nyonyodawa
Member
- Nov 11, 2024
- 40
- 122
Kwa wanaofuatilia siasa za Mozambique, hali ni mbaya kwa chama tawala cha Frelimo pamoja na serikali iliyoko madarakani. Baada ya uchaguzi kuisha na serikali kujitangaza kushinda kwa wastani wa asilimia sabini, wananchi wameikata, wakiongozwa na kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane.
Kinachotokea sasa hivi ni kwamba huyu kiongozi wa upinzani ndiye mwenye nguvu na sauti kuliko serikali; yeye ndiye anayeamuru nini kifanyike. Anaratibu maandamano akiwa mafichoni, baada ya kukimbia nchi kufuatia mauaji ya wakili wake.
Hali si shwali. Mfano jana, ameamrisha kufanyika maandamano kwa siku tatu bila kupumzika, akilenga bandari kufungwa pamoja na mipaka. Kumeitikiwa kwa muitikio mkubwa katika miji yote mikubwa ya Maputo, Beira, na Nampula pamoja na miji mingine midogo, huku karibu watu 40 wakiwa wameuwawa na polisi.
Inchi inaongozwa na mtu aliyeko mafichoni, huku Rais Nyusi akiwa hana sauti. Ukiona mwenzako ananyolewa.
Soma, Pia: Yanayojiri kwenye Uchaguzi Mkuu wa Msumbiji: FRELIMO (Chama rafiki ya CCM) kushinda Uchaguzi 09 Oktoba?