeze mawaziri wako waache miemko na fedha za umma. Mtamaliza miaka kumi majengo haya yote yamebomoka tutaanza kujenga upya. Tujenge majengo kwa standard za miradi ya Kitaifa tuache maono ya kutoa milioni Mia mia kwa wakurugenzi kwa malengo yakisiasa yakuwaambia wananchi tumejenga majengo mia tujikite kwenye quality.

Mnaosimamia kususa pigeni kelele kuzuia fedha hizi kupelekwa kwa watu wasio na taaluma za ujenzi kwa malengo ya kisiasa.
Balaa limeanza aisee
 
Kutakuwa na vyombo vingapi vya ujenzi,acha ujinga wewe.Halmashauri zina vitengo vya ujenzi Kazi yao ni ipi? Tba,Suma jkt, TARURA,Tanroads nk nk
 
Back
Top Bottom