Ukoloni ni unyama. (voice of Samora Machel)
MAPAMBANO YANAENDELEA (STRUGGLE) ALUTA CONTINUA DHIDI YA WALIOHODHI MADARAKA BAADA YA 'UHURU'
Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra, Ukoloni Hauna Rangi
View: https://m.youtube.com/watch?v=Omh25kcA1Lw
Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona
m-bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.
Samora Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.
Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.
Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.
Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.
Samora Machel anakumbushia kuwa Mozambique walipambana na ukoloni mkongwe wa miaka 500 wa Mreno uliokuwapo Mozambique, na kama kawaida pamoja na umasikini wa taifa la Portugal barani ulaya,lakini walikuwa wakoloni kama wakoloni wengine.
Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.
N.B
Kiongozi wa kwanza wa Mozambique alikuwa rais Samora Moises Machel aliyekuwa kiongozi wa chama kilichoongoza mapambano cha FRELIMO dhidi ya utawala mkongwe wa Ureno uliodumu miaka 500.
FRELIMO ilikuwa na makao yake makuu jijini Dar es Salaam na kambi za wapiganaji huko Kongwa Dodoma na pia FARM 17 mkoani Mtwara nchini Tanzania ambapo wapiganaji wa FRELIMO walijipenyeza kuanza mapambano ya kuungoa utawala mkongwe wa Mreno kwa kuanzia mkoa wa Capo Delgado kaskazini ya Msumbiji
Samora Moises Machel kiongozi mcheshi (charismatic), hotuba zake za hasama hadi leo kizazi hiki zinasilizwa kwa kuwa zililenga kuwa na mtu huru kifikra. Moja ya hotuba yake motomoto hapo juu.