Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya miradi kuchelewa, ambapo hivi karibuni kisingizio kimekuwa ni janga la COVID19
Amesema hayo baada ya kuzindua gati namba 0 hadi 7 katika Bandari ya Dar es Salaam. Ameeleza, kwa sasa COVID-19 tumeshaizoea hivyo ni muhimu kujifunza kuishi nayo isiwe tena kigezo cha miradi kuchelewa